Nilitangulia kusema kuwa Mkandara kaleta maada hii lakini watu wapo tayari kukubali ukweli?
Nlijuwa majina haya yatakuja tu na aliyeyapoteza au kusabibisha yapotee anajuulikana. Hawa ndo walikuwa wenye mji i.e wazee wa Mujini wakati huo. Mwalimu akaja kuwaita "...Mamwinyi tu hawa....waswahili tu hawa....n.k..." akawatupilia mbali baada ya kwisha tumia makasha yao.
ukweli unauma lakini huwezi kuzungumzia historia ya nchi yetu bila kumtaja Sheikh
Suleiman Takadir then kulikuwa na akina
Mzee Fundi Muhindi mwanasiasa mkongwe, muasisi wa African Association Tabora, kulikuwa na
Idd Faiz Mafongothen kulikuwa na
Ali Mwinyi Tambwe (sina hakika kama ana uhusiano wowote na balozi Tambwe bba yake abdurabi lakini
FMESanaweza kuniweka sawa)....leo hii watu wanashangaa ilikuwaje wamanyanyema waliikamata Kariakoo lakini ukweli ni kuwa huwezi kuzngumzia hilo bila kujua chombo kilichokuwa kinaitwa
BATETERA UNION (Congo Association) chama kilichokuwa kikiwaunganisha Wamanyema wa Tanganyika na
Mzee bin Sudi ndie inasemekana alikuwa muasisi wa chama hiki unless Mkandara aje kunikosoa lakini ukweli ni kuwa Batetera Union kilikuwa chama kilichoshikamana na chenye nguvu sana miongoni mwa vyama vya kikabila. Wamanyema ni kabila la Waislam watupu na kwa sababu hii hakukuwa na pingamizi katika kuunga mkono TANU enzi hizo
mnataka zaidi? hamuwezi kupata zaidi kwa kukaaa kwenye computer zenu na kwenye mapango mkienda Dar..mambo haya adimu lazima upite pale nje ya msikiti wa MANYEMA jioni baada ya swala ya ALAASIRI ndio utakjua kama historia toka kwa wazee wetu pale
watoto wa KARIAKOO wanajua historia hii na angekuwepo MSWAHILI angekuwa anawapa viapnde adimu kabisa
anyway kwa kuendelea ni kuwa
BATETERA UNIONBatetera Union ilikuwa na nguvu sana kiuchumi kwa kuwa kilikuwa katika wafuasi wake, watu waliomiliki majumba na walihodhi takriban nusu ya nyumba zilizojengwa mjini Dar es Salaam kati ya vita kuu mbili za dunia...(sitozungumzia WARAMO tulivyongizwa mjini na wanawake wa kimanyema) hapa lakini nayo inahitaji muda kuizungumzia
Anyway, Uuwezo huu wa kiuchumu uliwafanya Wamanyema kuwa wapinzani wagumu wa serikali ya kikoloni na uliwanyanyua hadi kufikia kuwa mbele katika siasa mjini Dar es Salaam na katika miji mingine ya Tanganyika ya enzi hizoooooooooooo. Kwa msiojua tuu ni kuwa Umoja wa Wamanyema ndiyo uliojenga msikiti maarufu wa Wamanyema mwaka 1912 uliokuwa karibu na makao makuu ya African Association...msio jua msikiti huu uko wapi basi si kazi sana upo pale karibu na Lumumba CC lakini kwa nyuma kidogo...
Zaidi ya kuwa na wanawake wazuri , ukweli ni kuwa wamanyema wanajulikana kama watu wenye damu ya kali na wana sifa ya ushujaa....unaambiwa Mmanyema anaweza kuulipia fedha ugomvi ili na yeye awemo, na kadri mpinzani anavyokuwa na nguvu na hodari, ndivyo Mmanyema anavyofaidi ugomvi wake na unaambiwa katika siku hizo Wamanyema walikuwa wameshikwa katika magomvi.
nimetoka kidogo nje ya topiki lakini huwezi kutaja watu bila kutaja struggles za enzi hizo
Mambo adimu kama haya huwezi kupata mapaka ukae na kina mzee
KATUNGUNYA ndio mntajua