Watu na serekali

yap ni kweli nakubariana na hii habari picha! wafanyakazi wana-toil a lot, mwisho wa mwezi mishahara yao inakatwa kodi (P.A.Y.E.) kubwa kinomaa! pesa yao inachukuliwa na gvt! goma uone mabomu ya machozi hata kama unatetea ukweli!
 
Kweli serikali ina kamba ndefu (au mkono mrefu????) na ndoano kubwa!
 
Hii ni serekali isiyo na aibu hata chembe, huyu aliyeshikilia ndoano kama vile namjua.
Amepewa u..............
 
Mkuu unataka Serikali ikale wapi? Inabidi iwe hivyo ili barabara zijengwe, hospitali zifanye kazi, huduma za jamii ziwepo nk.
 
hii itakuja kutokea kwenye serikali ya CHADEMA kama ikingia madarakani !
 
Tu hodari wakubwa wa kulalamika, lakini inapofikia kipindi cha kufanya mabadiliko sijui tunakuwa usingizini? nakumbuka "wafanyakazi tuliambiwa na JK sihitaji kura zenu" tulifanya maamuzi gani kwenye chumba cha kupigia kura??
 
Hakuna anayekataa serikali isikusanye kodi tatizo mishahara tunayolipwa hailingani/haizingatii ukuji wa gharama za maisha na bado kodi tunayokatwa hapo ni kubwa. Tuna rasilimali nyingi sana katika nchi yetu ambazo zingetumiwa vizuri zingeongeza pato la taifa na mzigo wa kodi kwa mwananchi wa kawaida ungepungua. Matokeo yake rasilimali hizi ziko kwa ajili ya kuwanufaisha watu wachache.

Kinachoumiza zaidi ni hizo kodi tunazotowa kwa kiasi kikubwa hazina udhibiti unaofaa kiasi kwamba zinaishia mikononi mwa wachache na siye walala hoi tunaishia kukosa hata asprin tunapokwenda mahospitalini.

TAFAKARI.... CHUKUA HATUA.. fragan11
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…