Watu wa zamani #4

Watu wa zamani #4

kafumo

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
26
Reaction score
15
Watu wa zamani walijifanyia hazina za vitu vya thamani kwao wenyewe.
Ndani ya hazina zao palikuwepo na thamani za aina mbalimbali ikiwemo elimu au maarifa ya kimaandiko, michoro , alama na vitu vingine.

Maandiko, michoro na alama vilikuwa ni maelekezo ya uhalisia wa jambo flani.
Hata sasa ni wazi kuwa unaweza kusimulia au kusimuliwa jambo flani lakini usielewe namna za ndani za uhalisia wake mpaka kudhihilika kwake hilo jambo.

Pamoja na mambo yote, maandiko mengine au ujuzi mwingine ulionekana chanzo chake kuwa ni ajabu kwa watu hasa wale walio kuwa hawafahamu usomi wa elimu na maarifa ya kale hiyo na hata sasa.

Kama ambavyo hata sasa unaweza kuwa na kitu na usielewe kama unaweza fanya hivi na hivi ikawa hivi, lakini akija mtu au kitu chenyewe au mtu mwenyewe kwa hiari yake akakueleza au hata kwa kumuomba na kweli ikawa katika uhalisia kwa jinsi na namna ya maelekezo yake basi mtu unaamini na kukiishi kitu hicho ikiwa kina manufaa kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom