Watu wa kipato cha chini wanaongoza kujenga nyumba sababu ya janja-janja nyingi!

Sasa vipato vinatofautiana ndio maana sio wote tunataka kukaa nje ya mji au kujenga nyumba kama polisi post
 
Nimekaa na baadhi ya watu wa kipato cha chini ambao wamejenga nyumba, ukisikia trick zao, then unaona kuwa hata hawa wasomi wangefuatisha wao, basi wangeweza kutoboa.

Kiwanja:
Wakati wewe unangoja upate milioni ishirini za kununua kiwanja Goba, Makongo juu, Kinyerezi nk. watu wa kipato cha chini hukimbilia nje nje ya mji ambapo kuna viwanja vya bei chee, hadi kwa tsh milioni moja...

Material za ujenzi
Wakati wewe unatafuta hela ya kukodi 'Mende' likuletee kokoto ambazo zinagharimu hadi Tsh 1.6M, mtu wa kipato cha chini ananunua kokoto za kwenye viroba ambavyo huuzwa hadi Tsh 1500 kwa kiroba.

Wakati wewe unatafuta hela ya kununua bati za Msouth, mtu wa kipato cha chini ananunua haya mabati ya bei nafuu ya mchina au ALAF na kuezeka kwa gharama nafuu.

Wakati wewe unatafuta pesa ya kununulia milango ambapo mlango mmoja hugharimu milioni moja, mwenzako wa kipato cha chini anaagiza milango toka Songea au Moshi ambapo ataipata kwa sh laki mbili.

Wakati wewe unaendelea kusubiri muujiza wa kujenga mansion, mwenzako wa kipato cha chini anakuwa ameshamaliza nyumba yake ya vyumba vitatu na kuja kukupangisha wewe unayeishi kwenye ndoto huku akikucheka.

Jamani graduates mlioko maofisini, amkeni.... Hii life style ya kutanua na kutumia magari inawanyonya sana.

Gari kama linakughariimu Tsh laki tatu hadi nne kwa mwezi, kwa mwaka ni karibu M5. Hapo bado hujalinunua. Ukiuza gari lako leo, ukaibuka Chanika unapata kiwanja cha m3, na milioni mbili nyingine unaanza ujenzi, ndani ya mwaka mmoja hadi miwili unajikuta unakaa kwako ukiwa na uhuru wa kuendelea na bata zingine kama vile kumiliki magari ya kifahari, kula tours nje ya nchi na kuvaa vizuri nk.

Maisha ya kupanga ni maisha ya kutanga tanga... Kuna mahali nyumba za kupanga zinatiwa nyumba za kutanga tanga!
Mtu wa Mpitimbi Utamjua tu, hasa wa maporini hawawezi ongea bila kutaja taja kwao, hapa tumefahamu Wewe wa Songea
 
Usiipambe mkuu, gari ni investment ya anasa/luxury! Iko wazi, unainvest katika kitu kinachokumalizia pesa taratibu! 300000-400000 kwa mwezi jumlisha na za wear and tear! Matairi,oil,brake pads,plug n.k!
Ha haaa,siipambi mkuu kwa tafsiri maendeleo ni kuhama toka hatua moja kwenda nyingine iliyo bora kuliko ya awali,so kwa tafsiri hyo km ulikuwa unatembea kwa mguu/daladala/baiskel nk ukanunua gari ni development. Problem ni km umenunua gari kwa ajili ya ufahari huku linakunyonya utakuwa huna tofauti na anayejenga huku ubavu mdogo,kwa zama hizi gari is no longer luxurious!
 
Mtu anayejenga maana yake ana investment tayari. Sasa wewe unadhani kujengea mshahara utaweza! Mishahara yenyewe mingi ni chini ya million moja, af makato kibao...Ndio yale unajenga watoto wanateseka na dagaa miaka 7 kisa unajenga, kwa mangi mideni kibao!
Tunao wengi mkuu,mtu anajenga km kashkiwa bunduki afu anahaha hata hela ya kula anataka akope na kibaya zaidi anakuwa kajiwekea ugumu mwenyewe watu wanaona zako ukajengee afu zangu zikalishe familia yako!
 
Mimi nimeapa sitaki kukaa sehemu ambayo haijapimwa.Nashukuru Mungu sijawahi kaa sehemu kama hizo tangu mwanzo.
Sikuhizi maeneo yaliyopimwa ni mengi sana tena unalipa kwa awamu kadhaa.Kwanini nihamie sehemu halafu nianze kuhesabu nimebakiza nguzo ngapi umeme ufike nyumbani.Hapana!
 
Sasa vipato vinatofautiana ndio maana sio wote tunataka kukaa nje ya mji au kujenga nyumba kama polisi post
Hata mimi mkuu huwa siwazi kujenga sababu kuna kiwanja cha bei rahisi huko sijui wapi, afu tabia ya kukaa na watu wa chini(mnisamehe) nilishakataaga unazalisha problemz nyingi sn kwny maisha. Yaani unaweza haribu hadi kizazi sababu ya watu wanaokuzunguka tu.
 
Tunao wengi mkuu,mtu anajenga km kashkiwa bunduki afu anahaha hata hela ya kula anataka akope na kibaya zaidi anakuwa kajiwekea ugumu mwenyewe watu wanaona zako ukajengee afu zangu zikalishe familia yako!
Huo ufala ndio sifanyi, yani nijenge kwa mateso kiasi hicho!?
 
No wonder tuna vibanda vingi badala ya nyumba, kama wajenzi wenyewe ndio sampuli hii?!
 
Wengine hawataki kuhama kinondoni na kuishi sehemu nyengine et! kisa yeye na Lady J dee ni majirani hahahaa! ujinga mbaya anaona akiondoka kinondoni na kumwacha jirani yake msanii atakuwa kapotea. Watoto wa marehemu Majungu wa pale kinondoni hananasif baada ya kufa baba yao waliuza mjengo na kupiga kama 600mil wakagawana na kila mtu katimukia anapopajua sas hivi wametulia.
 
Nimekaa na baadhi ya watu wa kipato cha chini ambao wamejenga nyumba, ukisikia trick zao, then unaona kuwa hata hawa wasomi wangefuatisha wao, basi wangeweza kutoboa.

Kiwanja:
Wakati wewe unangoja upate milioni ishirini za kununua kiwanja Goba, Makongo juu, Kinyerezi nk. watu wa kipato cha chini hukimbilia nje nje ya mji ambapo kuna viwanja vya bei chee, hadi kwa tsh milioni moja...

Material za ujenzi
Wakati wewe unatafuta hela ya kukodi 'Mende' likuletee kokoto ambazo zinagharimu hadi Tsh 1.6M, mtu wa kipato cha chini ananunua kokoto za kwenye viroba ambavyo huuzwa hadi Tsh 1500 kwa kiroba.

Wakati wewe unatafuta hela ya kununua bati za Msouth, mtu wa kipato cha chini ananunua haya mabati ya bei nafuu ya mchina au ALAF na kuezeka kwa gharama nafuu.

Wakati wewe unatafuta pesa ya kununulia milango ambapo mlango mmoja hugharimu milioni moja, mwenzako wa kipato cha chini anaagiza milango toka Songea au Moshi ambapo ataipata kwa sh laki mbili.

Wakati wewe unaendelea kusubiri muujiza wa kujenga mansion, mwenzako wa kipato cha chini anakuwa ameshamaliza nyumba yake ya vyumba vitatu na kuja kukupangisha wewe unayeishi kwenye ndoto huku akikucheka.

Jamani graduates mlioko maofisini, amkeni.... Hii life style ya kutanua na kutumia magari inawanyonya sana.

Gari kama linakughariimu Tsh laki tatu hadi nne kwa mwezi, kwa mwaka ni karibu M5. Hapo bado hujalinunua. Ukiuza gari lako leo, ukaibuka Chanika unapata kiwanja cha m3, na milioni mbili nyingine unaanza ujenzi, ndani ya mwaka mmoja hadi miwili unajikuta unakaa kwako ukiwa na uhuru wa kuendelea na bata zingine kama vile kumiliki magari ya kifahari, kula tours nje ya nchi na kuvaa vizuri nk.

Maisha ya kupanga ni maisha ya kutanga tanga... Kuna mahali nyumba za kupanga zinatiwa nyumba za kutanga tanga!
Natafakari
 
Mkuu nakuelewa sana unachomaanisha,kimtazamo kwny hili suala la makazi nahisi tuko sawa. Shida ya watu wa hali duni huwa wanaona rejareja ni too cheap simply bze they cant afford to pay at once. Mtu anakimbilia kujenga then analala njaa hana hela ya kula,unajiuliza hyu mtu yuko timamu? Angedunduliza hyo hela akainvest then faida ndo aelekeze kwny ujenzi!
Tatizo kwa namna jamii zetu zilivyo asingeweza kudunduliza. Hela ikipatikana haikosi kazi
 
Kuna jamaa hapa nimepanga kwake huwa anakusanya mchanga barabarani mwenyewe ananunua mifuko ya simenti hata mi5 tu anatengeneza matofali mwenyewe anajenga chumba ki1
Anabonge LA nyumba
 
Maisha sio gwaride kwamba ukiambiwa nyuma geuka wote mnageuka kwa pamoja
 
Kujenga kunataka ujasiri sana vlvl hasa kama kipato cha kuunga unga
Nakumbuka miongoni mwa naamini yalikuwa maamuzi magumu na sahihi ilikuwa kuamua kujenga. Nakumbuka miaka mitatu iliyopita nilikuwa nakaa Sinza nyumba sh 300,000/mwezi nalipankodi kwa mwaka mzima wala sijali. Lkn kuna siku jamaa yangu alikwama alikuwa na mkopo benki, biashara zake zikawa haziendi vema. Jamaa kanichukua hd Kigamboni na kunionyesha kiwanja kina pagale na kunimbia anauza mil 15 tu japo gharama ya eneo lile ni kubwa. Maana ukicheki upande wa pili unavuka lami thwn kuna beach, kuna vlvl privte beach za watu wenye pesa. Moyo ulipiga paaah! Kucheki akaunt ina akiba ya mil 3.4 hv. Nilichofanya ni kumpa mil 3 na then kufanya maamuzi ya kuuza gari yangu ambayo alhamdulillaah niliiuza kwa mil 18.
Jamaa zangu walinicheja kwa maamuzi ya kurudi kupanda daladala. Nikaona isiwe shida, nikapambana sana baada ya miezi 6 nyumba ikawa imekamilika na kuhama Sinza. Ss hv hali ilivyokuwa ngumu jamaa zangu walionicheka hd nawaonea huruma jinsi kodi zinavyowasumbua.
Na kizuri zaidi nafurahi jamaa na watu wengi wanakuja huku kubarizi upepo wa beach wanalipa na viingilio wakati mm huku ni nyumbani! Vlvl kutoka kwangu hadi Ferry hata nikiamua kutembea hazizidi dkk 15! Na ukivuka tu Ferry tyr nipo maeneo ya ofcn
Kuwa na nyumba hapa Dar kuna raha sana! Big up sana baba na mama mwenye nyumba!
IMG20181003175452.jpeg
 
Nyumba ina raha yake aisee, kuna mzee aliniuliza kodi ninayolipa nikamwambia ni 150k kwa mwezi, akasema ni pesa nyingi sana yeye aliajenga nyumba kwa kuuza Maembe pale kigamboni,
Anayatoa shamba huko tundwi songane anauza ,kaweka wapangaji mambo yanaenda...
Kimsingi kodi inaumiza sana Kwa mjini, rotation ya kodi iko karibu sana kiasi kwamba kinachobaki katika mshahara unabaki kula , kunywa na mavazi
 
Back
Top Bottom