Watu Watano wafariki dunia mgodini, Mkoani Tabora.

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Watu watano wamefariki
dunia na wengine sita
kujeruhiwa baada ya
kudondokewa na mwamba
wa mawe katika shimo la
mgodi wa zamani wa
Resolute, uliopo Nzega
mkoani Tabora.

Akizungumzia swala hilo,
Mkuu wa wilaya ya Nzega,
Godfrey Ngupulla alisema
tukio hilo limetokea jana saa
7:00 baada ya kundi la
wachimbaji wadogo wa
mgodi wa Umoja kuvamia
eneo hilo ambalo limepigwa
marufuku na Serikali.

Alisema eneo hilo limezuiwa
kuchimbwa kutokana na
hatari iliyopo lakini baadhi ya
wachimbaji wamekuwa
wakiingia kwa kificho
kuchimba.

Aliwataja waliopoteza maisha
kuwa ni Joseph Mpenda,
mkazi wa shinyanga,
Mohamed Mohamed mkazi
wa Singida , Manona Nyombi
mkazi wa Bariadi na Modesta
Leonard mkazi wa Nzega.

Waliojeruhiwa ni Kangwa
Mayenga mkazi wa Bariadi,
Agness Antony mkazi wa
Chato, Deus Alphonce mkazi
wa Igunga na aliyefahamika
kwa jina moja la Mapunda
mkazi wa Chato.

Chanzo -
Mwananchi.
 
Back
Top Bottom