Watumishi 11 wa Manispaa ya Kigamboni kortini kuisababishia TAMISEMI hasara ya Milioni 169

Watumishi 11 wa Manispaa ya Kigamboni kortini kuisababishia TAMISEMI hasara ya Milioni 169

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Wafanyakazi 11 wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali, yakiwemo ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Shilingi 169,617,520 kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Kesi hiyo imetajwa leo, Juni 24, 2025, mbele ya Hakimu Nestory Balo, ambapo washitakiwa walitajwa kukabiliwa pia na makosa ya utakatishaji fedha, genge la uhalifu, ubadhirifu, uchepushaji na urakatishaji wa mali ya umma.

Wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU, Neema Kazoka, ameomba kibali cha mahakama kuchukua sampuli za maandishi kutoka kwa baadhi ya washitakiwa kusaidia katika upelelezi wa kesi hiyo.

Washitakiwa hao ni Jonathan Manguli, Geoffrey Martin, Jovenalis Mauna, Josephat Mtembei, Bibiana Lugani, Annie Maugo, Tumsifu Kachila, Aidan Mponzi, Hamis Kashinji, Paulo Mwakyusa na Godwin Cheyo.

Kesi imeahirishwa hadi Julai 8, 2025 kwa ajili ya kutajwa tena huku upelelezi ukiendelea.

1768288230498.png
 
Watu 11 izo Mil 169 ni kama 15 kila mtu. Ata IST hauagizi JP.
Bado kuna waliokula mgao bila kuacha footprint.
 
Back
Top Bottom