Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Watu wapatao watatu wafunga safari Kutokea Mwanza kuja Arusha KWA MIGUU wakitembea huku wanafanya DUA Maalum yakumuombea Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema,safari hiyo waliianza tarehe 02.03.2017 ikiwa ni siku moja tu kabla ya Mhe.Mbunge kuachiwa kwa dhamana siku ya ijumaa tarehe 03.03.2017.
Watu hao watatu walipata taarifa wakiwa safarini kuwa Mbunge waliokuwa wanamfata kumsalimia katika Gereza kuu Arusha ameshapata dhamana,walimshukuru Mungu na kuona Mungu amejibu Maombi yao, baada ya kusikia kwamba mh Lema amepata dhamana hawakukatisha safari yao wapo njiani kwa takribani siku 16 sasa, leo, Kesho ama Keshokutwa watafika Arusha na kutimiza lengo ama Kusudi lao la kumuona na kumtia Moyo Mbunge wanaeamini ni Jasiri na Shujaa aliyewekwa Magereza kwa takribani siku 120.