Watu wengi hujutia baadae kwa kupuuzia haya mambo

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,531
14,435
Leo wewe yajue na ujiepushee..

1. Jiepushe na watu wasio na malengo na wasiojua kusudi lao la kuja duniani, watakupotezea muda na kukukatisha tamaa na hutojifunza kitu cha kukusaidia kwao.

2. Mahusiano sahihi tu ndio yatakusaidia kutimiza malengo yako na ndoto zako. Kama hayakusaidii yanakuharibia.

3. Kadri unavyozidi kujitambua na kuonekana ni mtu unayejua nini unatafuta, watu wataacha
KUKUTUMIA VIBAYA na kukupa thamani.

4. Utaanza kukutana na watu sahihi wa kukuvusha na kukupa fursa kubwa pale UTAKAPOANZA KUCHUKUA HATUA kubadilit maisha yako.

5. Kujiamini ni hatua ya kwanza itakayobadilisha maisha yako kwenye vitu vingi.
....

6. Jifunze kusema HAPANA kwa mambo usiyoyapenda. Kama hujui kusema hapana Kuna watu watatumia huo udhaifu wako vibaya kukuumiza

7. Siku unazopoteza hupelekea kupoteza miezi na miaka. Mwisho utapoteza muda mwingi pasipo kufanya chochote. Usikubali siku ipite hujafanya jambo la maana.

8. Mtu wa kwanza kukusaidia kutimiza malengo na ndoto zako ni wewe mwenyewe, Usipoteze muda kusubiri mtu mwingine kukuvuta juu.

9. Acha Kufanya mambo nusunusu na kuishia njiani. Hakuna kitu utafanya itaonekana kikubwa kama ni mtu wa kuishia njiani kwenye mipango yako.

10. Tafuta kitu cha kuuza. Kama unafikiria kuwa na pesa nyingi na akiba baadae ni muhimu uwe na kitu cha kuuza.

𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔…
MAJUTO ni mjukuu, kama hutochukua hatua sasa ipo siku utakua unajilaumu sana huku ukisema
"ningejua" .
 
Pole mkuu ndo ubadilike . Na kwa kuwa ushajijua utabadilikaa🤏😎
Elewa kwamba una mambo makubwa sana na yenye faida wewe unayafanya na kutaka upate matokeo hapo hapo hio ni ngumu weka dira ya mipango yako. Dira ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu hapo uta
Nilijitahidi kuweka Hadi viapo vya kutokurudia makosa lakini nimejikuta narudia mule mule
 
Nilijitahidi kuweka Hadi viapo vya kutokurudia makosa lakini nimejikuta narudia mule mule
Screenshot_20231201_165820_Lark Player.jpg

🔨🔨💯
 
Back
Top Bottom