Watumishi hewa: Kompyuta yenye rekodi yaibwa, wakopa benki kwa majina hewa

Asisahau pia na mawaziri pamoja na manaibu wao, hawa jamaa wanamishahara na posho mbilimbili za ubunge na uwaziri.
Kubana matumizi kwa sera ya serkali aondoe kimoja.
 
Watumishi hewa Ni mtandao mrefu sana,kuumaliza huu mtandao ilitakiwa kufuatia hata miaka ya nyuma kuliko kuangalia mwaka huu mmoja lakini hawa wahusika walikuwa wanatoaje pesa benki bila kushirikiana Na watu wa benki ? Serkali ikifuatilia vizuri wezi Ni wengi Na watakamatwa mtu mmoja hawezi kuchukua mishahara mingi benki wasijue au jamii nifafanulieni
 
Computer systems zote huwa zina server hata nne tofauti na zinakuwa katika nchi tofauti tofauti, au hawakuweka online backup?!
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe, Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uandaaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.

Akizungumza kando ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Kaimu Mhazini wa Halmashauri hiyo, Baraka Munuo alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Mwanza, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.

”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Wakati huo huo, MSAKO ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.

Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.

Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.

Akizungumza jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege. Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.
CHANZO: Habarileo
hivi kwani hakuna back up
 
Daaah nimecheka sana, ni kweli nampata huyo Dogo, alikuwa anaendesha pikipiki flan hivi ki 110.
Kumbe alikaimishwa udt? Namuona fb na picha zake akila bata Mwanza town.
Alitakiwa amtafute mtaalamu mtasiwa amfudishe jinsi ya kupiga.

wew sasa anayo xtrail mpya kabisa
 
Hao walioiba computer moja nadhani wamejisumbua tu. Maana kwa utaratibu wa hiyo system huwa wanapeleka backup hazina. Kwahiyo alichotaka kisijulikane kitakuwa hazina.
 
wew sasa anayo xtrail mpya kabisa
aisee amejitahidi, ndio maendeleo yenyewe. sasahivi maofisini watu wamekaa kiupigaji zaidi, watu wanakopa mikopo benki kuficha upigaji.
Namjua sana huyo kijana, wewe upo huko nini?
 
Fox should be chased away first then the hen warned wandering into the bush....ni bora tukitumia mwaka mzima huu kusafisha nchi kutokana na madhila ya wizi,ufisadi,rushwa na uzembe kazini uliojengeka na serikali ya awamu ya 4,baada ya hapo tuanze kuijenga nchi ikiwa na watendaji safi,inaumiza sana kundi la watu wachache waliopata nafasi za kiutendaji wakifuja mali huko wengi wakibaki "malofa"
 
Back
Top Bottom