Watu Wanaopinga Maendeleo ya Magufuli

Watu Wanaopinga Maendeleo ya Magufuli

Akishafanya yote hayo nani atayatumia maana either watu tutakua hatuna nauli hata ya ku afford au wengi watakua washatangulia mbele ya haki kwa magonjwa ya moyo na saratan zilizosababishwa na ugumu na ukali wa awamu hii......

Ukitaka maendelea ya kweli lazima uangalie pia nabya raia mmoja mmoja
 
Maendeleo ni pamoja na kuteka watu?, kuua watu?, kutesa watu, kupiga risasi watu?, kunyanyasa watu?, kama hayo nayo ni maendeleo basi hatuyataki maendeleo ya namna hiyo
Uzuri ameandika ni maendeleo ya Magufuli..kama Nchi bado sana...hakuna cha maendeleo zaidi ya unafiki..[emoji41]
 
hayo maendeleo unayoringia kuwa kayafanya.unaweza ukasema Tanzania ni Dubai mpya.
Ila kikubwa anafeli kwenye kutawala na ameshawaambukiza mpaka wafuasi wake.leo hii tunalazimishwa tumuone MTU mmoja ndo anaiweza hii nchi tukipinga tunaonekana sio wazalendo na wengine wanatekwa Na hata kuuliwa pia kufunguliwa kesi.
Kwanini mnalazimisha aonekana ni MTU sahihi kuliko wengine.?
Kwako wewe kama ungepata nafasi ya kuongoza ungeanza na nini?
Akishafanya yote hayo nani atayatumia maana either watu tutakua hatuna nauli hata ya ku afford au wengi watakua washatangulia mbele ya haki kwa magonjwa ya moyo na saratan zilizosababishwa na ugumu na ukali wa awamu hii......

Ukitaka maendelea ya kweli lazima uangalie pia nabya raia mmoja mmoja
Kwani watu wanapopanda mabasi sasa wanapanda bure?
Hakuna anayepinga maendeleo watu wachopinga kwenye maendeo hayo ni kwanamna utaratibu unavyoenda na wananchi wakawaida walivyo ukilinganisha na maendeleo yenyewe. Kama wafanyakazi hawapandishiwa madaraja toka aingie madarakani utasemaje tunaendelea,wakati huo huo pengo la mwenye nacho na asiyekuwa nacho bado liko vile vile
Sababu ya kutopandishwa madaraja mwenyewe alisema kwasasa tunajenga miundombinu, huu ni wakati wa kujifunga mikanda.
 
Tatizo Elimu. Sisi watanzania tunataka Maendeleo ya Watu. Siyo Maendeleo ya Vitu. Nyerere aliimba sana hili. Kuwa Maendeleo ni Pamoja na Kukuza Ustawi, Uchumi wa Mtu Binafsi, Uhuru wa Maoni, Huduma Bora za Jamii Demokrasia Huru. Reli, ndege, barabara, viwanja nk, bila UHURU, DEMOKRASIA na UCHUMI BORA BINAFSI ni bora ya Ukoloni wa Mwingereza.

Hukuwepo wakati wa Nyerere mambo mengi yalikuwa yanafanywa kwa amri hujui tu, inawezekana ni kijana mdogo huelewi, ulizia watu au wazazi wako, kulikuwa na mambo mazito yalikuwa yanatekezwa leo isingewezekana kabisa, oparesheni vijiji iliacha watu na majunzi makubwa, vita vya kagera,watu binafsi walikuwa hawaruhusiwi kumiliki biashara, kununua Magari kwa vibali, vita vya uhujumu uchumi iliacha watu na majonzi makubwa, nadhani watu wengi umri mdogo, hawajui tulikotoka, hapakuwa na matusi kama kizazi hiki,
 
Chamoto,

..natofautiana na wewe kuhusu treni ya umeme kusafirisha wauza sangara.

..pia natofautiana na Naibu Waziri Mh.Mavunde aliyedai treni ya umeme itakuwa ikisafirisha wauza mchicha.

..Kama hayo ndiyo matarajio ya aina ya mizigo itakayokuwa ikisafirishwa na sgr basi taifa litaingia ktk hasara na mzigo mkubwa wa madeni.

..kuhusu kilimo umeeleza kuhusu kuongezeka kwa uzalishaji toka mwaka hadi mwaka.

..Sasa kuna kiwango cha ukuaji ktk sekta ya kilimo, nadhani ni asilimia 9 kila mwaka, ambacho wataalamu wa uchumi wanasema lazima tukifikie.

..Na ukuaji huo unapaswa uwe sustained kwa miaka kadhaa. If we do not reach that target wataalamu wanasema masikini hautakwisha hapa Tz.

..Nadhani unanielewa kwanini naona Jpm amepungukiwa ktk mbinu za kuikwamua nchi yetu toka ktk umasikini.
 
Nadhani wapingaji hawana tatizo na maendeleo, wana tatizo na anayeleta hayo maendeleo (labda hawampendi) maana barabara watazitumia, ndege watapanda na hawajagoma kuchangia kodi.
Swali sahihi linaweza kuwa ni kwanini wapingaji hamumpendi wakati anawaletea maendeleo?

Ni sawa na mwanamke anayezitaka pesa zako Ila wewe hakutaki, atakuponda tu ila ela atachukua.
 
Ndege na sgr ni hasara tu... Upotevu wa pesa...
Bora ata anepambania barabara pekee uku akihakikisha wakulima wanamazingira mazuri..


Utasafirisha nini?
Nadhani wapingaji hawana tatizo na maendeleo, wana tatizo na anayeleta hayo maendeleo (labda hawampendi) maana barabara watazitumia, ndege watapanda na hawajagoma kuchangia kodi.
Swali sahihi linaweza kuwa ni kwanini wapingaji hamumpendi wakati anawaletea maendeleo?

Ni sawa na mwanamke anayezitaka pesa zako Ila wewe hakutaki, atakuponda tu ila ela atachukua.
 
Maendeleo ni pamoja na kuteka watu?, kuua watu?, kutesa watu, kupiga risasi watu?, kunyanyasa watu?, kama hayo nayo ni maendeleo basi hatuyataki maendeleo ya namna hiyo
Ili uendelee lazima utakutana na wapingaji na wasaliti na hukumu ya msaliti ni moja tu nayo ni kumwondoa duniani na kumpeleka kwa Mwenyezi Mungu ili akapata hukumu stahiki.
 
Toka awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na maendeleo mengi sana yakifanyika. Iwe ujenzi wa hospitali, barabara, madaraja, reli, ununuzi wa ndege na hata bwawa la umeme. Baadhi yetu umuhimu wa vitu hivi ni dhahir na nia ya Rais iko wazi.

Ukiangalia kwa asilimia nyingi ya maamuzi yake yamelenga katika ujenzi wa mifumo ya usafirishaji.

Hata ukichukulia katika makuzi ya viumbe hai, mifumo ya mwazo kabisa kujengwa wakati mtoto yupo tumboni mwa mama yake ni ile ya usafirishaji. Moyo na mishipa ya damu huanza kujengwa kwanza kabla ya mifumo ya fahamu na mimeng'enyo. Mifumo yote ya viumbe hai hutegeme mfumo wa usafirishaji.

Kama asili yetu imeone umuhimu wa mifumo ya usafirishaji, iweje leo tubeze umuhimu wake katika uchumi?

Sasa Kwa kuwa kuna watu wanaopinga Mh. Rais kufufua/kujenga reli, bwawa la umeme na ununuzi wa ndege, basi wao watuambie ni kipi muhimu kufanywa kwanza.

Maendeleo ni nini?
maendeleo ya magufuli? maendeleo ya nchi
 
hiy
Yeye alianza na kujenga miundombinu ya usafirishaji ili gharama za maisha zipungue na hivyo kupunguza umaskini. Mtu ataweza kutoka Mwanza akaja na treni ya umeme Dar akauza sangara wake na jioni akarudi Mwanza, siku hiyo hiyo.

Ajira zitaongezeka kutokana na urahisi wa kufanya biashara.

Serikali inatoa mkopo wa matrekta kwa bei nafuu, mwaka huu tumepata ziada ya chakula tani milioni 3.32 wakati mwaka 2014 tulikuwa na ziada ya tani milioni 2.3.
mwaka jana wakulima wa KOROSHO WALIPORWA KOROSHO ZAO
 
Ili uendelee lazima utakutana na wapingaji na wasaliti na hukumu ya msaliti ni moja tu nayo ni kumwondoa duniani na kumpeleka kwa Mwenyezi Mungu ili akapata hukumu stahiki.
unamkumbuka kijana wa MAKAMBO? RAISI ALIAMRISHA ASHIKISHWE ADABU/ APIGWE KISA KABEBA BANGO LENYE UJUMBE WA MAJI
 
Chamoto,

..natofautiana na wewe kuhusu treni ya umeme kusafirisha wauza sangara.

..pia natofautiana na Naibu Waziri Mh.Mavunde aliyedai treni ya umeme itakuwa ikisafirisha wauza mchicha.

..Kama hayo ndiyo matarajio ya aina ya mizigo itakayokuwa ikisafirishwa na sgr basi taifa litaingia ktk hasara na mzigo mkubwa wa madeni.[
Naona hukuelewa muktadha wa hayo maneno, haikumaanisha kuwa reli yenye axel load ya tani 35 itakuwa ikibeba mchicha bali abiria (wananchi wa kawaida), wafanyabiashara wadogo wadogo wanaweza beba michicha yao humo.

Hiyo ilikuwa kuonesha kuwa treni hiyo itafaidisha watu wote.
..kuhusu kilimo umeeleza kuhusu kuongezeka kwa uzalishaji toka mwaka hadi mwaka.

..Sasa kuna kiwango cha ukuaji ktk sekta ya kilimo, nadhani ni asilimia 9 kila mwaka, ambacho wataalamu wa uchumi wanasema lazima tukifikie.

..Na ukuaji huo unapaswa uwe sustained kwa miaka kadhaa. If we do not reach that target wataalamu wanasema masikini hautakwisha hapa Tz.
Ongezeko la mazao kwa mwaka huu lilikuwa ni 124%
..Nadhani unanielewa kwanini naona Jpm amepungukiwa ktk mbinu za kuikwamua nchi yetu toka ktk umasikini.
Kuna sekta nyingi ambazo serikali hii imeziimarisha ikiwemo madini, sasa hivi mapato yaliyokuwa yanapatikana kwa mwaka sasa yanapatikana kwa siku moja.

maendeleo ya magufuli? maendeleo ya nchi
Maenedeleo yaliyoletwa na Magufuli.
hiy
mwaka jana wakulima wa KOROSHO WALIPORWA KOROSHO ZAO
Wale waliostahili walilipwa.
 
Yeye alianza na kujenga miundombinu ya usafirishaji ili gharama za maisha zipungue na hivyo kupunguza umaskini. Mtu ataweza kutoka Mwanza akaja na treni ya umeme Dar akauza sangara wake na jioni akarudi Mwanza, siku hiyo hiyo.

Ajira zitaongezeka kutokana na urahisi wa kufanya biashara.

Serikali inatoa mkopo wa matrekta kwa bei nafuu, mwaka huu tumepata ziada ya chakula tani milioni 3.32 wakati mwaka 2014 tulikuwa na ziada ya tani milioni 2.3.

Kama maendeleo ndio kitu pekee kinachofanya matawala aungwe mkono, kipi kilitufanya tuwaunge mkono waeusi wa Afrika kusini wakati wazungu waliweka maendeleo mara mia ya haya ya Magufuli?
 
Kama maendeleo ndio kitu pekee kinachofanya matawala aungwe mkono, kipi kilitufanya tuwaunge mkono waeusi wa Afrika kusini wakati wazungu waliweka maendeleo mara mia ya haya ya Magufuli?
Ni wapi nimesema maendeleo ndiyo kila kitu?
 
Back
Top Bottom