Watumiaji wa mtandao wa instagram pitieni hapa

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,779
Poleni na majukumu ya hapa na pale ya kulijenga taifa. Nahisi mmejiandaa vyema kuhesabiwa.

Kuna mtu nilikuwa nafanya nae kazi ya kutangaza bidhaa online kupitia instagram. Juzi tumekorofishana, katika harakati za kupozea machungu yake kaamua kufuta hiyo business account ya instagram ambayo kiukweli username yake imezoeleka kwa wengi.

Nilivyojaribu ku create account nyingine kwa email iliyokuwa kwenye account iliyofutwa, team ya instagram imekataa (Access Denied)! Nilipojaribu kutumia email mpya kufungua account mpya kwa username iliyokuwa ikifahamika, instagram wamekataa pia! Siwezi kuunda account mpya yenye username jipya maake nitapoteza attention kwa wateja!

Hoja yangu ni kuwa:

- Ninatakiwa kusubiri kwa muda gani (siku ngapi) ili email hii iliyofutiwa account iweze kuruhusiwa tena kutumika kufungua account nyingine?

- Ninatakiwa kusubiri kwa siku ngapi ili nifungue account yenye username sawa na hii lililotumika kwenye account iliyofutwa?

Msaada tafadhari!
 
haiwezi kukubali tena hiyo username,
baada ya siku 14 account inafutwa kabisa haiwezi kurudi tena
hapo fungua mpya anza kuipromo tena tofauti na hapo email ulofungulia account ya kwanza kama una acces nayo basi account unairudisha ileile ila tu kama hazijapita siku 14 toka ilipofutwa
 
Hapana. Same username haitokaa ijitokeze.

Mfano: username madmax nikafuta account au nika change username nikitaka rudia madmax itakataa. Labda madmax1 itakubali.
Mkuu, je ikitokea mfano username liwe izobiz, baada ya muda nibadili kwenda izo_biz, halafu account ifutwe ikiwa na hii izo_biz. Inawezekana baada ya muda kufungua nyingine yenye izobiz? Au majina yote yatakataliwa?
 
Hapana kamwe jina haliwezi kujirudia miaka nenda rudi.

91C09758-40A8-40B6-AECD-78EAE554F1D7.jpeg
 
email moja inaweza kufungua akaunti idadi yeyote ila akaunti mama inakuwa moja, zingine zinaluwa kama matawi tu, ikiingia kwenya akaunti kuu zingine zote zina-log in automatically.

Username subiri siku 14.

Bytheway, kwanini afute akaunti badala ya kuiuza tu? Na kwanini access details awe nazo yeye tu?. Baada ya kugombana ungebadili password na credentials zote.
 
Username subiri siku 14.
Dah! Afadhari, maake nilikuwa nshawaza kupoteza

Bytheway, kwanini afute akaunti badala ya kuiuza tu? Na kwanini access details awe nazo yeye tu?. Baada ya kugombana ungebadili password na credentials zote.
Si unajua tena mkuu hasira za watoto wa kike?
 
Dah! Afadhari, maake nilikuwa nshawaza kupoteza

Si unajua tena mkuu hasira za watoto wa kike?
Kurudisha username ile ile inaweza pelekea mhusika kulalamika inta na wakaifuta tena.

tengeneza username nyingine, ifanyie promo kwa ku like na ku follow account zenye majina makubwa.
 
Kurudisha username ile ile inaweza pelekea mhusika kulalamika insta na wakaifuta tena
Kwamba huyu mtoto wa kike alalamike! Kama nikibahatika kufungua nyingine yenye username kama iliyokuwepo, nabadili na email, access zote nabaki nazo! Na hatahusika kwa hili, hata nitakapoifungua nitahakikisha hajui chochote!
 
Mkuu, je ikitokea mfano username liwe izobiz, baada ya muda nibadili kwenda izo_biz, halafu account ifutwe ikiwa na hii izo_biz. Inawezekana baada ya muda kufungua nyingine yenye izobiz? Au majina yote yatakataliwa?
π™Ώπš˜πš•πšŽ πšœπšŠπš—πšŠ πš—πšπšžπšπšž πš’πšŠπš—πšπšž π™Έπš£πš£πš˜ π™±πšžπšœπš’πš—πšŽπšœπšœ πš”πš πšŠ πš”πšžπšπšžπšπš’πš πšŠ πšŠπšŒπšŒπš˜πšžπš—πš πš”πš πšŠ πš–πšŠπš›πšŠ πš—πš’πš’πš—πšπš’πš—πšŽ
 
Mmegombana??!!

Mlipe chake mmalizane
Hakuna cha malipo kwa kuwa biashara ilikuwa ni yetu sote, na hata gharama za ads na promotion tumekuwa tunagharamikia wote! Labda tuipasue biashara katikati ili ife kila mtu akatange na maisha yake! Ye akaolewe mi nikajiandae kuhesabiwa

Sababu ni ya ajabuajabu tu, nimemzushia kutoka kimapenzi na mlinzi wa jengo, ilikuwa ni kama utani, na nimemwambia kuwa ni utani. Baada ya taarifa kumfikia rafiki yake ndo kaamua kuharibu kila kitu!

Hata yeye huwa ananitania vitu vingi tu
 
Back
Top Bottom