Watu wa kipato cha chini wanaongoza kujenga nyumba sababu ya janja-janja nyingi!

Kuna vijana wengi sana kwa sasa wanastrugle wapate hata vyumba 2 lakini hali imekua ni tete...
Fursa hakuna
 
Mkuu wewe fanya utunze hela zako ujenge majumba yako utakavyo lakini hela za mwingine na jinsi anavyozitumia haikuhusu..

Unakuta wakati mtu anasoma na kuhangaika kuzitafuta hela watu wanamkatisha tamaa na kukejeli .
Siku akipata hela ndio mnajifanya mnajua kupangiana budget eti sijui uanze kujenga kabla ya kununua gari..

Tafuta hela zako zitumie utakavyo sio kupangiana..

ASANTE
Kuanza kujenga kabla ya kununua gari ni uoga wa maisha mkuu.....
Nunua gari nyumba itakujaga tu polepole
 
Mkuu wewe fanya utunze hela zako ujenge majumba yako utakavyo lakini hela za mwingine na jinsi anavyozitumia haikuhusu..

Unakuta wakati mtu anasoma na kuhangaika kuzitafuta hela watu wanamkatisha tamaa na kukejeli .
Siku akipata hela ndio mnajifanya mnajua kupangiana budget eti sijui uanze kujenga kabla ya kununua gari..

Tafuta hela zako zitumie utakavyo sio kupangiana..

ASANTE
Haki ya nani wewe unajua Mo alipo.
 
Nimekaa na baadhi ya watu wa kipato cha chini ambao wamejenga nyumba, ukisikia trick zao, then unaona kuwa hata hawa wasomi wangefuatisha wao, basi wangeweza kutoboa.

Kiwanja:
Wakati wewe unangoja upate milioni ishirini za kununua kiwanja Goba, Makongo juu, Kinyerezi nk. watu wa kipato cha chini hukimbilia nje nje ya mji ambapo kuna viwanja vya bei chee, hadi kwa tsh milioni moja...

Material za ujenzi
Wakati wewe unatafuta hela ya kukodi 'Mende' likuletee kokoto ambazo zinagharimu hadi Tsh 1.6M, mtu wa kipato cha chini ananunua kokoto za kwenye viroba ambavyo huuzwa hadi Tsh 1500 kwa kiroba.

Wakati wewe unatafuta hela ya kununua bati za Msouth, mtu wa kipato cha chini ananunua haya mabati ya bei nafuu ya mchina au ALAF na kuezeka kwa gharama nafuu.

Wakati wewe unatafuta pesa ya kununulia milango ambapo mlango mmoja hugharimu milioni moja, mwenzako wa kipato cha chini anaagiza milango toka Songea au Moshi ambapo ataipata kwa sh laki mbili.

Wakati wewe unaendelea kusubiri muujiza wa kujenga mansion, mwenzako wa kipato cha chini anakuwa ameshamaliza nyumba yake ya vyumba vitatu na kuja kukupangisha wewe unayeishi kwenye ndoto huku akikucheka.

Jamani graduates mlioko maofisini, amkeni.... Hii life style ya kutanua na kutumia magari inawanyonya sana.

Gari kama linakughariimu Tsh laki tatu hadi nne kwa mwezi, kwa mwaka ni karibu M5. Hapo bado hujalinunua. Ukiuza gari lako leo, ukaibuka Chanika unapata kiwanja cha m3, na milioni mbili nyingine unaanza ujenzi, ndani ya mwaka mmoja hadi miwili unajikuta unakaa kwako ukiwa na uhuru wa kuendelea na bata zingine kama vile kumiliki magari ya kifahari, kula tours nje ya nchi na kuvaa vizuri nk.

Maisha ya kupanga ni maisha ya kutanga tanga... Kuna mahali nyumba za kupanga zinatiwa nyumba za kutanga tanga!
Umenena
 
Hili wazo la ujenzi kidogokidogo ni Wazo chanya kwa ubongo wa Bin-Adam!!
IMG-20180928-WA0026.jpeg
 
Wazo zuri sana 🔥
 
Ni sawa mkuu lkn tofauti ya kujenga na kupanga ni kuwa,anayepanga analipa kodi rejareja ila anayejenga ameamua kulipa kodi ya jumla ss kiuchumi sio afya ndo mana tunashauri uinvest hyo pesa then sehemu ya faida jengea utapata double benefits.
Je uki invest halafu usipopata faida ? mayolo au sio 😂😂😂😂😂
 
Tunao wengi mkuu,mtu anajenga km kashkiwa bunduki afu anahaha hata hela ya kula anataka akope na kibaya zaidi anakuwa kajiwekea ugumu mwenyewe watu wanaona zako ukajengee afu zangu zikalishe familia yako!
Nimecheka hadi nimelia ndg
Wabongo mna mambo jamani
 
Mkuu elimu nayo ina gharama kubwa.
Unajenga kwa gharama ya mara tatu ya msomi.
Nyumba haina hata barabara ya kufika huko,eneo halijapimwa.
Sebule yako choo cha jirani!
Kama barabara ipo bajaji hazipishani.
Kama ukibahatika kupata gari, unalaza ofisi za Chama!
Kokoto Tshs 1,500 kwa mfuko wa kilo 20 unajua ni kiasi gani?
Hiyo ni Tshs 900,000 kwa gari ya tani 12.
Kama unge agiza gari nzima ni laki tatu au tatu na nusu.
Umasikini una gharama ila hatuzioni.
kwa hiyo ulale kwenye gari na familia. toa mawazo mbadala
 
Mkuu nakuelewa sana unachomaanisha,kimtazamo kwny hili suala la makazi nahisi tuko sawa. Shida ya watu wa hali duni huwa wanaona rejareja ni too cheap simply bze they cant afford to pay at once. Mtu anakimbilia kujenga then analala njaa hana hela ya kula,unajiuliza hyu mtu yuko timamu? Angedunduliza hyo hela akainvest then faida ndo aelekeze kwny ujenzi!
Dunduliza ya kipato cha bongo ili zijae ujenge ni ndoto. Anza kujenga na kiroba na mfuko mmoja wa cement
 
Back
Top Bottom