Watumishi hewa: Kompyuta yenye rekodi yaibwa, wakopa benki kwa majina hewa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe, Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uandaaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.

Akizungumza kando ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Kaimu Mhazini wa Halmashauri hiyo, Baraka Munuo alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Mwanza, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.

”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Wakati huo huo, MSAKO ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.

Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.

Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.

Akizungumza jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege. Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.
CHANZO: Habarileo
 
Zoezi la Wafanyakazi hewa kwa sasa ni kaa la moto kwa viongozi wakuu.

Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela ambaye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa karibu sana na Rais Magufuli imekuwa kama benchmark kwa Wakuu wa Mikoa hata wale waliokuwa wamezoea business as usual.

Swali la kujiuliza kwa sasa, ina maana wale Wakuu wa Mikoa ambao wamekuwepo tokea kwenye awamu ya nne hawakufahamu kama kulikuwa na wafanyakazi hewa katika Mikoa yao?

Nini kimewabadilisha kiasi kwamba kwa sasa wanaonekana very active kuhakikisha Mikoa yao haina wafanyakazi hewa?

Yanayoibuka katika zoezi hili yanatuambia kuna watumishi ambao walifanya wizi ni sehemu ya majukumu yao kikazi.

Kadri zoezi linavyofanyiwa uchunguzi zaidi ndivyo wafanyakazi hewa wanazidi kuongezeka.

Tutaona na kusikia mengi kwenye hili zoezi la wafanyakazi hewa!
 
Tone at the top!!
 
Bi kijo simba haki za binadamu zilindwe hao wezi waheshimiwe kutimiza haki za binadamu
 
Server pia imeibwa. Hakuna kurudi nyuma. Tunaunga mkono juhudi za Mr President JPM. Juhudi zenu za kunkatisha tamaa hazitasaidia kitu
 
Wananikumbusha ile CCM ya zamani ambayo haikutaka kusikia neno ufisadi kutoka CHADEMA.

Kwa sasa CHADEMA haitaki kusikia neno Ufisadi au wabadhilifu wa mali ya umma wakishughurikiwa.
Jamaa wanachekesha sana wao ndiyo walikuwa wasemaji wakuu wa ufisadi eti leo hawauoni ajabu na kweli.
 
Mhasibu wa
Halmashauri ya Wilaya ya
Singida, Imani
Nyamangaro, alipandishwa
kizimbani akidaiwa kujilipa
mishahara ya wastaafu 57,
yenye thamani ya Sh
milioni 29.4.

#####################
 
Daa hivi watendaji wote wa serikali awamu 4 wanajisikiaje? Mwigulu nae aliwahi kujisifia kuwa atakomesha wafanyakazi hewa akiwa naibu waziri! Sikumuelewa aliposema amedhibiti!! JK alikuwa rahisi kuliko Rais!
 
Wananikumbusha ile CCM ya zamani ambayo haikutaka kusikia neno ufisadi kutoka CHADEMA.

Kwa sasa CHADEMA haitaki kusikia neno Ufisadi au wabadhilifu wa mali ya umma wakishughurikiwa.
MsemajiUkweli sina mashaka na uelewa wako. Najua mengine unaandika kwa ushabiki tuu wa kisiasa. Naomba nikwambie kitu kimoja na naomba ukiweke kwenye kumbukumbu zako.
Athari za kuchukulia matukio haya ya kijinai kwa mtindo wa kukurupuka kisiasa zitaleta shida na kutukosesha mengi kwani kesi nyingi serikali itapoteza mahakamani kwani hazitajengewa hoja nzito. Jee hilo litakuwa limetunufaisha? Ndio maana tunasema uhalifu huu usichukuliwe kama kutumbua majipu kisiasa bali vyombo husika vifanye operation ya kisayansi ya kupambana na jinai hizo hapo ndio tutashinda.
Good day to you
 
Mkuu MsemajiUkweli sasa ndio naamini zoezi la watumishi hewa linatekelezwa na kuthibitisha hili si unaona madudu yanatokea ofisi za uhasibu na idara za utumishi sio kipindi kile walikuwa wanatuletea maigizo tu ya kutuletea taarifa za walimu walio masomoni.
 
Huyo jamaa anaitwa baraka abanwe vizuri asema komputer zimeenda wapi alikuwa alikuwa anakaimu DT hapo UKEREWE sasa kwa muda mfupi tu miaka miwili amenunua xtrail mpya ameshaajinga mwanza ,na viwanja kibao kule buhongwa ,
Kijamaa flani kina nyodo sana waseme komputer za EPICOR zimeenda wapi
 
Zoezi la Wafanyakazi hewa kwa sasa ni kaa la moto kwa viongozi wakuu.

Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela ambaye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa karibu sana na Rais Magufuli imekuwa kama benchmark kwa Wakuu wa Mikoa hata wale waliokuwa wamezoea business as usual.

Swali la kujiuliza kwa sasa, ina maana wale Wakuu wa Mikoa ambao wamekuwepo tokea kwenye awamu ya nne hawakufahamu kama kulikuwa na wafanyakazi hewa katika Mikoa yao?

Nini kimewabadilisha kiasi kwamba kwa sasa wanaonekana very active kuhakikisha Mikoa yao haina wafanyakazi hewa?

Yanayoibuka katika zoezi hili yanatuambia kuna watumishi ambao walifanya wizi ni sehemu ya majukumu yao kikazi.

Kadri zoezi linavyofanyiwa uchunguzi zaidi ndivyo wafanyakazi hewa wanazidi kuongezeka.

Tutaona na kusikia mengi kwenye hili zoezi la wafanyakazi hewa!
Kama mfumo mzima ni corrupt usitegemee mtu mmoja kufanya mabadiliko. Sasa hivi yametokea mabadiliko ya kimfumo ambapo lazima uchape kazi au mfumo ukuteme kama alivyotemwa Anna Kilango...

Serikali ya awamu ya nne ilikaribisha wezi hadi Ikulu, serikali ya awamu ya tano imetumia muda wake wote toka imeanza kufukuza wezi tu. Hapa mambo mengine ya maendeleo yanasubiri wezi hawa waondoshwe. Hatua moja nyuma lakini muhimu kupata base nzuri
 
MsemajiUkweli sina mashaka na uelewa wako. Najua mengine unaandika kwa ushabiki tuu wa kisiasa. Naomba nikwambie kitu kimoja na naomba ukiweke kwenye kumbukumbu zako.
Athari za kuchukulia matukio haya ya kijinai kwa mtindo wa kukurupuka kisiasa zitaleta shida na kutukosesha mengi kwani kesi nyingi serikali itapoteza mahakamani kwani hazitajengewa hoja nzito. Jee hilo litakuwa limetunufaisha? Ndio maana tunasema uhalifu huu usichukuliwe kama kutumbua majipu kisiasa bali vyombo husika vifanye operation ya kisayansi ya kupambana na jinai hizo hapo ndio tutashinda.
Good day to you
Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa.

Naomba pia uelewe kuwa katika nchi yetu, Rais ni kila kitu.

Serikali ilikuwa inashindwa kesi mahakamani kwa sababu katika utawala uliopita, Rais alikuwa ameziachia mahakama nafasi hata ya kupokea rushwa.

Utawala wa Awamu ya nne ulikuwa hauchukii pale serikali inaposhindwa mahakamani na kwa sababu hiyo hata mawakili wa serikali wakawa mawakala wa watuhumiwa.

Mawakili wa serikali walikuwa wanatengeneza maksudi mashitaka dhaifu yenye mlengo wa kushindwa mahakamani baada ya kupokea rushwa.

Take my word, Kwa sasa serikali itakuwa inashinda kesi nyingi.
 
Ukipiga mahesabu utakuja kugundua kuwa pesa nyingi sana iliishia mifukoni kwa watu.
Hili lilikuwa ni janga la taifa!

Tumepoteza hospitali ngapi au vifaa vingapi vya kufundishia watoto wetu mashuleni kwa pesa hizi.
 
Back
Top Bottom