Watu wenye ajira tunaomba mtusaidie sisi ambao hatuna ajira

Finder boy

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
608
150
Wasalamu wanajamvi wenzangu!

Mara baada ya salamu naomba niwasilishe ombi langu kwenu: naomba wale wote wenye kazi zao na ajira zao watushike mkono siye vijana ambao tuko mtaani hatujui kitu cha kufanya. tumejaribu jitihada zetu zote tumeshindwa, hatuna mtu wa kutushika mkono, tuko sisi kama sisi, wazazi, walezi na ndugu zetu hawana uwezo wa kutusaidia.

Tumebahatika kusoma hadi chuo kikuu lakini tupo tu mtaani tunaangaika. Tuliamua kusoma ualimu wetu wa sanaa tukijua mara baada ya kuhitimu tutapata ajira, kumbe tulikuwa ndotoni, ndoto ambayo pengine tulilazimishwa kuiota.

Tunaambiwa tujiajiri bila kuoneshwa njia ya kujiajiri, sio kuwa hatupendi kujiajiri, ila tatizo mazingira ya kujiajiri, hatuna mitaji, tukiomba kukopeshwa pesa tunaambiwa hatuna vigezo vya kukopeshwa, tukiomba kwa ndugu na jamaa nao wanakataa kutukopesha kuwa hawana hela, sasa tukimbilie wapi jamani? Ikumbukwe sisi hatukuchagua kuzaliwa kwenye familia zetu maskini ambazo tumezaliwa na wala hakuna aliyechagua au anayependa kuwa kwenye hali ngumu na mbaya ambayo yuko nayo kwasasa. Yote ni mipango ya Mungu, Mungu aliagiza upendo, tupendane jamani, kwanini wewe huwe na furaha wakati mwenzako ana huzuni na masononeko?

Tusaidiane jamani, tushikeni mkono, binadamu tunaishi kwa kutegemeana, pengine wewe uko hapo ulipo maana kuna mtu alikushika mkono, nawe mshike mwingine mkono ili nae aje amshike mwingine huko mbeleni. Maombi ya kazi tunatuma sana, lakini hatubahatiki kupata, wengine hatupati kwakuwa hakuna mtu wa kutushika mkono, hakuna mtu wa kutuonesha fursa. Ikumbukwe hakuna mtu anayependa kuwa omba omba au kulia shida kila siku, ila ndio maisha yenyewe.

Tunafanya vitu tusivyovipenda, tunatukanwa, tunazalilika kwasababu ya shida zetu, kwasababu ya umaskini wetu. Wenye shule zenu tukumbukeni sie walimu ambao hatuna pakwenda, tulijifunza kufundisha sisi, basi tusaidieni jamani. kila mtu na fani yake, hata nje ya fani yake tusaidieni. tupeni izo part time kazi tufanye. kila mtu apate riziki yake na Mungu atawaongezea. kama wahitaji ni wengi basi wagawane hata icho kidogo. kama unalipa mshahara wa laki sita kwa mtu mmoja, sio mbaya kuwa na watu wawili alafu wakagawana laki tatu tatu kwenye hiyo post moja.

Vijana tunahangaika, vitu tulivyojifunza vinakuwa useless, kama ilivyo Imani bila matendo imekufa, basi ni sawa na fani tulizosomea bila kuzifanyia kazi (practice) tutajikuta tunapoteza vyote tulivyojifunza na kungundua kua tulipoteza muda kujifunza vitu vingi ambavyo hatujavifanyia kazi.
ninayomengi ya kuandika, ila naomba niweke nukta hapa maana majozi yananibubujika.

TUSHIKENI MKONO, NISHIKENI MKONO. ASANTENI.
 
Neno Uliloandika Hakika Lina Hisia Ndani Yake Naahamin Wale Wenye Mashule Watakutafuta
 
Mkuu unataka kaz?

Ndiyo mkuu. kazi au mtaji ndugu yangu. kazi ya kufundisha kuanzia shule ya msingi hadi chuo. Au mtaji wa Milioni Mbili. Nina project ya ufugaji kuku, sema mtaji ndio tatizo. ivyo nahitaji kazi, mtaji au fursa yoyote, cha msingi ili nami nifanye kazi ili nile ndugu yangu. Ahsante. kama waweza nisaidia karibu ndugu yangu.
 
Kijana naelewa sana concern yako, lakini katika hali yako hii ya kutokuwa na ajira, hebu angalia advantage ya wewe kutokuwa na ajira. Lakini katika kitu kitakachokufanya ufe maskini ni ajira.

Nakushauri kwa hali yeyote ngumu itakavyokuwa najua ni vigumu sana, jiajiri . Mungu atakubariki tu, anza kufanya kitu, Mungu huwa habariki patupu. Utafanikiwa tu, tena utashukuru kwa kutokuajiriwa
 
Wasalamu wanajamvi wenzangu!

Mara baada ya salamu naomba niwasilishe ombi langu kwenu: naomba wale wote wenye kazi zao na ajira zao watushike mkono siye vijana ambao tuko mtaani hatujui kitu cha kufanya. tumejaribu jitihada zetu zote tumeshindwa, hatuna mtu wa kutushika mkono, tuko sisi kama sisi, wazazi, walezi na ndugu zetu hawana uwezo wa kutusaidia.

Tumebahatika kusoma hadi chuo kikuu lakini tupo tu mtaani tunaangaika. Tuliamua kusoma ualimu wetu wa sanaa tukijua mara baada ya kuhitimu tutapata ajira, kumbe tulikuwa ndotoni, ndoto ambayo pengine tulilazimishwa kuiota.

Tunaambiwa tujiajiri bila kuoneshwa njia ya kujiajiri, sio kuwa hatupendi kujiajiri, ila tatizo mazingira ya kujiajiri, hatuna mitaji, tukiomba kukopeshwa pesa tunaambiwa hatuna vigezo vya kukopeshwa, tukiomba kwa ndugu na jamaa nao wanakataa kutukopesha kuwa hawana hela, sasa tukimbilie wapi jamani? Ikumbukwe sisi hatukuchagua kuzaliwa kwenye familia zetu maskini ambazo tumezaliwa na wala hakuna aliyechagua au anayependa kuwa kwenye hali ngumu na mbaya ambayo yuko nayo kwasasa. Yote ni mipango ya Mungu, Mungu aliagiza upendo, tupendane jamani, kwanini wewe huwe na furaha wakati mwenzako ana huzuni na masononeko?

Tusaidiane jamani, tushikeni mkono, binadamu tunaishi kwa kutegemeana, pengine wewe uko hapo ulipo maana kuna mtu alikushika mkono, nawe mshike mwingine mkono ili nae aje amshike mwingine huko mbeleni. Maombi ya kazi tunatuma sana, lakini hatubahatiki kupata, wengine hatupati kwakuwa hakuna mtu wa kutushika mkono, hakuna mtu wa kutuonesha fursa. Ikumbukwe hakuna mtu anayependa kuwa omba omba au kulia shida kila siku, ila ndio maisha yenyewe.

Tunafanya vitu tusivyovipenda, tunatukanwa, tunazalilika kwasababu ya shida zetu, kwasababu ya umaskini wetu. Wenye shule zenu tukumbukeni sie walimu ambao hatuna pakwenda, tulijifunza kufundisha sisi, basi tusaidieni jamani. kila mtu na fani yake, hata nje ya fani yake tusaidieni. tupeni izo part time kazi tufanye. kila mtu apate riziki yake na Mungu atawaongezea. kama wahitaji ni wengi basi wagawane hata icho kidogo. kama unalipa mshahara wa laki sita kwa mtu mmoja, sio mbaya kuwa na watu wawili alafu wakagawana laki tatu tatu kwenye hiyo post moja.

Vijana tunahangaika, vitu tulivyojifunza vinakuwa useless, kama ilivyo Imani bila matendo imekufa, basi ni sawa na fani tulizosomea bila kuzifanyia kazi (practice) tutajikuta tunapoteza vyote tulivyojifunza na kungundua kua tulipoteza muda kujifunza vitu vingi ambavyo hatujavifanyia kazi.
ninayomengi ya kuandika, ila naomba niweke nukta hapa maana majozi yananibubujika.

TUSHIKENI MKONO, NISHIKENI MKONO. ASANTENI.
Mmh mkuu pole sna umeandika uzi kwa hisia mno umenigusa sna mm binafsi nimehangaika kutafta ajira sna tangu nipate hata mwaka haujatimia nakuomba usikate tamaa pambana mkuu , kwa fani yako walimu wa sanaa hata nchi za kiarabu munahitajika sana kama hapa bongo pamekua pagumu naamin mungu atakufanikishia
 
Chanzo cha yote haya kwa sasa ni huyu Baba Ubaya (Magufuli) kitendo chake cha kuzuia ajira za moja kwa moja za walimu wa masomo ya Sanaa kimekua mwiba kwa vijana wengi nchini Zee halina huruma kabisa kisa yeye anakula,kunya,kuvaa,kwa kodi zetu basi katusahau vijana
 
Ndiyo mkuu. kazi au mtaji ndugu yangu. kazi ya kufundisha kuanzia shule ya msingi hadi chuo. Au mtaji wa Milioni Mbili. Nina project ya ufugaji kuku, sema mtaji ndio tatizo.
Najua hali unayopitia ndugu. Maisha ni katili sana na binadamu hawana wema. Labda kama ungekuwa unatafuta pesa ya kunywa bia au umekamatwa kwa kutukana wanasiasa ungechangiwa. Kaza roho, kuwa na subra na jaribu mambo madogo madogo.
- Nipo kwenye hali ngumu labda hata kuliko yako, naishi kwa nguvu ya Tumaini na Subra tu. Sina thamani yoyote kwa sasa, natengwa na watu kila siku. Nikibahatika kupata Lunch nakosa uhakika nitakula tena lini.
- Nimetafuta kazi viwandani, madukani, kutembeza bidhaa barabarani bila mafanikio. Nina idea yangu nzuri sana ya biashara nimejaribu kuipitch kwa watu lakini hawaniamini.Nimetafuta mkopo Tsh 300,000 hakuna aliyenipa kumbuka Hauko peke yako katika hali hiyo, kuwa mvumilivu ni MAPITO tu yanapita. FINALLY YOU WILL SEE LIGHT AT THE END OF THE TUNNEL!!
 
Mmh mkuu pole sna umeandika uzi kwa hisia mno umenigusa sna mm binafsi nimehangaika kutafta ajira sna tangu nipate hata mwaka haujatimia nakuomba usikate tamaa pambana mkuu , kwa fani yako walimu wa sanaa hata nchi za kiarabu munahitajika sana kama hapa bongo pamekua pagumu naamin mungu atakufanikishia
asante na Amen
 
Najua hali unayopitia ndugu. Maisha ni katili sana na binadamu hawana wema. Labda kama ungekuwa unatafuta pesa ya kunywa bia au umekamatwa kwa kutukana wanasiasa ungechangiwa. Kaza roho, kuwa na subra na jaribu mambo madogo madogo.
- Nipo kwenye hali ngumu labda hata kuliko yako, naishi kwa nguvu ya Tumaini na Subra tu. Sina thamani yoyote kwa sasa, natengwa kila siku.
sawa mkuu. Asante kwa ushauri
 
Kijana naelewa sana concern yako, lakini katika hali yako hii ya kutokuwa na ajira, hebu angalia advantage ya wewe kutokuwa na ajira. Lakini katika kitu kitakachokufanya ufe maskini ni ajira.

Nakushauri kwa hali yeyote ngumu itakavyokuwa najua ni vigumu sana, jiajiri . Mungu atakubariki tu, anza kufanya kitu, Mungu huwa habariki patupu. Utafanikiwa tu, tena utashukuru kwa kutokuajiriwa
asante kwa maneno yako ya faraja. muda mwingine maneno ya faraja kama haya hunifanya nihisi jamii haijanienga. Asante sana, muda mwingine vijana tunahitaji maneno ya kutufanya tusonge mbele zaidi ya pesa. Ahsante sana, upigapo goti lako kusali, nikumbuke nami niliyepost uzi huu, Mungu asikie kilio changu. Asante
 
Back
Top Bottom