Uso wa nyoka
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 4,791
- 2,381
Nyinyi ndio mnaodekezwa na baba zenu na mwishowe mnakuja kulelewa na wanaume wanaofanana ba baba zenu..mtoto wa kiume na baba yake ni ndita na ubabe kwa kwenda mbele..wewe unataka ulishwe hadi icecream na baba yako? Mwisho utalambishwa visivyolambwa na wanaume wenzio..
Mkuu unachozungumza kinaweza kuwa sahihi ila ukumbuke watu wasio na akili timamu hutoa visingizio vingi kwa upuuzi wanaoufanya.
Kujenga urafiki na mtoto wako ni kitu kizuri sana kwa sababu mtoto anajifunza kujiamini, kuheshimu watu wazima na hata kufanya maamuzi ya busara. Asilimia kubwa ya watoto wasio watii shuleni, watukutu, wasiojiamini, ni wale wanaopigwa sana nyumbani na wazazi wao aidha hawana muda wa kukaa na familia nyumbani na kushare mambo au wazazi hawapatani wao kwa wao au ni single parents. Sisemi wote ila asilimia kubwa ni hivyo.
Kuna watu wengi hawawezi hata kuhutubia au kuendesha mazungumzo katika hadhira kwa sababu ya kutojiamini kutokana na kukosolewa na wazazi wao tangu wakiwa wadogo na matokeo yake wakajiona kuwa hawawezi kuzungumza kitu na kusikilizwa na watu walio serious kwa vile wao hawawezi kuwa na wazo la kufaa, yote kutokana na aliyekuwa father figure kuwa mkali na mkosoaji. Kuna watu wengi hawezi kufanya kazi bila kuongozwa kwa vile tu tangu wakiwa wadogo, walizoea kukosolewa walipotoa mawazo yao na kuelekezwa kinachowafaa kwa kushurutishwa kwa hiyo wasipoongozwa huwa hwaamini kuwa wataweza kufanya chaguzi zilizo sahihi kikazi.
Kuna watu wanagombana na kila mtu mtaani au katika maeneo ya kazi kwa vile hawajui urafiki na maelewano vikoje kutokana na kuishi katika mazingira ambayo hayakuwafundisha jinsi ya kupatana na kuelewana walipokuwa na wazazi wao wa kiume.
Kuna asilimia kubwa ya mashoga ambao wanalalamikia maelewano mabovu na wazazi wao wa kiume kama chanzo cha wao kutafuta attention ya wanaume wengine.
Lea mtoto wako kirafiki, utamsaidia kwa mengi sana.