Ali Nassor Px
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,433
- 4,042
Ukimaliza kupanga Mipango yako ya Maisha.. Usisahau kuna kitu kinaitwa KIFO.
Watu tunachukulia poa sana kuhusu hiko kifo lakini kuna ndoto nyingi sana zimezimika. Kuna mabillion ya mawazo ya maana yamezima ghafla tu maana kifo hakina taarifa.
Ukihisi una idea ya kitu usichelewe kufanya hiyo idea yako, fanya haraka sana uanze kuitendea kazi. kwa sababu kuna kitu kinaitwa kifo.
Lengo kuu la kuandika hili sio kutishana laaaasha ila tu jana nilikaa na ndugu yangu akaniuliza swali ambalo kwa haraka haraka nilikosa jibu la kumpa aliniuliza.
HIVI WATU WALIOKUFA NA WALIO HAI WAPI IDADI YAO NI KUBWA ZAIDI?
Nilikosa jibu la kumpa ila baadae nilivyotulia nikapata majibu mazuri tu ambayo hata wewe unaesoma hii post yanakufaa.
Ili binadamu mmoja azaliwe inaitajika miezi 9 ila ili binadamu moja afe inaitaji kama dakika 5 tu.
Na uwezo wa binadamu kuzaliana kwa kila binadamu moja ni mtoto moja tu sasa hebu siku moja nenda pale Mloganzila kwenye geti la out tazama yale magari yanayotoka na maiti yapo mangapi halafu nenda kaombe idadi ya watoto wanaozaliwa kwa siku.
Au unaweza ukajiuliza kwenye familia yako ni wangapi wamekufa na wangapi wamezaliwa jibu litakalo kuja ni kuwa waliokufa ni wengi kuliko waliozaliwa.
Mpaka sasa hivi dunia ina watu Billion 7. 753 Source Worldometer 2020.
Lakini idadi kamili ya waliokufa bado haijalikani kamili maana ukiachana na hospital kuna binadamu wengi sana wanakufa nyumbani.
Wengine kwenye ajali baharini, misituni na sehemu nyingine nyingi tu. Hivyo idadi ya wanaokufa ni kubwa zaidi mno kuliko ya wale wanaozaliwa.
Ukiachana na maradhi ya uzeeni, vita, ukame na majanga mengine lakini unaambiwa kiume adui namba moja duniani anayemaliza watu duniani wala sio simba na wala sio nyoka na wala sio tembo.
Ni mdudu mdogo tu ambae ni MBU kwa mujibu wa WHO(SHIRIKA LA AFYA DUNIANI )
MBU anaua binadamu laki moja kwa mwaka kwa magonjwa kama malaria na homa ya manjano.
Sasa unaweza ukapiga hesabu mwaka mmoja wanakufa watu laki moja lakini binadamu ili azaliwe anaitaji kukaa tumboni kwa mama yake ndani ya miezi 9.
Kwahiyo vijana sipo hapa kwa ajili ya kutishana hapana ila ni kukumbushana. Ukipata nafasi itumie tufanye ibada kwa sana.
Tujitahidi kuishi vizuri na watu ili tuache kumbukumbu nzuri katika fikra na mawazo ya watu kama tulivyozaliwa tulikuwa tunalia na ndugu jamaa na marafiki walifurahi na walikuwa na furaha kuongeza member mpya ndani ya jamii na familia basi.
Pia tuishi na watu vizuri ili hiyo siku tukifa wao walie sisi tuwe na furaha uko tuendako.
Kumbuka pia ukipoteza pesa unaweza ukaitafuta ukaipata pesa nyingine lakini ukipoteza uhai ndo imeisha hakuna aliyewahi kwenda akarudi.
Jitunze pia jali sana Afya yako.
Mwandishi ; Ali Nassor