Elections 2010 Watu wajitokeza kwa wingi

wihanzi

Member
Feb 10, 2009
62
3
Wakuu, nimemaliza kupiga kura, na pia nimepita katika vituo kadhaa jimbo la kawe, lakini nasikitika kusema kuwa idadi tuliyoitegemea katika uchaguzi huu ni ndogo sana sielewi tatizo ni nini. Wanajamvi hebu tupeni data za maeneo mengine mlipo vinginevyo ninawasiwas sana na ule uchangamfu niliouona wakati wa kampeni.

Au hiyo milioni 19 tuliyoambiwa inawalakini?
 
Kweli Vijana Na Wanaume wamejihimu kupiga kura mapema sana. Kuanzia mchana watu wamekatika kabisa vituoni. Ni takribaki zimebaki dk 40 vituo vifungwe na hakuna sudden flow ya watu kwenye hizi dk za majeruhi kama ilivyozoeleka. Waliokaribu na vyombo vya hbr chondechonde wahimizeni watu wajitokeze na waondoeni hofu juu ya foleni.
 
Sasa kama wasimamizi na mawakal watabaki peke yao vituoni, si ndio muda wa kunanihiino?, nina mashaka hapo!!
 
Nilifika kituoni 6:00am sharp, Kinyerezi Dar. Na nilikuta wananchi wenzangu wapo kituoni. Nilikuwa wa 15 hivi kupiga kura mara tu baada ya vituo kufunguliwa saa moja sharp. Nadhani wengi wamepiga asubuhi.

Lakini pia wengine wanaogopa jua. Kuna mmoja amedai kichwa kinamgonga sana hawezi kusimama juani. Wa ndugu wa vyombo vya habari watusaidie kuhamasisha kwani jua limepoa.
 
Nani anayesema turn out is very poor? Watu wengi wamepiga mapema zaidi..

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom