Watu Wote Mlio Wema, Msibariki Dhambi

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,512
Reaction score
15,098
Watu wote tusipenda uovu, tunaomkiri Mungu wa Kweli, tujitenge kabisa na uchaguzi huu uliojaa uovu, unaotumika kuwahalalisha waovu.

Hivi kuna mtu asiyejua ni nani anahusika na utekaji na mauji ya watu wanaokosoa maovu?

Kuna mtu asiyejua ni chama gani kinahusika na huu uovu wa kuteka, kuua, kupoteza na kubambikia watu kesi za uwongo?

Hivi kuna mtu asiyejua ni nani walitaka kumwua Fr. Dr. Kitima kwa sababu alikemea uporwaji wa bandari zetu?

Wewe unayeamini unamwabudu Mungu wa kweli, bila ya kujali dini au dhehebu lako, kweli hujui kuwa kuteka na kuua watu ni dhambi?

Wewe unayesema unamwabudu Mungu na kufuata mafundisho yake, ina maana hujui kuwa kumbambikia mtu kesi ya uwongo, kudhulumu haki za watu ni dhambi?

Hata kama wewe siyo mkatoliki, ina maana kweli hujui kuwa tendo lile la kutaka kumwua Fr. Kitima, ambaye kwa upendo wake kwa watu, aliamua kukemea uporwaji wa rasilimalu za nchi, ilikuwa ni uharamia na dhambi kubwa?

Hivi ina maana wewe unayesema unamwabudu Mungu wa kweli, hujui kuwa kuunga mkono uovu, kuwaunga mkono waovu, kuhalalisha uovu, ni dhambi na chukizo mbele za Mungu?

Hata kama huna sauti ya kupaza, ni aheri ukae kimya, lakini jitenge mbali kabisa na michakato hii iliyojaa uovu mkubwa ambapo waovu wanataka wapate baraka zenu.

Ninyi hata mkibariki dhambi, mtambue Mungu kamwe hatabariki dhambi, nanyi nyote mliobariki dhambi mtaibeba laana ya hao wanaoteka na kuua watu kwa sababu tu wamekemea uovu wao.

Mungu ni mwingi wa huruma na tajiri wa msamaha. Enyi waovu geuzeni mienendo yenu, mtubu na kumrudia Mungu. Shetani mnayemtegemea kamwe hatawapa ushindi wa kudumu, bali atawafanyia hadaa ya muda mfupi ili apate kuwapoteza.

Hii ni sauti yenye dhamira njema iliojaa upendo kwa wanadamu wote.
 
Hata kama huna sauti ya kupaza, ni aheri ukae kimya, lakini jitenge mbali kabisa na michakato hii iliyojaa uovu mkubwa ambapo waovu wanataka wapate baraka zenu.
Mkuu 'Hamatan', hili andiko lako hapa natamani sana lisambae mitaani kote Tanzania.

Hivi kweli hakuna njia za kusambaza taarifa maalum iliyo tengenezwa ili iwafikie wananchi wengi kadri iwezekanavyo, kati ya sasa hadi aoktoba 29?

MTanzania yeyote anayekwenda kupiga kura baada ya kusoma taarifa kama hii, ni wazi atakuwa na sababu zake maalum binafsi, kwa kufanya hivyo, na siyo kulisaidia taifa.

Nadhani itabidi pawepo na mikakati ya kuwaamusha waTanzania huko mitaani kuhusu taarifa kama hizi, hasa wiki ile kabla ya uchafuzi.
 
Mimi tokea yule dogo aliyechoma picha apotee na huku kuna mtu anatangaza habari ya utu na blahblah zingine napata taabu sana
 

Basi tuyatunze maandiko yote ya kuwafunulia watu ufahamu, na lile wiki la huo uchaguzi bandia, tuyambaze kote, iwe ni kwa njia ya mitandao au vipeperushi.
 
Mimi tokea yule dogo aliyechoma picha apotee na huku kuna mtu anatangaza habari ya utu na blahblah zingine napata taabu sana
Wananchi wamefanywa hawana akili. Yaani unateka na kuua watu, unawafunga na kuwabambikia watu kesi, halafu unasema unasimamia kazi na utu! Kwa hiyo kuua watu ni kuheshimu utu?
 
Mimi kibao aliniuma sana bora wangemfunga
Kufanya uharamia kama ule, ni lazima anayefanya, dhamira yake iwe imekufa, roho yake iwe imebakia kuwa pango la shetani.

Hakuna mwanadamu kamili mwenye Roho wa Mungu anaweza kufanya unyama ule aliofanyiwa Kibao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…