Watu saba waliopotea katika mazingira ya kutatanisha

Watu saba waliopotea katika mazingira ya kutatanisha

Mwaka 2016 bibi wa miaka 98 alipotea pia hadi sasa aijulikani halipo.

Alipotea pasipo kuondoka na kitu chochote ikiwa pamoja na fimbo aliyokuwa akitumua kutembea.
 
Nasubiri kwa hamu mkuu sema tu sijui nazipata wapi hizi mambo, pia nyenzo sina..
Mtandaoni, mkuu na documentary youtube halafu kuna IDx so ukachanganya hizi sources tatu unapata full package ya story nzima maana kote kote unachukua details za same story
 
Mtandaoni, mkuu na documentary youtube halafu kuna IDx so ukachanganya hizi sources tatu unapata full package ya story nzima maana kote kote unachukua details za same story
Mkuu ulielewa nini niliposema "Nyenzo"..?
 
Mkuu ulielewa nini niliposema "Nyenzo"..?
Hahaha kwanza kilichoniijia kichwani ni simu au computer au tv yenye channel z haya mambo, ila nikajiuliza kama ni hivyo mbona uko humu jf basi utakuwa walau una access na simu.
Basi nikahisi labda ulikosea andika ulimaanisha vyanzo (source).
 
Hahaha kwanza kilichoniijia kichwani ni simu au computer au tv yenye channel z haya mambo, ila nikajiuliza kama ni hivyo mbona uko humu jf basi utakuwa walau una access na simu.
Basi nikahisi labda ulikosea andika ulimaanisha vyanzo (source).
Source zangu kuu hua ni Chaneli ya Da Vinci Learning, Jf na muvi tofauti za Ki_Intelligence.
Nyenzo.
Pc/phones
Bundles..
 
Source zangu kuu hua ni Chaneli ya Da Vinci Learning, Jf na muvi tofauti za Ki_Intelligence.
Nyenzo.
Pc/phones
Bundles..
Hapo safi hiyo da vinci ndiyo ile iko star times sometimes uwa kuna vipindi vya kuwafunza watoto?
 
Hapo safi hiyo da vinci ndiyo ile iko star times sometimes uwa kuna vipindi vya kuwafunza watoto?
Yeah ila fuatilia vipind vinavyo anza saa tatu usiku kuendelea hua vipo vizur..
Pia Discovery
 
Yeah ila fuatilia vipind vinavyo anza saa tatu usiku kuendelea hua vipo vizur..
Pia Discovery
Yah hata mimi uwa natazama discovery na national geographic mfano kuna kipindi walielezea history ya science ilivyosaidia kusolve crimes wakaanza na historia ya fingure print wakaelezea kisa kimoja miaka hiyo ya zamani mama aliua watoto wake halafu akamaingizia ex wake so akakamatwa akateswa ila kuna jamaa ndiye father wa fingure print ndiye alikuja kusolve hiyo crime wakaja kwenye dna sasa hiyo ndiyo inavutia ilikuwa inamhusisha serial killer mmoja aliwasumbua police kwa miaka kadhaa na alikuwa anaibika anaua mfululizo then anapotea kama mwaka ipo siku ntaandika hiki kisa.
 
Yah hata mimi uwa natazama discovery na national geographic mfano kuna kipindi walielezea history ya science ilivyosaidia kusolve crimes wakaanza na historia ya fingure print wakaelezea kisa kimoja miaka hiyo ya zamani mama aliua watoto wake halafu akamaingizia ex wake so akakamatwa akateswa ila kuna jamaa ndiye father wa fingure print ndiye alikuja kusolve hiyo crime wakaja kwenye dna sasa hiyo ndiyo inavutia ilikuwa inamhusisha serial killer mmoja aliwasumbua police kwa miaka kadhaa na alikuwa anaibika anaua mfululizo then anapotea kama mwaka ipo siku ntaandika hiki kisa.
Wapo vzr sana hao mkuu..
Walinikosha kwenye kisa cha Jesus &Marry Magdarene..
Walichambua vzr sana japo sidhani kua ni Ukweli..

Da vinci Learning niliipenda na kuuanza kuifuatilia Siku moja walivyo elezea Jinsi Herufi zilivyo vumbuliwa pia Jinsi Wamisri walivyojenga mapiramids..

Kiukweli ktka Startimes hii ndio My favourite Channel followed by Bollywood swahili & kung fu 1
 
Wapo vzr sana hao mkuu..
Walinikosha kwenye kisa cha Jesus &Marry Magdarene..
Walichambua vzr sana japo sidhani kua ni Ukweli..

Da vinci Learning niliipenda na kuuanza kuifuatilia Siku moja walivyo elezea Jinsi Herufi zilivyo vumbuliwa pia Jinsi Wamisri walivyojenga mapiramids..

Kiukweli ktka Startimes hii ndio My favourite Channel followed by Bollywood swahili & kung fu 1
Tatizo mimi sina startimes natumia azam ila nilienda sehemu siku moja nikakuta wameka hiyo channel
 
1. Tarehe 9, mwezi wa pili mwaka 2004, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Massachusetts aliyejulikana kwa jina la Maura Murray, alituma email kwa maprofesa wake aliwataarifu kuwa hatakuwa chuoni kwakuwa inabidi ahudhurie msiba wa kifamilia (ilikuja kubainika siyo kweli kwamba kulikuwa na msiba).

Usiku wa siku hiyo Maura alipata ajali alipokuwa akiendesha gari pale alipogonga mti katika mji wa Woodsville, New Hampshire. Siku kadhaa nyuma, Maura alikuwa amepata ajali nyingine wakati akiendesha gari hivyo basi, hiyo ilikuwa ajali ya pili ndani ya week mbili.

Dereva wa basi alimfuata akamuuliza kama ameumia akamjibu hajaumia na akamuuliza kama amsaidie kuwataarifu polisi, Maura akakataa ila dereva aliondoka akaenda kwenye banda la simu na kuwataarifu polisi. Baada ya dakika kama kumi polisi walifika ajabu Maura hakuwepo eneo la tukio.

Hakukuwa hata na alama za miguu labda kuashiria kuwa aliondoka wala hakukuwa na dalili zozote zinazoonyesha vurugu ya hali yoyote kwenye eneo la tukio.
Kesho yake mchumba wa Maura alipokea ujumbe wa sauti unaosadikiwa ulitoka kwa Maura ila anasikika akilia tu. Yapata miaka kumi na tatu toka apotee, japo Maura alionyesha tabia zisizoeleweka siku kadhaa kabla ya kupotea kwake, ila wazazi wake hawaini kama aliondoka kwa mapenzi yake.

e9b80ab25fca91072a8889ae8b610bf9.jpg


2. Brandon Swanson, huyu wakati alipopotea alikuwa na umri wa miaka 19, tarehe 14, mwezi wa tano mwaka 2008.

Siku hiyo Brandon alikuwa akiendesha gari kurudi nyumbani kwao Marshall, Minnesota wakati akipita kwenye barabara ya chagarawe gari lake liliingia na kunasa kwenye shimo pembeni ya barabara.

Brandon aliwapigia wazazi wake na kuwaomba wamfuate ila wazazi wake walipofika, hawakumkuta na baba yake alipompigia simu Brandon alimwambia ameamua kuelekea mji Lynd ambao uko karibu na hapo ila katikatiki ya mazungumzo yao baba yake alisikia Brandon akisema "Oh my God" na simu ikakatika.

Kila alipojaribu kumpigia simu ilikuwa haipatikani. Polisi walipojaribu kumtafuta hawakumpata wala kuweza kutambua ilipo simu yake, hivyo wakahisi labda alianguka mtoni lakini upekuzi wa mto hakuzaa matunda.

Mpaka leo hajapatikana na hakuna anayejua kwanini alisema Mungu wangu.

3116da15f3364fec342b620ca66a18b4.jpg


3. Lois Le Prince. Huyu alikuwa mvumbuzi wa kifaransa ambaye ndiye inasemekana alikuwa mtu wa kwanza kuchukua picha zimazotembea kwenye filamu.

Huyu ndiye baba wa cinematography ila anakumbukwa kwa tukio lake la kupotea bila maelezo. Tarehe 16, mwezi wa 9, mwaka 1890, Le Prince alimtembelea kaka yake aliyekuwa akiishi katika mji wa Dijon, Ufaransa na baadae alipanda gari moshi kuelekea Paris.

Gari moshi lilipofika Paris, Le Prince hakuwemo kwenye gari moshi alikuwa kapotea katika mazingira ya kutatanisha. Mara ya mwisho mtu yoyote kumwona Le Prince ni pale alipoingia kwenye chumba chake katika gari moshi baada ya kuhifadhi mizigo yake katika chumba kingine, lakini mizigo yake haikuwepo wala yeye mwenyewe hakuonekana tena.
Hakukuwa na dalili zozote za kuonyesha labda kulikuwa na vurugu, hakuna mtu aliyemuona akitoka chumbani, madirisha ya chumba hicho cha gari moshi yalikuwa yamefungwa kama kawaida, hivyo wazo la kwamba labda alijirusha kupitia dirishani lilifutwa.

Le Prince alikuwa ana mpango wa kusafiri kwenda Marekani kuchukua hati miliki ya ugunduzi wake, hivyo kutokana na kuwa alipotea bila kusajiri ugunduzi wake, Thomas Edison ndiye alichukua sifa ya kuwa mgunduzi wa picha zinazotembea (motion pictures).
Mpaka leo haijulikani nini kilimkuta Le Prince.

5284136174650339c466a312ac4ff938.jpg


4. Tarehe 10, mwezi wa 12 mwaka 1999, saa kumi kamili usiku, aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha California, Los Angels (UCLA) aliyejulikana kama Michael Negrete alizima laptop yake baada ya kuitumia kucheza michezo ya kompyuta na marafiki zake usiku kucha.

Saa tatu asubuhi, rafiki zake aliokuwa anaishi nao chumbani walipoamka walishangaa Michael hayumo chumbani ila wallet, funguo kadi zake za benki na vutambulisho pamoja na viatu vilikuwa humo humo chumbani.

Uchunguzi wa polisi kwa kutumia mbwa maalumu wa kunusa harufu, waliwaongoza polisi mpaka kwenye kituo cha basi. Lakini swali likawa je inawezekanaje Michael aache vitu vyake na atembee miguu peku mpaka kwenye kituo cha basi apande basi?

Zaidi ya kuwepo fununu kwamba kuna mwanaume asiyejulikana alionekana kwenye ukumbi ujulikanao kama Dykstra hapo chuoni mida ya saa kumi na dakika 45 usiku, hakukuwa na ushahidi au kitu cha ziada cha kusaidia upelelezi.
Mpaka leo kupotea kwake kumebaki utata mtupu.

48de603901413ed98e3804e6f2078c5d.jpg


5. Barbara Bolick, tarehe 18 mwezi wa 7 mwaka 2007, mwanamama aliyekuwa na umri wa miaka 55, aliyekuwa akiishi Corvallis, Montana alienda tembea kwenye milima ya Bitteroot akiwa na rafiki yake ajulikanaye Jima Ramaker. Jim alikuwa ametoka California kuja kumtembelea Barbara.

Walikuwa wanaelekea sehemu ya milima ijulikanayo kama Bear Creek Overview, Jim alikuwa katangulia huku Barbara akiwa nyuma yake wamezidiana umbali wa kati ya futi 6-9.

Jim anadai alisimama kutazama kitu flani na alipogeuka upande alipokuwa Barbara, alishangaa kutomuona.

Polisi walifanya msako wa kumtafuta lakini hakukuwa na dalili yoyote ya uwepo wake. Stori ya Jim inashangaza na ni ya kutilia shaka ila polisi hawamchukulii kama mtuhumiwa kwakuwa alionyesha ushirikiano na wanadai mtu ambaye angekuwa kahusika angekuja na stori nzuri ya kushawishi kuliko hiyo maana angejua ingetiliwa shaka.
Mpaka sasa Barbara hajulikana alipoteaje na kama bado yuko hai.

969e4d39ec24b5d1eb59cdfaae869611.jpg


6. Brian Shaffer, huyu alikuwa na umri wa miaka 27, tarehe 1, mwezi wa 4, mwaka 2006 alipopotea.

Brian alikuwa mwanafunzi wa fani ya Uuguzi katika chuo Kikuu cha jimbo la Ohio.
Siku hiyo alionekana katika bar ijulikanayo kama Ugly Tuna akiwa anabugia pombe kali na kalewa sana. Inasemekana alimpigia mpenzi wake kwa simu yake ya mkononi wakazungumza na baada ya hapo watu wanakumbuka kumwona mara ya mwisho akiwa anazungumza na akina dada wawili na baada ya hapo hakuna aliye muona tena.

Jambo la kushangaza ni kwamba kamera za ulinzi zilizo kwenye bar hiyo kwenye mlango wa kuingilia na kutoka zinamuonyesha Brian akiingia bar lakini hazimuonyeshi akitoka, hivyo kama alitekwa swali ni je huyo mtekaji aliwezaji kumtoa kwenye bar bila kuonekana kwenye kamera au watu kumuona?

Mpaka sasa si ndugu wala marafiki wanaoamini kwamba Brian aliamua kuondoka tu japo inadaiwa kwamba alikuwa na msongo wa mawazo baada ya mama yake kufariki wiki mbili nyuma kabla ya kupotea kwake, ila alikuwa anaendelea vizuri baada ya kuwa anafanya vizuri chuoni na walikuwa wamepanga kwenda likizo ya matembezi yeye na mpenzi wake.

f3aa7bdabd54b0292714dc539bf8816d.jpg


7. Ben Saanane. Huyu alikuwa Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti Baraza la Vijana Chadema. Inasemekana alipotea tarehe 14, mwezi wa 11 mwaka 2016 siku ambayo ni mara yake ya mwisho kuonekana katika ofisi za CHADEMA, zilizoko mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam na hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kuonekana wala kuongea na mtu yoyote.

Mazingira ya kupotea kwake yamebaki kuwa utata japo kuna maneno mengi yanaongelewa wengine wakidai kuwa katekwa na vyombo vya serikali, wengine wakidai kaamua kujipoteza mwenyewe na wengine wakisema chama chake kinahusika lakini mpaka sasa bado ni utata.

Mpaka leo yapata mwaka mmoja, polisi hawajaweza kutoa ripoti ya kueleweka juu ya alipo Ben. Ben alikuwa msaidizi wa karibu wa Mwenyekiti wa Chadema Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Siku alipotoweka vikao vya bunge vilikuwa vikiendelea Dodoma na ni siku hiyo hiyo ambayo kifo cha aliyewahi kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Samuel Sitta kilitangazwa.

Wakati hayo yakiendelea Ben hakuwa dodoma ila aliwasiliana na Mheshimiwa Mbowe kwa kumtumia sms kumpa pole kwa msiba wa Marehemu Sitta, na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho ya Ben kuwasiliana na bosi wake.

Kwa wanachadema Ben walimuona mara ya mwisho tarehe 14, November, ila kwa majirani zake alionekana mpaka tarehe 15, nyumbani kwake Mabibo jijini Dar ws Salaam.
Taarifa ya ufuatiliaji wa simu yake inaonyesha Ben alitoka nyumbani kwake Mabibo na kuelekea au kupelekwa Mikocheni ambapo alikaa kwa muda mrefu na baada ya kukaa Mikocheni kwa masaa mengi alirudi au kurudishwa Mabibo jioni.

Swali la alikuwa akifanya nini na alikuwa na nani ni swali ambalo mpaka sasa halijajibika.
Simu yake pia inaonyesha siku hiyo hiyo jioni ilitumika kutoa mpesa kiasi cha Tshs 50,000 kwa wakala aliyeko Mburahati, na muamala huu ndiyo ulikuwa wa mwisho maana baada ya hapo simu yake ikapotea kabisa ikaondolewa hewani.

John Mrema ambaye ni mkurugenzi uenezi na mambo ya nje CHADEMA, anadai walijaribu kufuatilia zaidi namba yake lakini inaoneka imefungwa, hivyo alidai ya kwamba mtu anayeweza kufanya hivyo siyo mtu wa kawaida. Aliongeza kuwa walikuwa wakitumia njia mbalimbali kumtrace sasa hawawezi tena.

Aliongeza kwamba ukweli ni kwamba ukiingiza namba ya Ben kwenye mfumo ili kuitrace mfumo unadai password, wakati namba nyingine zote hazihitaji password ili kuzitrace hivyo inaelekea kuna mtu mmoja tu mwenye hiyo password na kwanini namba ya Ben tu ndiyo waiwekee password isiwe traced.

Wakati viongozi wa chadema na ndugu wakiwa wanazidi kuhangaika kumtafuta, siku moja kabla ya sikukuu ya Christmas yani tarehe 24, mwezi wa 12 mwaka 2016, makala zake zote za kuikosoa serikali au ambazo zilionekana ziko dhidi ya serikali katika mtandao wa kijamii wa facebook ziliondolewa.

Mrema anajiuliza huyu mtu ambaye alikuwa na nywila ya kumwezesha kuingia kwenye ukurasa wa Ben na kufuta baadhi ya vitu ni nani?

Ama alikuwa Ben mwenyewe au mtu aliyekuwa na nywila yake, na kama alikuwa na nywila ya Ben je aliipataje? Ben alimpatia kwa uamuzi wake mwenyewe au kwa kuteswa?
Siku alipoonekana ofisini aliwaaga wenzake kuwa alikuwa ana safari ya kuelekea Afrika ya kusini ambako anakwenda kutetea tasnifu yake ya shahada ya Uzamivu (PhD) aliyokuwa akisoma.

Hivyo iliposikika Ben haonekani wengine walidhani atakuwa kasafiri kama alivyowambia.
Baba yake Ben Mzee Saanane anadai yeye aliongea na Ben kwa mara ya mwisho tarehe 11, mwezi wa 11 mwaka 2016 siku tatu kabla ya kupotea kwake.

Leo yapata mwaka hajulikani alipo huyu kijana mwenzetu na Mtanzania mwenzetu. Hakuna aliyetoa ripoti ya kueleweka na siku baada ya siku kesi yake inazidi kupoa atapita ashaulike kama wengine walivyosahaulika.

Naye nimemweka kama mtu aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha.

dccc1160011c7f2e34ce1a8f47ee71af.jpg


(Details za Ben nimeziandika kwa Msaada wa Mwananchi online katika mahojiano waliyofanya na John Mrema)
Duh
 
Kupotea kwa Maura Murray kuna conspiracy theories nyingi sana. Lakini yule askari wa kwanza kufika kwenye crash site anaweza kujua zaidi. Sijui kwanini polisi hawakuzingatia ushahidi wa "shahidi namba moja" .
 
Nilidhani wewe ni Lumumba buku 7 umeamzisha uzi huu ili tuone Ben kapotea kama walivyopotea wengine tu na ya kwamba sirikali haihusiki.
Kumbe umeandika vizuri.
Hongera na asante kwa uzi mzuri.
 
Back
Top Bottom