Watu milioni 89.3 wamekimbia makazi yao Duniani, kwa mujibu wa UNHCR

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) za mwaka 2021 ambazo pia zinatumuka mpaka sasa zinaonesha kuna idadi ya watu milioni 89.3 ambao wamekimbia makazi yao, kati yao watu milioni 27.1 ni wakimbizi, pia nusu ya hao Wakimbizi wana umri chini ya miaka 18.

Watu milioni 4.3 hawana utaifa wa nchi yoyote na hivyo kukosa haki ya mahitaji ya msingi kama elimu, afya, ajira na uhuru wa kusafiri.

Nchi zilizohifadhi wakimbizi wengi zaidi ni Uturuki (milioni 3.8), Colombia (milioni 1.8), Uganda (milioni 1.5), Pakistan (milioni 1.5) na Ujerumani (milioni 1.3).


Source: UNHCR
 
Back
Top Bottom