Watumishi hewa 515 wagundulika katika mikoa mitatu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Siku 15 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa Wakuu Wapya wa Mikoa kuhakikisha wanawabainisha na kuwaondoa wafanyakazi hewa zimeanza kutoa picha kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa nchini.

Mpaka sasa imebainika kuna wafanyakazi 515 katika mikoa mitatu ambayo ni Kigoma (169), Dodoma (144) na Singida (202).

Taswira hii inaonyesha jinsi ambavyo tatizo la wafanyakazi hewa linaweza kuwa ni kubwa zaidi ya ilivyofikiriwa hasa ikichukuliwa limekuwepo kwa muda mrefu huku mamilioni ya pesa za walipa kodi yakienda kwenye mifuko ya wajanja wachache.

Inakadiriwa serikali ina wafanyakazi zaidi 500,000 na inalipa mishahara takriban Sh. bilioni 549 kwa mwezi, ambayo kati ya fedha hizo kuna malipo ya wafanyakazi hewa.

Katika repoti yake ya mwaka 2013/14, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha kuna zaidi ya Sh141.4bn zimelipwa kwa wafanyakazi hewa katika mwaka wa fedha.

======================================================
Mdau mmoja ametoa angalizo muhimu kuhusu kinachoendelea kwenye zoezi la kuhakiki wafanyakazi ambapo amesema;
Mwingine amesema/ameandika hivi;
 
Kwa mtaji huu haishangazi kuona nusu ya makusanyo kitaifa yanatumika kulipia mishahara ya watumishi wa serikali.

Haishangazi kuona gap la wenye nafasi za kupiga dili kama hizi (accumulation of dubious wealth) lilikuwa linapanuka kwa haraka ukilinganisha na wasio na nafasi.

Kazi iliyoko mbele ya Rais Magufuli ni pevu. These are high pressure situations and he has to keep a cool, calm and collected head, otherwise he'll go nut.

Hii nchi ina maajabu na vituko!
 
Ndo maana wakati wa Kikwete nchi ilifika hatua imenock, system ilifail kabisa.

Haya yote unaoyaona na matokeo ya Kikwete kuanzisha system ya kuyabaini hayo, jisomee:

Katika repoti yake ya mwaka 2013/14, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha kuna zaidi ya Sh141.4bn zimelipwa kwa wafanyakazi hewa katika mwaka wa fedha.
 

Ok, then alichukua uamuzi gani mgumu wa nkutatua hizo kero zaidi ya kuishia kwenye report zenu hizo magumashi.
 
Tatizo la ajira serikalini/mashirika hapa Tanzania sio tu wafanyakazi hewa. Kuna wale ambao naweza kuwaita viongozi wasio na umuhimu. Kwa mfano kila mkoa una utitiri wa vyeo vinavyoenda sambamba na mkuu wa mkoa. Kwenye wilaya ni hivyo hivyo. Na zaidi mimi nadhani wakuu wa wilaya hawana umuhimu wowote. Ukirudi kwa wabunge ni wengi sana. Bila kufumua system nzima na kubaki na viongozi wachache hatutafika mbali.
 
Ningemwita Kikwete shujaa angetuambia Escrow ya nani na nani alihusika, bila kupepesa na kwa kumuogopa Mungu from his heart.
 
Serikali iwabane wakuu wa idara,hilo lilikuwa chaka lao la kujipatia malipo ya ziada.Wapewe pay roll wabainishe kituo cha kila mtumishi,then waangalizi (TISS/TAKUKURU) wagawane japo Tarafa moja au kata kuhakiki kama watu hao wapo vituoni au nje ya kituo kwa taarifa,ndo watafahamu ukubwa wa tatizo.
Zichukuliwe hatua kali dhidi ya wakuu wa idara walioisababishia serikali na watanzania hasara kubwa.
 
Angalizo lako ninakubaliana nalo 101%

Hakuna kitu kinachonichukiza kama kuwa na bunge lenye wabunge wa viti maalum ili tu kuweka uwiano katika jinsia. Haya ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.
 
Idadi hiyo ya mikoa mitatu umeitoa wapi mbona haiko kwenye taarifa ulioambatisha????????? @ msema ukweli??
 
Ndio maana watumishi wanapenda kuajiliwa serikali ata kama mshahara mdogo wanafikiria kwenda kuiba maana walio ndani wanajitamba sana mitaani na wao wanafikiria kuiba na kugushi nyalaka mwenyezimungu awalaani.sisi huku vifaa na DAWA Hanna wazee wanakufa kwakukosa dawa
 
Shikamoo Bibi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…