Watu kutokujiandikisha kupiga kura wa kulaumiwa ni Serikali yenyewe

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Serikali isijifanye inaziba masikio juu ya kwanini watu hawajiandikishi kupiga kura sababu Ni hizi

1.Kauli za rais

Kauli alizotoa mh rais kwamba ole wake mkurugenzi atakaemtangaza mpinzani wakati anamlipa mshahara anampa gari na walinzi ole wake hii inawafanya watanzania waone hakuna umuhimu maana matokeo yatatangazwa kibabe hata Kama si chaguo lao.

2.Kuunga mkono juhudi

Haya yalikuwa Ni maigizo ya kimbumbumbu Sana yaliyochukiwa na watanzania na hakika hapa ndipo walipowadharau wanasiasa mtu anajiuliza niache kwenda shamba nikapange foleni kumchagua mtu ambae kesho atanisaliti kirahisirahisi kwasababu za kipumbavu za kuunga mkono juhudi za rais never.

3.Kuzuiwa mikutano halali ya kisiasa.

Kimsingi hili nalo limechangia Sana kwasababu Ni ukweli kabisa kwamba CCM haipendwi Tena Tanzania Sasa unapowazuia vyama vya upinzani wasikutane na watu wao unapunguza uzito unaoshamirisha siasa nchini watu wanataka kuwaona kina

Halima mdee
Tundu lisu
Freeman mbowe
Mch msigwa
Godbless lema
Joseph Mbilinyi
John mnyika
Joseph selasini
Ester matiko
Nk
Sasa unapowanyima Hawa watu freedom ya kwenda popote kufanya siasa kimsingi unauhujumu upinzani na siasa Safi za taifa unazihujumu
Kwa manufaa ya CCM ambayo watu hawaioni Tena Ni mkombozi ila Ni kikundi Cha madikteta.

4. Fujo

Siasa za Tanzania toka serikali ya awamu ya tano ishike madaraka zimenasibishwa na fujo na uvunjifu wa amani matukio ya kuuwawa wapinzani kama jaribio la kumuua tundu lisu na mauwaji ya akwilin akwilina yamewafanya watanzania kutokujiona salama Tena katika Mambo ya siasa.kiufupi watanzania wamegawanyika katika makundi mawili A. Wanaoipenda ccm wanajiona wako salama na wanalindwa na dola B.Wanaoipinga CCM wanajiona hawako salama na Ni victims wa uhalifu unaofanywa na dola. Taifa limegawanyika huo ndio ukweli.

5. Hofu

Kwasasa wananchi wamejawa na hofu kujihusisha na Mambo ya siasa hata Kama Yana tija kwao sababu ya hofu hiyo Ni hiyo namba nne hapo juu. (Fujo na vurugu) watanzania wamekata tamaa na siasa zao zilizonawiri enzi za JK wakibishana kwa hoja taifa lilichangamka punde nchi ikaingia gizani awamu ya tano.

Mwisho

Wanufaika wakubwa wa Hali hii Ni CCM watanzania wasidhani kususa kwao wanaikomoa CCM hapana CCM inafurahia hii Hali ya political Injustice wananufaika nayo // ngoja tuone mwisho wa haya yote Mungu ibariki Tanzania!!
 
Mods naomba msiunganishe huu uzi una maudhui yanayojitegemea Sana please nawaomba Sana.
 
Leo anawatisha ma rc na ma dc wakati yeye ndio kiini Cha tatizo kweli viongozi chini ya awamu hii wanatabu Sana maana hawajui kwa usahihi kipiki wakifanya kwa matakwa ya Sheria Ni kosa na kipi wakifanya against Sheria sio kosa yani Ni full kuyumba na kuyumbishwa
 
Wananchi hatupigi kura,. CCM jipigieni kura wenyewe
Nadhani maeneo mengi wanasema hivi Kama bujibuji alivyoandika hapa maana wananchi wanaona Kama ni kupotezeana muda ccm wanatumia polisi kutangaza matokeo hata ya uongo Sasa kwanini watujumuishe kwenye dhambi yao?
 
Back
Top Bottom