Watu wote washauri wa Rais Samia?

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Nov 1, 2019
1,028
2,448
Nawasalimu kwa jina la JMT!

Tangu Bi. Samia ashike hatamu ya kiti cha urais wa nchi, basi kumezuka mengi ya kushangaza, kusisimua na kufurahisha.

Sijui watu wanamuonaje Mama Samia?

Kila mtu sasa amegeuka kuwa mshauri wa Samia kuhusu maswala mbalimbali yahusuyo nchi!

Wengine wamegeuka kuwa washauri-nasaha, wengine washauri-koko. Basi ilimradi tu fujo na vurumai kutoka pande zote.

Kila mtu anataka kumuongoza na kumuelekeza Rais kwa kadiri ya matakwa yake binafsi.

Chadema wanalilia maandamano, wengine wanalilia sijui mabadiliko ya kitu gani! Kila mtu anataka lake!

Naamini kuna ajenda za kitaifa, dira ya nchi, sera, ilani, katiba ya nchi, vipaumbele na miongozo mbalimbali.

Tumuache mama huyu atimize wajibu wake kwa kadiri inavyompasa. Tusimuandame na kumzonga zonga.

Msifikiri ni mpole kiasi hicho, maana siku atakapoamua kutumia rungu lake ipasavyo, mtaparaganyika na kukimbia.

Tuache kumzonga zonga Rais! Tunaweza kumshauri lakini tusimzonge zonge!

Ramadhan Kareem!
 
Nyie mliozoea udikteta mnapata shida sana kuona rais anakuwa msikivu kwa watu wake, mtateseka sana!
 
Tatizo watu tumezoea kwamba watanzania hawaruhusiwi kutoa maoni, tunafiki anayeongoza nchi ndiye mwenye akili. Lakini mnasahau jambo moja mama yuko tofauti sana, mpaka Mimi sasa napenda wateuliwe akinimama wengi zaidi kwenye nyadhifa. Wanaume waongo, wezi, wana tamaa utafikiri wamelogwa. Wanaume wakatiri, hawaoni shida kutoa roho za wengine, wanapenda kuwamiliki wananchi kama mifugo yao. Wanaona sifa kusema Mimi mkali, msifikiri Mimi mpole.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom