Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Unamkumbuka kijana Benjamin wakati wa Azimio la Arusha? Aliyetembea kwa miguu kutoka Arusha kwenda Dar kuunga mkono Azimio la Arusha akafia mkoani Kilimanjaro baada ya kuugua maleria kali? Aliitwa shujaa wa Azimio. Matembezi ni moja ya mambo yanayoweza kufikisha ujumbe wa kishujaa juu ya jambo fulani.
Hali hiyo ndiyo imesababisha vijana watatu wa mkoani Mwanza, kufunga safari kutokea Mwanza kwenda Arusha KWA MIGUU wakitembea, na kufanya DUA Maalumu njiani ya kumuombea Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema, baada ya kukaa gerezani kwa muda mrefu.
Vijana walianza safari tarehe 02/03/2017 ikiwa ni siku moja tu kabla ya Mhe.Lema kuachiwa kwa dhamana. Lengo la kufanya maandamano hayo ya umbali mrefu wa takribani kilomita 1,000 ilikua kumsalimia Mhe.Lema katika Gereza kuu Arusha (Kisongo), na kutuma ujumbe wa kishujaa kwa watawala juu ya kutokukubaliana na uonevu aliofanyiwa Lema. Lakini kabla ya kumaliza safari yao Lema akawa ameshapata dhamana.
Walimshukuru Mungu na kuona amejibu Maombi yao, lakini hawakukatisha safari yao. Takribani siku 17 sasa wanatembea usiku na mchana kufika Arusha, wakilala masaa machache kwenye maeneo ya shule wanazokutana nazo njiani.
Kwa sasa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema Amesha wapokea watu hawa watatu Muda huu nyumbani kwake.