Tetesi: Walimu hewa Manispaa ya Kinondoni

Tanaluza

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
212
121
Kufuatia zoezi la kuhakiki watumishi hewa katika taasisi za uma. Baadhi ya walimu wa Manispaa ya Kinondoni waliofukuzwa kazi miaka 5iliyopita kwasababu mbalimbali juzi waliitwa kwenye zoezi la uhakiki ili kuthibitisha kwamba wao ni walimu halali waliojariwa na Manispaa na walikuwa wakipokea mishahara yao kwa muda wote waliofukuzwa jambo ambalo si kweli. Walimu hao walifukuzwa kazi na hawakuwa wakipokea mishahara yao kwa muda wote mpaka kufikia tarehe ya uhakiki.
 
Chanzo cha habari, weka vielelezo vya kutushibisha kama vipo.
 
U

UsHawahi kwendakitanda ulichozaliwa ukauliza nesi n hiki ama kile
Sijabahatika kuzaliwa kitandani wala mama alienizaa hakupata bahati ya kusaidiwa na nesi kipindi mimi nakuja hapa duniani, Je kwa swali lako hilo ndio linaondoa ukweli kuwa mtu akiweka tuhuma yake humu tusimuhoji chanzo cha taarifa yake bali tukubali kibubusa?
 
Uyo Mkurugenzi anaogopa kutumbuliwa sasa imekula kwake atakwenda na maji maana iyo ni forgery na kesi anafunguliwa as long as barua ya kuwatimua kazi ipo
 
Naomba kujuzwa wakati huo manispaa ya kinondomi ilikuwa ikiongozwa na meya kutoka chama gani na mkuu wa wilaya wakati huo Makonda alichukua hatua gani?
 
Kufuatia zoezi la kuhakiki watumishi hewa katika taasisi za uma. Baadhi ya walimu wa Manispaa ya Kinondoni waliofukuzwa kazi miaka 5iliyopita kwasababu mbalimbali juzi waliitwa kwenye zoezi la uhakiki ili kuthibitisha kwamba wao ni walimu halali waliojariwa na Manispaa na walikuwa wakipokea mishahara yao kwa muda wote waliofukuzwa jambo ambalo si kweli. Walimu hao walifukuzwa kazi na hawakuwa wakipokea mishahara yao kwa muda wote mpaka kufikia tarehe ya uhakiki.

Hoja yako hapa ni nini hasa?

Walimu waliokuwa wamefukuzwa walikuwa hawapokei mishahara yao au?

Kama ndivyo unatuambiaje sasa? Wangapi hao walimu? Hiyo mishahara yao ilikuwa inaenda wapi?
 
soma post vizuri utaelewa usikurupuke kucomment
 
Sijabahatika kuzaliwa kitandani wala mama alienizaa hakupata bahati ya kusaidiwa na nesi kipindi mimi nakuja hapa duniani, Je kwa swali lako hilo ndio linaondoa ukweli kuwa mtu akiweka tuhuma yake humu tusimuhoji chanzo cha taarifa yake bali tukubali kibubusa?
Kutosaidiwa NA nesi kuja duniani akukufanyi usizaliwe kitandani dadangu amezalisha majiranimanytimes majumbani mwao wakiwa kitandani mwao.......unaruhusiwa mkuu
 
Naona hujaelewa nilimaanisha, yaani wanikumbusha mwalimu wangu mmoja pale chuo enzi hizo mungu amrehemu huko akhera, alikuwa akiogopa kutumia neno 'Kumaanisha' kwani alikuwa akiamini lina utusi ndani yake, mimi nakuambia sijazaliwa kitandani wewe wanilazimisha niwe nimezaliwa kitandani ebo! ndio kumaanisha nini sasa?
 
soma post vizuri utaelewa usikurupuke kucomment

Nimekusoma pasipo kukuelewa, hakuna kukurupuka hapo. Wewe ndiye hujamaliza kuandika insha ya swali la mtihani wako!!

Malizia mkubwa ueleweke. Jibu maswali yangu hapo juu, itakusaidia siku nyingine kuleta habari iliyokamilika!!
 
Back
Top Bottom