Natafuta Watu wa kung'oa visiki shamba heka mbili Mlandizi

The bump

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,136
1,952
Natafuta Watu wa kung'oa visiki shambani kwangu Mlandizi, shamba halina visiki vikubwa ni visiki vya miti size ya mkono wa mtu mzima.

Ukubwa ni Heka Mbili, Mtu au Watu watakaofanya hii kazi ni lazima Wakae huko huko shamba kwa kipindi chote watakachokua wakifanya hiyo kazi ili kuepuka gharama za nauli.

Kutoka Mlandizi stand hadi Shamba nauli kwa bodaboda ni 5000 Daladala 2500.

Chakula na Malazi itakuaa juu yangu mimi maana itajengwa kambi pale pale kiwanjani so baada ya kazi kuisha watu watapewa Chao wataondoka.

Kwa yeyote mwenye anajua watu wanaoweza fanya hiyo kazi Tuwasiliane kazi haihitaji watu zaidi ya wawili kwa kuokoa muda.

Ila ni kazi ya kufanya hata mtu 1.
 
Kuna kikosi cha wagogo wanne hiyo kazi wanaweza kuimaliza ndani ya siku 3. Ila ofa ya 70 naona kama ni ndogo vile
 
Mkuu hii kazi uliifanya kwa bei gani?
Sikuifanya mkuu, niliajiri vijana ambao wapo shamba wanakaa huko huko nawalipa kwa mwezi, wao ndio walitoa hivyo visiki na kazi zingine zote za pale wanazifanya, mimi na wao malipo ni mwisho wa mwezi.

Nilifikiria kung'oa tu visiki nilipe watu kisha waondoke, ije kazi nyingine nilipe watu tena kisha waondoke nikaona ni uchezeaji pesa kwakuwa malengo ya mbele nayajua basi ikabidi niajiri vijana, nimefanikiwa pata wawili.

Hapa natafuta wa mwisho mmoja waungane wawe watatu kisha rasmi nikianza project zangu najua nina majembe yangu matatu.
 
Nicheki na mimi Nina site yangu uku ninao wanakaa hapa hapa na Bei Yao Ni nzuri tu kama uko serious nicheck niku link Mara moja
 
Back
Top Bottom