Watu Wanaopinga Maendeleo ya Magufuli

Watu Wanaopinga Maendeleo ya Magufuli

Toka awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na maendeleo mengi sana yakifanyika. Iwe ujenzi wa hospitali, barabara, madaraja, reli, ununuzi wa ndege na hata bwawa la umeme. Baadhi yetu umuhimu wa vitu hivi ni dhahir na nia ya Rais iko wazi.

Ukiangalia kwa asilimia nyingi ya maamuzi yake yamelenga katika ujenzi wa mifumo ya usafirishaji.

Hata ukichukulia katika makuzi ya viumbe hai, mifumo ya mwazo kabisa kujengwa wakati mtoto yupo tumboni mwa mama yake ni ile ya usafirishaji. Moyo na mishipa ya damu huanza kujengwa kwanza kabla ya mifumo ya fahamu na mimeng'enyo. Mifumo yote ya viumbe hai hutegemea mfumo wa usafirishaji.

Kama asili yetu imeona umuhimu wa mifumo ya usafirishaji, iweje leo tubeze umuhimu wake katika uchumi?

Sasa kwa kuwa kuna watu wanaopinga Mh. Rais kufufua/kujenga reli, bwawa la umeme na ununuzi wa ndege, basi wao watuambie ni kipi muhimu kufanywa kwanza.

Maendeleo ni nini?
Mkuu,
Mbona hii inafanana-fanana na kutafuta mashambulio yaasiyo ya muhimu. Kaa chonjo.
Mishipa haswa.

Maendeleo ni matukio ya hayo.

Ambaye haoni anachokifanya ni ujinga wa ktafuta.
 
Mkuu kwa mtazamo na uelewa wangu hivyo vyote ulivyovitaji si maendeleo ila matokeo ya maendeleo,hivyo vitu tunavijenga kwa kukopa pesa toka nje,lakini hao wanaotukopesha hivyo vitu wanavyotayari,je wao walikopa wapi?Jibu ni kwamba wao walitafuta maendeleo ya watu wao kwanza kwa maana ya kuhakikisha watu wao wanapata elimu bora,watu walipoendelea uwezo wao wa kulipa kodi ukaongezeka,serikali ikakusanya pesa ya kutosha ndo ikaanza kufanya hivyo unavyoita maendeleo, acha tujidanganye tu
Ni nani hao ambao hawakopi? Hivi unajua nchi zinazoongoza kuwa nakiasi kikubwa cha debt to gdp ratio?
Mkuu,
Mbona hii inafanana-fanana na kutafuta mashambulio yaasiyo ya muhimu. Kaa chonjo.
Mishipa haswa.

Maendeleo ni matukio ya hayo.

Ambaye haoni anachokifanya ni ujinga wa ktafuta.
Nimejaribu kukusoma lakini nimeshindwa, naomba unieleweshe ulitaka kusema nini.
 
Ni nani hao ambao hawakopi? Hivi unajua nchi zinazoongoza kuwa nakiasi kikubwa cha debt to gdp ratio?

Nimejaribu kukusoma lakini nimeshindwa, naomba unieleweshe ulitaka kusema nini.
Aisee
 
Chamoto,

..pamoja na ujenzi wa miundombinu, Magu anatakiwa apambane na umasikini na tatizo la ukosefu wa ajira.

..tatizo lake he is too one dimensional, yuko kwenye miundombinu tu. He needs to do more, na ni bahati mbaya kwamba hataki ushauri na anachukia sana akikosolewa.
Wewe huoni ujenzi wa miundo mbinu na ununuzi wa ndege umeongeza ajira. Au unataka upewe pesa bure.
 
..atcl inaendeshwa kwa HASARA.

..kwa hiyo ajira zilizotokana na kufufua atcl hazina faida kwa nchi.

..atcl ni KUPE anayefyonza kodi za waTz.

NB.

..naunga mkono sgr.

..napinga daraja la salender/coco beach.
 
Yeye alianza na kujenga miundombinu ya usafirishaji ili gharama za maisha zipungue na hivyo kupunguza umaskini. Mtu ataweza kutoka Mwanza akaja na treni ya umeme Dar akauza sangara wake na jioni akarudi Mwanza, siku hiyo hiyo.

Ajira zitaongezeka kutokana na urahisi wa kufanya biashara.

Serikali inatoa mkopo wa matrekta kwa bei nafuu, mwaka huu tumepata ziada ya chakula tani milioni 3.32 wakati mwaka 2014 tulikuwa na ziada ya tani milioni 2.3.
Unajua kilimo kinakua kwa asilimia ngapi? Sasa hivi tuko kwenye negative growth rate. Hiyo haijawahi kutokea katika awamu zote isipokuwa awamu hii.

Tourism mwaka 2015 ilikuwa inakua kwa 15% sasa ni 3.6%. Uwekezaji 2015 ulikuwa unakua kwa 28% lakini sasa ni 4%. Hivi kwa mwenendo huo tuna la kujivunia?

Tusiwe kama kuku wanaotupiwa mahindi ili wakamatwe wakachinjwe, nao wanafurahia kama vile wamealikwa kwenye sherehe. Kwa sasa, kuna baadhi ya watu wamekosa uelewa na ufahamu, wamebaki kushangilia kifo chao.
 
Naona hukuelewa muktadha wa hayo maneno, haikumaanisha kuwa reli yenye axel load ya tani 35 itakuwa ikibeba mchicha bali abiria (wananchi wa kawaida), wafanyabiashara wadogo wadogo wanaweza beba michicha yao humo.

Hiyo ilikuwa kuonesha kuwa treni hiyo itafaidisha watu wote.

Ongezeko la mazao kwa mwaka huu lilikuwa ni 124%

Kuna sekta nyingi ambazo serikali hii imeziimarisha ikiwemo madini, sasa hivi mapato yaliyokuwa yanapatikana kwa mwaka sasa yanapatikana kwa siku moja.

Maenedeleo yaliyoletwa na Magufuli.

Wale waliostahili walilipwa.
Kwenye madini ni uwongo mkubwa. Makusanyo ya kodi yaliyoongezeka ni ya kutoka kwa wachimbaji wadogo, ambayo ni peanut ukilinganisha na yale ya kutoka kwa makampuni makubwa. Mapato ya jumla ya sekta yameanguka. Usisiskiliza maneno ya jumla ya wanasiasa.

Ukweli wa kuanguka makusanyo ya madini yameilazimisha serikali kukubali mkataba mbaya kati yake na Barrick, mbaya kuliko hata ule wa awamu zilizopita
 
Unajua kilimo kinakua kwa asilimia ngapi? Sasa hivi tuko kwenye negative growth rate. Hiyo haijawahi kutokea katika awamu zote isipokuwa awamu hii.
Hizo takwimu unazitoa wapi wakati mwaka huu tunaongezeko la asilimia 120% ya chakula cha ziada?
Tourism mwaka 2015 ilikuwa inakua kwa 15% sasa ni 3.6%.
Mapato ya utalii yameongezeka kutoka Kutoka $2.1b (2018) to $2.2b (2019). Vile vile tembo na faru wameongezeka katika awamu hii, sasa tuambie huku kushuka kwa mapato wewe umetoa wapi?
Uwekezaji 2015 ulikuwa unakua kwa 28% lakini sasa ni 4%. Hivi kwa mwenendo huo tuna la kujivunia?
Kodi imeongezeka kutoka wastan wa bilioni 800m mpaka 1.3trilioni kwa mwezi hilo kwako ni ongezeko au pungufu?
 
Kwenye madini ni uwongo mkubwa. Makusanyo ya kodi yaliyoongezeka ni ya kutoka kwa wachimbaji wadogo, ambayo ni peanut ukilinganisha na yale ya kutoka kwa makampuni makubwa. Mapato ya jumla ya sekta yameanguka. Usisiskiliza maneno ya jumla ya wanasiasa.

Ukweli wa kuanguka makusanyo ya madini yameilazimisha serikali kukubali mkataba mbaya kati yake na Barrick, mbaya kuliko hata ule wa awamu zilizopita
Mapato yameshuka kivipi wakati hata mrahaba tulikuwa tunapata 3% (sheria ya madini ya 1998) wakati sasa tutapata 50% ya mapato au wewe unaongea kwa maslahi ya makampuni ya nje?
 
Ili tuendelee tunahitaji..

Watu..

Siasa safi

Uongozi Bora.

Watu ndiyo hao wanatekwa na kupotezwa,serikali iko kimya .

Siasa ndiyo hiyo hata mikutano ya ndani ni shida,ni vizuri kuwepo na Uhuru wa Kujieleza.

Uongozi Bora hatuna ni Mtu Mmoja anaamua atakavyo bila kufuata Sheria na Katiba, ona wakuu wa Wilaya na Mikoa wanavyoivunja Katiba.
 
Siwezi kufurahia mtu yeyote akikubwa na hayo ila kuna watu wamekuwa wakuwa wakifanya hayo halafu wakimlaumu serikali?

Kama wana nguvu ya kufanya hayo wasidhibitiwe INA maana wana nguvu kuliko serikali
 
Ili tuendelee tunahitaji..

Watu..

Siasa safi

Uongozi Bora.

Watu ndiyo hao wanatekwa na kupotezwa,serikali iko kimya .

Siasa ndiyo hiyo hata mikutano ya ndani ni shida,ni vizuri kuwepo na Uhuru wa Kujieleza.

Uongozi Bora hatuna ni Mtu Mmoja anaamua atakavyo bila kufuata Sheria na Katiba, ona wakuu wa Wilaya na Mikoa wanavyoivunja Katiba.
Kama wana nguvu ya kufanya hayo wasidhibitiwe INA maana wana nguvu kuliko serikali
Watu wanafumwa na wake za watu, wanafanyiziwa unasingiziaje serikali?
 
Bugirichato hajaleta maendeleo yoyote yale bali wizi, ufisadi na ubadhirifu wa kutisha na yote haya yamo kwenye ripoti mbili za CAG ya mwaka jana na mwaka huu na pia malalamiko ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara.

Toka awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na maendeleo mengi sana yakifanyika. Iwe ujenzi wa hospitali, barabara, madaraja, reli, ununuzi wa ndege na hata bwawa la umeme. Baadhi yetu umuhimu wa vitu hivi ni dhahir na nia ya Rais iko wazi.

Ukiangalia kwa asilimia nyingi ya maamuzi yake yamelenga katika ujenzi wa mifumo ya usafirishaji.

Hata ukichukulia katika makuzi ya viumbe hai, mifumo ya mwazo kabisa kujengwa wakati mtoto yupo tumboni mwa mama yake ni ile ya usafirishaji. Moyo na mishipa ya damu huanza kujengwa kwanza kabla ya mifumo ya fahamu na mimeng'enyo. Mifumo yote ya viumbe hai hutegemea mfumo wa usafirishaji.

Kama asili yetu imeona umuhimu wa mifumo ya usafirishaji, iweje leo tubeze umuhimu wake katika uchumi?

Sasa kwa kuwa kuna watu wanaopinga Mh. Rais kufufua/kujenga reli, bwawa la umeme na ununuzi wa ndege, basi wao watuambie ni kipi muhimu kufanywa kwanza.

Maendeleo ni nini?
 
Bugirichato hajaleta maendeleo yoyote yale bali wizi, ufisadi na ubadhirifu wa kutisha na yote haya yamo kwenye ripoti mbili za CAG ya mwaka jana na mwaka huu na pia malalamiko ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara.
Kama wewe upo kwenye nafasi yake ungefanya nini?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nisingefanya ujinga anaoufanya unaosababisha Watanzania kuishi kwa hofu kubwa ya kutekwa, kuteswa hata kuuawa kwa kuikosoa Serikali au kuandika ukweli kuhusu yanayojiri nchi I.

Ningeheshimu katiba ya nchi, mahakama, bunge na Watanzania. Ningeheshimu ushauri wa washauri wa mambo mbali mbali yenye vipaumbele kwa Watanzania. Ningeheshimu uhuru na haki ya vyama vingine vya siasa ili kufanya shughuli zao nchi nzima bila kuingiliwa na yeyote.

Ningeiheshimu ofisi ya CAG na kumpa uhuru wote ambao CAG anauhitaji kuweza kutenda kazi zake za kila siku katika kudhibiti matumizi ya pesa za walipa kodi.

Ningedumisha uhuru, haki, amani na mshikamano wa Watanzania wote bila kujali itikadi. Ningehakikisha Bunge linakuwa na meno ya kutimiza wajibu wake wa kuisimamia Serikali bila vitisho ya kutorudi Bungeni.

Ningehakikisha tuna katiba mpya isiyopendelea chama chochote na inayokubalika na Watanzania wote pia ningehakikisha tuna Tume huru ya uchaguzi inayosimamia uchaguzi huru na wa haki.

Ningehakikisha pesa za walipa kodi nchini zinatumika kuboresha vipaumbele vya Watanzania ikiwemo elimu, matibabu, umeme, maji, madarasa yenye hadhi, walimu wa kutosha, madawati ya kutosha, kuongeza ajira nchini na kuweka wazi mikataba yote ya rasilimali ambayo nchi inaingia na kuhakikisha magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama Malaria, kuhara, kipindu pindu tunayotokomeza kabisa nchini. Pia kipaumbele kikubwa cha miundo mbinu katika mikoa mbali mbali nchini ikiongozwa na jiji la Dar.

Nisingechota hata senti moja bila idhini ya Bunge wala kufanya matumizi makubwa ambayo si vipaumbele kwa Watanzania kama kununua ndege au trillions zilizomwagwa chato.

Kama wewe upo kwenye nafasi yake ungefanya nini?
 
Toka awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na maendeleo mengi sana yakifanyika. Iwe ujenzi wa hospitali, barabara, madaraja, reli, ununuzi wa ndege na hata bwawa la umeme. Baadhi yetu umuhimu wa vitu hivi ni dhahir na nia ya Rais iko wazi.

Ukiangalia kwa asilimia nyingi ya maamuzi yake yamelenga katika ujenzi wa mifumo ya usafirishaji.

Hata ukichukulia katika makuzi ya viumbe hai, mifumo ya mwazo kabisa kujengwa wakati mtoto yupo tumboni mwa mama yake ni ile ya usafirishaji. Moyo na mishipa ya damu huanza kujengwa kwanza kabla ya mifumo ya fahamu na mimeng'enyo. Mifumo yote ya viumbe hai hutegemea mfumo wa usafirishaji.

Kama asili yetu imeona umuhimu wa mifumo ya usafirishaji, iweje leo tubeze umuhimu wake katika uchumi?

Sasa kwa kuwa kuna watu wanaopinga Mh. Rais kufufua/kujenga reli, bwawa la umeme na ununuzi wa ndege, basi wao watuambie ni kipi muhimu kufanywa kwanza.

Maendeleo ni nini?
Ivi kumbe unahangaika na hawa watu kumi wanaopinga kwenye mtandao ,?wacha wataona kivumbi 2020 ndio watajua wanchi wanyonge waliokuwa wanaibiwa haki zao wanampigia kura JPM kwa kishindo
 
Maendeleo ni maprof vilaza
Toka awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na maendeleo mengi sana yakifanyika. Iwe ujenzi wa hospitali, barabara, madaraja, reli, ununuzi wa ndege na hata bwawa la umeme. Baadhi yetu umuhimu wa vitu hivi ni dhahir na nia ya Rais iko wazi.

Ukiangalia kwa asilimia nyingi ya maamuzi yake yamelenga katika ujenzi wa mifumo ya usafirishaji.

Hata ukichukulia katika makuzi ya viumbe hai, mifumo ya mwazo kabisa kujengwa wakati mtoto yupo tumboni mwa mama yake ni ile ya usafirishaji. Moyo na mishipa ya damu huanza kujengwa kwanza kabla ya mifumo ya fahamu na mimeng'enyo. Mifumo yote ya viumbe hai hutegemea mfumo wa usafirishaji.

Kama asili yetu imeona umuhimu wa mifumo ya usafirishaji, iweje leo tubeze umuhimu wake katika uchumi?

Sasa kwa kuwa kuna watu wanaopinga Mh. Rais kufufua/kujenga reli, bwawa la umeme na ununuzi wa ndege, basi wao watuambie ni kipi muhimu kufanywa kwanza.

Maendeleo ni nini?
 
Maendeleo hayaletwi na mtu, bali na watu.., kitu anachoweza kufanya kiongozi mzuri ni kuunganisha nguvu kazi zote kuelekea kule anakotaka yeye.., thus uwezo wa ku-inspire jamii ili kuendelea..

Kosa kubwa hata wewe ulilofanya ni kuita maendeleo ya mtu (hapo ni kuwaside-step wengine hence kutokupata 100% kutoka kwao)..

Maendeleo ya muda mrefu sio one dimensional.., mazuri kayafanya.., ila kuna mabaya yanayofanyika ambayo misingi yake ilijengwa pole pole kwa zaidi ya miaka 50.., mfano uhuru wa habari na baadhi ya watu kuona wanaminywa kufanya kile ambacho ni haki yao kikatiba (sad enough kuminya kwake hao watu hakumsaidii na angewaachia ingemjenga maradufu sababu watu wangepima yasemwayo na kuchambua pumba na mchele.., sasa kwa kuwabana hata wenye pumba wanaonekana kwamba huenda wangeachiwa wangeleta mchele)

“A good leader takes more than his share of the blame and less than his share of the credit.”​
 
Nisingefanya ujinga anaoufanya unaosababisha Watanzania kuishi kwa hofu kubwa ya kutekwa, kuteswa hata kuuawa kwa kuikosoa Serikali au kuandika ukweli kuhusu yanayojiri nchi I.
Hivi utafananishaje na wakati ule Mwangosi anatolewa utumbo hadharani na Dr. Ulimboka alivyoumuliwa kama hamira?

Nani amefanyiwa hayo kipindi hichi?
Ningeheshimu katiba ya nchi, mahakama, bunge na Watanzania. Ningeheshimu ushauri wa washauri wa mambo mbali mbali yenye vipaumbele kwa Watanzania. Ningeheshimu uhuru na haki ya vyama vingine vya siasa ili kufanya shughuli zao nchi nzima bila kuingiliwa na yeyote.
Kuna chama kimefutwa wakati huu? Shughuli za chama ni maandamano? Hivi Canada watu huwa wanaandamana kiholela bila vibali?
Ningeiheshimu ofisi ya CAG na kumpa uhuru wote ambao CAG anauhitaji kuweza kutenda kazi zake za kila siku katika kudhibiti matumizi ya pesa za walipa kodi.
CAG kazi yao ni kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za serikali na kutoa taarifa, wao siyo law enforcement agent, sasa ni wapi wamezuiwa kufanya kazi yao?
Ningedumisha uhuru, haki, amani na mshikamano wa Watanzania wote bila kujali itikadi.
Watu wanatukana hapa JF kila siku na hakuna anayesumbuliwa ni haki gani unayoitaka?
Ningehakikisha Bunge linakuwa na meno ya kutimiza wajibu wake wa kuisimamia Serikali bila vitisho ya kutorudi Bungeni..
Kazi ya Bunge ni kutunga sheria na siyo kuisimamia serikali.
Ningehakikisha tuna katiba mpya isiyopendelea chama chochote na inayokubalika na Watanzania wote pia ningehakikisha tuna Tume huru ya uchaguzi inayosimamia uchaguzi huru na wa haki..
Unayo haki ya kufanya hivyo ila awamu hii imekuja na mikakati yake ambayo inaitekeleza, wao hawakuahidi katiba mpya.
Ningehakikisha pesa za walipa kodi nchini zinatumika kuboresha vipaumbele vya Watanzania ikiwemo elimu, matibabu, umeme, maji, madarasa yenye hadhi, walimu wa kutosha, madawati ya kutosha, kuongeza ajira nchini na kuweka wazi mikataba yote ya rasilimali ambayo nchi inaingia na kuhakikisha magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama Malaria, kuhara, kipindu pindu tunayotokomeza kabisa nchini. Pia kipaumbele kikubwa cha miundo mbinu katika mikoa mbali mbali nchini ikiongozwa na jiji la Dar.
Hakuna hata moja ambalo halifanywi na awamu hii.
Nisingechota hata senti moja bila idhini ya Bunge wala kufanya matumizi makubwa ambayo si vipaumbele kwa Watanzania kama kununua ndege au trillions zilizomwagwa chato.
Watanzania waliokuwa wanaenda India sasa wanalipa 1/4 ya gharama, huoni kuwa hili ni jambo zuri? Wewe unaweza ona ununuzi wa ndege siyo wa maana ila Rais wakati anagombea aliahidi kuifufua ATC, wananchi wakamchagua, sasa kosa lake ni nini kutekeleza ahadi zake?

Kutokana na kuwa na ndege zetu, utalii umeanza kuongezeka (50%) kwa kuwa watalii wanatumia pesa zaidi kwenda kwenye vivutio vingi kwa kutumia ndege zetu. Wewe huoni hilo?
 
Back
Top Bottom