Watu wengi wa Dar wamekaa kidili dili tu

Watu wengi wa Dar wamekaa kidili dili tu

Ujinga wao. Acha wapigwe tu....

Wanashindwa kuingia tradecarview na kununua gari?

Na showrooms zilivyojaa dsm kuna haja gani ya kumpa mtu ml 22 kizembezembe????
Teh teh..Amenichekesha huyo jamaa wa tatu..Kapigwa M22 zen kaenda kumaliza hasira kwa mke wa tapeli..Kanunua sex ya siku nne kwa M22 lol
 
Dar noma ... Watu wanawatapeli hata washua wao sembuse wewe jamaa... Wakaribu... Dar ni kuwa makini ... Hata baadhi ya viongozi wa dini hawaaminiki...
 
Nimeamua kuwapa onyo watu wa mikoani baada ya kuona kwa mda mrefu watu wa mikoani wanatapeliwa sana na jamaa zao au ndugu zao waishio dar-es- salaam.

Ninayo mifano mingi lakini leo nitaeleza mitatu tu. Kuna jamaa yangu wa kwanza alikuwa anataka gari akaenda Dar kwa ndugu yake ili akanunue lakini jamaa yake akamtafutia gari la milioni kumi na gari hilo lilisafiri hadi kufika nyumbani kwake ( mkoani) na kufa moja kwa moja.

Lakini mfano wa pili mnamo miezi kama minne iliyopita jamaa mwingine tena alienda dar kununua gari na alipofika kwa mwenyeji wake akamwambia anahitaji gari la milioni kumi na sita, jamaa akamwambia atamsaidia kupata gari nzuri matokeo yake ela amechukua amempiga kalenda jamaa amerudi bila gari na analalamika ametapeliwa na jamaa yake.

Na tatu niliitwa na rafiki yangu akiniomba kwenda kusuruhisha mgogoro na mke wake akidai kwamba walikopa fedha benki ili anunue gari na akaenda Dar kununua gari. Cha ajabu amerudi bila gari na fedha yote milioni 22 ametapeliwa na rafiki yake ambaye aliahidi kumsaidia kupata Harrier nzuri na mpaka anaondoka rafiki yake ameondoka nyumbani na kwenye simu hapatikani, akimuuliza mke wake mume wako yupo wapi anasema hajui wakati usiku wanapigiana simu na wanawasiliana.

Kwa kuwa jamaa alimwachia mke na nyumba alichoamua baada ya kugundua rafiki yake amekimbia na fedha zake ni kumgegeda mke wa rafiki yake siku nne na kuamua kurudi kwake mkoani huku akiumia makato ya deni kwenye mshahara kwa miaka mitano mbele.

Hivi nyie watu wa Dar watu wa mikoani mnawaonaje? Yaani nyie kila kitu dili, mtu unavunja undugu kwa ajili ya fedha. Acheni hizo bwana sisi tunatafuta fedha kwa shida, watu wanalima mwaka mzima halafu kipato chote unamwibia.

Ndio maana mimi mtu wa Dar huwa simwamini hata kidogo hata awe mkwe.

Na nyie watu wa mkoa mnakuja Dar kizezeta sana. Mtu anakwambia nipe hela nikakuletee gari unampa tu kirahisi. Showroom zipo kibao na hela wanakuambia kaweke bank uje na deposit slip tunakukabizi gari. Sasa unashindwa nini kuchangamsha akili na kuwa makini. Acha mtengenezwe tu mpaka mnyooke.
 
Sidhani kama suala uaminifu ni dar tu, kwa sasa kupata mtu mwanifu Tanzania ni kazi ngumu hata awe ndugu, ninajua rafiki yangu yupo nje ya nchi yeye ametapeliwa na mke wake kabisa. Walikuwa wote nje akampa mke fedha kuja kujenga Tanzania yeye aendelee na kazi lakini ilikuwa ndiyo mwishi wa ndoa yao. Mke aliingia Tz fedha nadhani alienda kujenga kwao na akaendelea kumwambia jamaa atume fedha hadi jamaa anakuja kushtuka hali tayari ilikuwa mbaya, mke ameshapata na kijana wa kumshughulikia. Kwa hiyo sidhani kama suala la uaminifu ni dar tu bali ni tatizo la kitaifa

Hii inafanana na ya yule mtangazaji runinga kule Kenya aliyepigwa risasi, yeye na baba yake.
 
Back
Top Bottom