Watu wa Protocol tafadhalini mpeni training ya Public Speaking Mama Janet Magufuli

Mada ni nzuri, lakini tusichanganye mtu anayejishusha na mtu mwoga.

Historia inasema wake wa maraisi wana mamlaka makubwa sana ya kinadhifa.

Haya mamlaka huwezi ukayaona, lakini akimua kesho mume wake aamke na mood gani, hakika anaweza.

Inawezekana anahitaji public speaking skills, lakini tutizame ujumbe anao utoa kuliko mtizamo wa nje.
 
Tanzania nchi yangu!
Tulihoji miaka michache iliyopita" uhalali wa Mama Salma jk kupewa public speak wakati wa ziara za kiserikali za rais. Tukahoji mbona enzi za mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere hakuwa anapewa nafasi ya kuzungumza kwenye hadhara?
Haya Mama Janeth, watanzania wanataka uzungumze,.
 
Bado anaikumbuka "mwaisela" chezea mkong"onto weye!

Huyu wetu anamzidi Hitler kwa uzober,
(Hitler alikuwa anakula vitasa kwa mkewe)
 
Tanzania nchi yangu!
Tulihoji miaka michache iliyopita" uhalali wa Mama Salma jk kupewa public speak wakati wa ziara za kiserikali za rais. Tukahoji mbona enzi za mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere hakuwa anapewa nafasi ya kuzungumza kwenye hadhara?
Haya Mama Janeth, watanzania wanataka uzungumze,.

Ulioji peke yako,hakuna mtu alieoji hivyo.
 
pengne hakujikua kua kuna siku atakua first lady nikama lilikuja ghafla na kuongea mbele ya watu wengi sio mchezo hasa kwa wanawake acording to her culture
 
umenikumbusha kuna speach moja iv mweshimiwa akaongea maneno ya kiingereza akasema to higher and fire the ecomic kwa msisito ilinifanya nicheke sana
 
Mama magufuli namkubali saana anayo haiba ya ualimu hadi sasa ,nadhani kipindi chake cha kukaa ikulu kikifikia ukomo atarudi kufundisha
 
Juzi nilimuona wakati anatoa msaada kwa wazee huko chato, anaongea kama vile anatetemeka yaani hana confidence ya kusimama mbele ya kundi la watu wengi,

Hilo tatizo lipo kwa watu wengi sana... Kujieleza mbele za watu
Wanawake wote wanaoamini waume zao wanawapenda na wako tayari kuwa support wakati wowote na hasa kama wanapewa haki yao ya kitandani sawa sawa huwa na confidence muda wote wakati wowote wanapopewa fursa.
 
Wanawake wote wanaoamini waume zao wanawapenda na wako tayari kuwa support wakati wowote na hasa kama wanapewa haki yao ya kitandani sawa sawa huwa na confidence muda wote wakati wowote wanapopewa fursa.
Unataka kusemaje mdau. Hitimisha sasa
 
Nitoe tu ombi langu la Kipekee kabisa kwa Watu wa Itifaki ( Protocol ) hasa wale mliopo Ikulu hebu jitahidini basi muweze kumpa mafunzo ( training ) maalum ya Public Speaking Mama yetu mpenda First Lady Janet Magufuli.

Leo si mara yangu ya Kwanza kuona kila anapopewa nafasi ya kusema chochote au kuzungumza na halaiki huwa anakuwa hana la kusema sana lakini pia huwa anakuwa na aibu na hata akimaliza kuzungumza anaonekana ni Mtu anayetetemeka hivi.

Kinachoniuma kama siyo kunisikitisha huu ni mwaka wa pili sasa nyie Watu wa Protocal hapo Ikulu mpo nae huyu Mama yetu mpendwa lakini sijui ni kwanini mmeshindwa kumsaidia Mama yetu kwa hili la Yeye kutokuwa mzuri katika Public Speaking.

Najua kuzungumza katika halaiki kubwa si jambo rahisi ila kama akipewa mafunzo maalum na Yeye pia akiwa tayari basi ataweza kumudu na kuwa mzungumzaji mzuri sana. Ni jambo la aibu na si zuri pia kwa Mke wa Rais kila anapopatiwa nafasi ya kuzungumza anabaki tu kuchekacheka na kuzungumza kwa Sekunde 13 hadi 17 kisha anarudi Kitini.

Katika maisha yangu yote sijawahi kuona Mwalimu anakuwa hawezi kufanya Public Speaking ila labda Mama yetu anashindwa kwakuwa muda mwingi alikuwa anazungumza tu na Wanafunzi Watoto wa pale Shule ya Msingi ya Mbuyuni alipokuwa akifundisha kwa miaka mingi achila mbali kuwa pia alisoma hapo hapo alipokuwa Mwanafunzi miaka hiyo.

Binafsi huwa nina hamu sana pale nikiona anapewa muda wa kuzungumza na halaiki basi aje mbele na azungumze mambo mengi ya maana ili kufukia ' mashimo ' ambayo pengine Mumewe aliyasahau kitu ambacho kitazidi kufanya Watu wamuamini, wampende na waamini kuwa kweli Mheshimiwa Rais ana ' Jembe ' la uhakika.

Tafadhali Mke wa Rais Mama Janet Magufuli apatiwe haraka sana mafunzo ya Public Speaking na Yeye mwenyewe pia ajitahidi kuondokana na hiyo aibu aliyonayo ambayo kiukweli na nafasi yake ya sasa aliyonayo hapashwi kuwa nayo.

Yangu ni hayo tu na ni matumaini yangu ushauri wangu huu utazingatiwa na kuanzia siku za baadae nitamuona Mama Janet Magufuli mpya anayechangamka, anatoa madini tupu mdomoni mwake na mpambanaji kama ambavyo tunawaona Wake wa Marais wengine sehemu mbalimbali duniani.

Akhsanteni na nawasilisha.
Mkuu umesema kweli lakini juwa huyu mama hapo mjengoni hayupo kwa amani kabisa na anaishi kwa basi tu lakini ukweli akipewa hata nafasi leo ya kukaa pembeni atona ni bora kuliko kuwepo humo ila labda kama kuna mtu hajui undani wa humo.
 
Back
Top Bottom