Watuhumiwa wa wizi wa Fedha za EPA waachiwa huru

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Watuhumiwa Wa Wizi Wa Fedha Za EPA Waachiwa Huru






1.jpg
Rajabu Maranda

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru Kada wa CCM, Rajabu Maranda na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi wizi wa Sh milioni 207 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Jopo la mahakimu watatu likiongozwa na Hakimu John Utamwa, Ignas Kitusi na Eva Nkya liliwaachia washitakiwa hao baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa hao.

Mbali na Maranda washitakiwa wengine walioachiwa huru ni Farijala Hussein na waliokuwa wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, Bosco Kimera na Imani Mwakosya.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Utamwa alisema washitakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka manne kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo BoT na wiziwa Sh milioni 207.2 wako huru kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka kama inavyotakiwa kisheria.

Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuithibitishia mahakama jinsi Maranda na Farijala walighushi makubaliano ya kukusanya deni kati ya Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya Tanzania.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa bila Mwakosya kuwepo mahakamani, Hakimu Utamwa alisema upande wa Jamhuri wameshindwa kumleta mpelelezi wa kesi hiyo ili aweze kuithibitishia Mahakama saini ambazo zinadaiwa kuwepo katika makubaliano hayo hivyo udhaifu huo hauwezi kuwatia washitakiwa hatiani.

Aliongeza kuwa, upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha shitaka la kughushi, kwa hiyo shitaka la kuwasilisha nyaraka za uongo litakuwa limekufa,kwa sababu wameshindwa kuonesha kweli nyaraka ni za kughushi.

Aidha alisemwa wameshindwa kuonesha ni jinsi gani fedha hizo zilihamishwa kama wanavyodai kuwa mchakato huo ulifanikiwa kwa sababu Maranda na Farijala walitumia nyaraka za kughushi.
"Hakuna shahidi aliyeweza kutoa ushahidi ukaenda sawa na hati ya mashitaka iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya washitakiwa,"
alisema Hakimu Utamwa.

Nyaraka zinazodaiwa kughushiwa ni hati za makubaliano ya kuhamishiwa deni kutoka Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya nchini Tanzania, ambazo walizutumia na kuiba fedha hizo.

Baada ya Hukumu hiyo, Farijala alirudishwa rumande kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka miwili jela alichohukumiwa katika kesi nyingine na Maranda aliachiwa lakini bado ataendelea kwenda mahakamani kwa kuwa anakabiliwa na kesi nyingine.

Ndugu na marafiki waliokuwepo katika eneo hilo la mahakama walishukuru mahakama kutoa uamuzi wa haki na kusema kweli Mungu ametenda miujiza.

*** Kweli Tanzania shamba la bibi
1.EPA
2.MEREMETA
3. KAGODA
4. RICHMOND
5. ESCROW
6. MABEHEWA MABOVU
7. BILLION 256 ZA MIUNDOMBINU
8. RADA MBOVU
9. NDEGE YA RAIS
Yaani katika matukio yote haya hakuna hata mmoja aliyefungwa jera kwa kusababisha upotevu huu mkubwa wafedha ila kilichobaki ni wananchi kuchangishana ili kujenga Maabara.

Chanzo: Habari leo
 
Hakika ni ujinga kuishabikia ccm. Yaani hay majizi daaaaaa october sio mbali tuombe mungu lazima tuwaondoe
 
kesi za madai ya fidia zinafuata.....watanzania tujiandae kisaikolojia kuwafidia hawa jamaa,hasa familia ya huyo aliyepata kichaa kwa kesi ya kipuuzi,
 
Naomba MwanaJF Mwenye uzoefu na hii kesiatutajie aliyetakiwa kuiwakilisha Jamhuri kwenda kutoa ushahidi ambaye aliamua kuweka mpira kwapani. Mara kesi nyingine unaambiwa DPP hakuona haja ya kuendelea na kesi.
 
ni somo tosha,si kila kesi iende mahakamani,si kila mtu umshitaki,wengine wanafaa kuwa mashahidi
 
Lakini hawa jamaa si walikuwa na kesi nyingi nyingi?? Ambazo zingine wameshatiwa hatiani?? Mi sijaelewa...kwamba wako nje kabisa au kesi hii moja ndio wako huru??
 
Mawakili wa serikali, PCCB, Mkurugenzi wa Mashitaka, Polisi na Mahakimu wameisha beba chao.

Tutegemee vurugu huku kitaa: magari makubwa makubwa, mijumba mikubwa kama mihekalu:

Uongozi wa JK ni zaidi ya Manager wa Club ya Local Wine!
 
Hoi jamhuri vipi?hawa wanapeleka Maelezo yasiyojitosheleza ili kuwalinda watuhumiwa.hiyo sio bahati mbaya.ni mpango maalum Wa kifisadi kupitia waendesha mashtaka hao.haitatokea fisadi kuadhibiwa na serikali ya CCM.tuing'oe tuwape UKAWA.
 
Hakika ni ujinga kuishabikia ccm. Yaani hay majizi daaaaaa october sio mbali tuombe mungu lazima tuwaondoe

Ni zaidi ya ujinga.
Ni upumbavu na ujuha uliopitiliza.
 
Yaani hainiingii akilini mtu aliyetakiwa kwenda kutoa ushahidi upande wa jamhuri kutotokea mahakamani inamaana alikosa pesa ya nauli au umuhimu wa kesi kwake haukuwepo au hakuwa na taarifa au alikuwa kwenye hani muni au alilewa mvinyo wiki nzima au alikuwa mgonjwa mwaka mzima au au au....dah kweli tusha logwa na aliyetundondocha kisha kufa na kaburi lake lilishombwa na mafuriko ya mto rufiji na yale maji yameingia bahari hindi na sasa yamefika india kwenye sunami....shenzi kabisaaaa
 
Hakika Nilitegemea Haya Mambo, Sishangazwi na Hukumu!


Usishangazwe na hukumu hiyo ,huo ndio mtindo wa ccm kuwa kila karibu na uchaguzi ni lazima wavunje BENKI KUU si umeona safari hii walivyokomba kupitia ESCROW!! Kumbuka kuwa huyo Rajab Maranda alikuwa mweka hazina wa mkoa wa ccm!!! Afadhali hao walifikishwa hata mahakamani kuna wengine walioiba fedha nyingi zaidi walifikishwa mahakamani lakini kesi zao hazijawahi kusikilizwa kwa mfano wakina JEETU Patel umewahi kuwasikia kesi zao?
 
Back
Top Bottom