...we ukimkuta mama... mwanae akilia huoni uruma?
Hhhmmm. . .Mbona hata hawaelekei? Au labda wanatamani ila hawana?Anataka ujue kama na yeye ana katoto nyumbani.
Miafrika ndivyo tulivyo - source : Rais wa wabeba maboksi / Mbeba maboksi pekee ambae ana permission ya kuhuzuria vikao vya UN
Unajua mtoto akilia ni ngumu sana kujua anataka nini, hata wewe uliyekuwa naye unaweza usijue exactly mtoto anachotaka. Wapita njia wanajaribu kutoa msaada tu wa ushauri, just in case............ siyo lazima kufwata wanachosema
Huruma ntaona ila siwezi kwenda mwambia "mpe nyonyo ana njaa huyo" wakati sijui mambo yao binafsi na ndio kwanza nimewaona hivyo sijui kama ni kula mara ya mwisho alikula saa ngapi, au kama ni kulala kawaida yake huwa saa ngapi n.k
Ila TU nikiona huyo mama anahangaika naweza muuliza tatizo ni nini na kama naweza kumsaidia.
hata mtu aliye na mtoto sometimes hawezi kumwelewa, ndo maana watu wanajaribu tu kutoa ushauri, na sometimes it works....... mpita njia tu anaweza kukuambia jaribu kumpa maji, ukampa na akanyamaza. mimi sioni ubaya wowote kumshauri mtu kwa mtoto anayeliaSasa msaada wa ushauri wakati mtu HAJUI CHOCHOTE kuhusu huyo mtoto na aliyeko nae?
@Konnie. . .
Nimekusoma ila binafsi naamini hamna mtu anaemuelewa mtoto kama yule aliye nae. Yani kidogo kinachowezekana kuelewa/fahamu kuhusu mtoto ni yule aliyeko nae, iwe mzazi, ndugu au dada yake mlezi.Unless nae ndio mara ya kwanza kumwangalia huyo mtoto ofcourse. Kwahiyo sioni haja ya mtu ambae hata jina la huyo mtoto halijui kusema na kuonyesha anajua sana MAHITAJI na MATAKWA ya huyo mtoto.
hata mtu aliye na mtoto sometimes hawezi kumwelewa, ndo maana watu wanajaribu tu kutoa ushauri, na sometimes it works....... mpita njia tu anaweza kukuambia jaribu kumpa maji, ukampa na akanyamaza. mimi sioni ubaya wowote kumshauri mtu kwa mtoto anayelia
Kumbe kumbeba mtoto siku hizi imekuwa ni gia ya kutongozea? Hii ni kali ya mwaka.
Lizzy umenikumbusha tabia za watu. Mfano uliotoa wa mtoto kulia mi mmoja kati ya mifano mingi. Gari yangu iliharibika ghafla nikaiegesha pembeni ya barabara na nilipoanza kutoka kuchek kitu nilichokuwa na waswas nacho kwenye injini tayari kundi la watu lilikuwa limeshanizingira.Kila mmoja wao alikuwa mtaalam wa gari na alijua tatizo la gari langu."Umeweka maji ya kutosha kwenye redieta?" aliuliza mmoja. "Hiyo itakuwa fuel pump, imeziba" alitabiri mwingine. Kila mmoja alikuwa na sababu yake kwa nini gari ina matatizo.Mama mmoja nilimsikia akisema ni pancha.
Mimi kimyaaa! Nikafungua hood na kuchungulia mahali nilipopashuku.Kumbe kweli, waya(cable) ya accelerator ilikuwa imefyatuka. Nikaiweka sawa na kuwasha gari na kuondoka. Kwenye tatizo, kila mtu anajua chanzo! Pengine ndo maana hatuendelei kwa sababu watu ni wajuaji mno!

...kama ni mwanamke makini ataonesha juhudi za kumsaidia mwanae na walioko jirani wataelewa yule mama anaju!
inaboa na kusababisha watu kutoa izo OPTIONS pale unapokuta mtoto analia, mama hana habari...hashtuki wala haoneshi kujali kile kinachoendelea pale (mtoto kulia)...
watanzania pamoja na umaskini wetu, tumeumbwa na roho ya UPENDO!