Watu wengi wa Dar wamekaa kidili dili tu

Watu wengi wa Dar wamekaa kidili dili tu

ibesa mau mmezidi na nyinyi kupenda magari; mkija tena piga mchongo wa viwanja vya kiyoyozini... yaani ni bonge la asset... magari cku hizi co inshu! Ukipata robo eka pande za Dege Beach kwa 15 million leo; kesho unauza 500 million; kwahiyo kama vp nikuunganishe kwa jamaa yangu wa ardhi, sema inabidi umwandalie kama laki 7 hv, 2 anakula yeye na 5 zinatembea kwa waungwana watakaopitisha makaratasi na full hati ya makazi. Kuhusu mimi utanifikiria kimtindo... ki JF JF poa, tu!!
 
Last edited by a moderator:
Jamaa nae ana hasira za ajabu, kwahy kula mzigo siku 4 ameshalizika na ameshasahau ela yake!

Ingekuwa ni mimi ningemuoa kabisa huyo mwanamke,niliwahi kuleta uzi hapa kuwa 60% ya wakazi wa dar wanaishi kitapeli uzi ukafutwa.
 
Pole sana usha liwa kichwa! Hilo la kugegeda inaweza kuwa uongo labda kama alimbaka....
#usijemjini
 
Kweli dar utapeli ujaaa sana watu awahaminiki hata kidogo hata kama mtu wako Wa karibu
 
Sasa best ndo nini kuja kuniumbua huku jamii forums..?
Nakumbuka unanidai mkuu lakini usimalize maneno kwa kajisenti haka nitakulipa nitakapokuja X-mass ila niongeze laki 5 ili nikulipe M 5 kabisa.

Duh!wewe ndie uliehenyekewa mkeo?kwa hasira za jamaa inaelekea ndani ya siku nne zile hakubakiza hata tundu moja kwa shemeji yetu.
 
Bongoo eeee! bongo dar esalaam utalialia lia ndani ya dar esalaaam
 
Kuna jamaa wa huko moro nilimkabidhi gari yangu anitunzie nikiwa nje, narudi akaanza saundi kumbe alishaiuza kitambo! Matapeli ni watu sio miji.
 
Nimeamua kuwapa onyo watu wa mikoani baada ya kuona kwa mda mrefu watu wa mikoani wanatapeliwa sana na jamaa zao au ndugu zao waishio dar-es- salaam.

Ninayo mifano mingi lakini leo nitaeleza mitatu tu. Kuna jamaa yangu wa kwanza alikuwa anataka gari akaenda Dar kwa ndugu yake ili akanunue lakini jamaa yake akamtafutia gari la milioni kumi na gari hilo lilisafiri hadi kufika nyumbani kwake ( mkoani) na kufa moja kwa moja.

Lakini mfano wa pili mnamo miezi kama minne iliyopita jamaa mwingine tena alienda dar kununua gari na alipofika kwa mwenyeji wake akamwambia anahitaji gari la milioni kumi na sita, jamaa akamwambia atamsaidia kupata gari nzuri matokeo yake ela amechukua amempiga kalenda jamaa amerudi bila gari na analalamika ametapeliwa na jamaa yake.

Na tatu niliitwa na rafiki yangu akiniomba kwenda kusuruhisha mgogoro na mke wake akidai kwamba walikopa fedha benki ili anunue gari na akaenda Dar kununua gari. Cha ajabu amerudi bila gari na fedha yote milioni 22 ametapeliwa na rafiki yake ambaye aliahidi kumsaidia kupata Harrier nzuri na mpaka anaondoka rafiki yake ameondoka nyumbani na kwenye simu hapatikani, akimuuliza mke wake mume wako yupo wapi anasema hajui wakati usiku wanapigiana simu na wanawasiliana.

Kwa kuwa jamaa alimwachia mke na nyumba alichoamua baada ya kugundua rafiki yake amekimbia na fedha zake ni kumgegeda mke wa rafiki yake siku nne na kuamua kurudi kwake mkoani huku akiumia makato ya deni kwenye mshahara kwa miaka mitano mbele.

Hivi nyie watu wa Dar watu wa mikoani mnawaonaje? Yaani nyie kila kitu dili, mtu unavunja undugu kwa ajili ya fedha. Acheni hizo bwana sisi tunatafuta fedha kwa shida, watu wanalima mwaka mzima halafu kipato chote unamwibia.

Ndio maana mimi mtu wa Dar huwa simwamini hata kidogo hata awe mkwe.

Sio dar tu ni Tanzania
 
Ndo maana itaitwa bongo. we njoo kib...ge b...ge utaisoma namba
 
kama hawana kazi warudi vijijini waje walime tumbaku

Weweeee!! nani alime yani nishike jembe nooooop!!! lima wewe mwenye mikono na vidole vilivyoota sugu. si tushazoea kula ships kiepe, kulima wapi na wapi?
 
ibesa mau mmezidi na nyinyi kupenda magari; mkija tena piga mchongo wa viwanja vya kiyoyozini... yaani ni bonge la asset... magari cku hizi co inshu! Ukipata robo eka pande za Dege Beach kwa 15 million leo; kesho unauza 500 million; kwahiyo kama vp nikuunganishe kwa jamaa yangu wa ardhi, sema inabidi umwandalie kama laki 7 hv, 2 anakula yeye na 5 zinatembea kwa waungwana watakaopitisha makaratasi na full hati ya makazi. Kuhusu mimi utanifikiria kimtindo... ki JF JF poa, tu!!

Aina ya utapeli mwingine huo!.
Huyo anayeuza kwa 15mln yeye hizo 500mln haihitaji siyo?

ibesa mau mmezidi na nyinyi kupenda magari; mkija tena piga mchongo wa viwanja vya kiyoyozini... yaani ni bonge la asset... magari cku hizi co inshu! Ukipata robo eka pande za Dege Beach kwa 15 million leo; kesho unauza 500 million; kwahiyo kama vp nikuunganishe kwa jamaa yangu wa ardhi, sema inabidi umwandalie kama laki 7 hv, 2 anakula yeye na 5 zinatembea kwa waungwana watakaopitisha makaratasi na full hati ya makazi. Kuhusu mimi utanifikiria kimtindo... ki JF JF poa, tu!!
Mh kama utapeli nao huu
 
Last edited by a moderator:
Dar ni kweli kabisa watu wanaishi kiujanja ujanja tu.

Na pia waongo sana watu wa dar maneno mengi sana.

Tuacheni na dar yetu,nyie mnakazania kuwaomba ndugu zenu wawanunulie magari ilihali be forward wamefungua mpaka maofisi dar,sijui mmekariri? Hamna namna wacha mpigwe tu hizo hela.
 
Ujinga wao. Acha wapigwe tu....

Wanashindwa kuingia tradecarview na kununua gari?

Na showrooms zilivyojaa dsm kuna haja gani ya kumpa mtu ml 22 kizembezembe????
 
Back
Top Bottom