Ng'wanambula
Senior Member
- Oct 2, 2011
- 197
- 54
Naomba JPM awe makini na jinsi atakavyoshughulikia tatizo la watumishi hewa kwenye halmashauri zetu. Ninavyojua tafsiri ya watumishi hewa ni:
1. Watumishi waliofariki, kuacha kazi au kufariki lakini wakiendelea kulipwa mishahara
2. Watumishi ambao hawapo, yaani ni majina tu yanalipwa mishahara ikiwz watu halisi hawapo
3. Watumishi ambao wameondoka kwenda masomoni huku kjkiwa hakuna barua au nyaraka za kuwaruhusu kufanya hivyo
4. Watumishi ambao wamejipandisha madaraja na mishahara kwa udanganyifu
5. Watumishi wanaoshika nafasi za ukuu wa Idara huku wakiwa hawana sifa na wenye sifa wapo
KINACHOTOKEA HIVI SASA
Baada ya agizo la mh Rais, hivi sasa wakurugenzi na wakuu wa idara wako bize kutengeneza nyaraka feki ili kuhalalisha uchafu wao. Wanaandaa nyaraka kuonyesha walioondoka kwenda masomoni kinyume na taratibu kuwa walifuata taratibu.
Aidha, wanajenga mazingira kuonyesha kuwa waliopewa ukuu wa idara wakiwa hawana sifa walistahili kwa kuwa wenye sifa hawakuwepo. Hili ni kutaka kujiokoa na kutumbuliwa.
Nashauri mh. Rais kupitia wawakilishi wake na wanausalama waombe CV za watumishi wote ili kubaini uongo huu na wanaostahili na walio na sifa wapewe nafasi.