Chamoto
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 9,883
- 22,310
Toka awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na maendeleo mengi sana yakifanyika. Iwe ujenzi wa hospitali, barabara, madaraja, reli, ununuzi wa ndege na hata bwawa la umeme. Baadhi yetu umuhimu wa vitu hivi ni dhahir na nia ya Rais iko wazi.
Ukiangalia kwa asilimia nyingi ya maamuzi yake yamelenga katika ujenzi wa mifumo ya usafirishaji.
Hata ukichukulia katika makuzi ya viumbe hai, mifumo ya mwazo kabisa kujengwa wakati mtoto yupo tumboni mwa mama yake ni ile ya usafirishaji. Moyo na mishipa ya damu huanza kujengwa kwanza kabla ya mifumo ya fahamu na mimeng'enyo. Mifumo yote ya viumbe hai hutegemea mfumo wa usafirishaji.
Kama asili yetu imeona umuhimu wa mifumo ya usafirishaji, iweje leo tubeze umuhimu wake katika uchumi?
Sasa kwa kuwa kuna watu wanaopinga Mh. Rais kufufua/kujenga reli, bwawa la umeme na ununuzi wa ndege, basi wao watuambie ni kipi muhimu kufanywa kwanza.
Maendeleo ni nini?