Watu hufa

Kila nafsi itaonja umauti....radha ya umauti ni ya kila nafsi
 
Mkuu yaani watu wanakufa balaa.. wale wote niliokua nawa consider km bibi/babu kule kijijini wakati nasoma primary & secondary washakufaga wote wakati huo mm hapa cjafikisha hata miaka arobaini... Huwa nashangaa sana
 
Basi sawa labda nimechanganya mafile kuna sehemu kuna deni la marehemu..

Nakemea mikosi kwa jina la Yesu..

 
Nampigia jamaa yangu tunaongea naye kila siku, anaumwa, tokea jana hapokei simu nipo njia panda
 
Hakika, watu hufa. Hata hivyo jf tunajitahidi kidogo, hatufi sana. ID nyingi bado zinasongesha, tushukuru kwa hilo.
 
Kuna mdada tulisoma nae, tulifahamiana Ila hatukua karibu kivile.
Siku hiyo naona amenitext messenger ananisalimia Kisha akaniambia amenimiss sana alikua anaikubali personality yangu, nikashangaa kidogo kwa sababu yeye kitabia alikua ni introvet kwa hiyo sikuwahi waza kama angekua anatazama watu wengine wapoje.

Basi tukachat kidogo kisha tukabadilishana namba za simu, akanipigia tukazungumza habari ya maisha nikamwambia Mimi bado ramani hazisomi mjini.
Akashangaa na kujilaumu Kwa Nini alichelewa kunitafuta, akaniambia kwenye kampuni Yao (miongoni mwa kampuni kubwa zaidi za kutoa huduma na uzalishaji nchini) nafasi zinatokeaga Ila hazitangazwagi nje na kwakuwa yeye alishakua na wadhifa tayari basi niandae CV yangu nimtumie atashughulikia.

Kesho yake akanipigia tena kunikumbusha sasa kulikua na ishu imenikamata kwa wakati huo nikawa naona aibu kumsalimia hivi hivi bila kukamilisha alivyoniambia nimuandalie.

Zikapita wiki mbili, nikawa nimekamilisha nikamtumia, hajajibu.. nikarudi messenger msg hajibu, najaribu kupiga simu haipatikani nikahisi labda amesafiri nje ya nchi, whatApp msg zimeenda Ila hazisomwi, nikahisi amenifanyia kusudi kwa nini anidanganye, nikakasirika sana nikaanza kukumbuka jinsi watu walivyokua wanamsema anaringa (kisa hajichanganyi) nikaona sasa ndio ananionyesha maringo yenyewe basi siku nikawa namuhadithia rafiki yangu yaliyonikuta akasema doh, kumbe hukusikia... Mbona huyu mtu ameshazikwa wiki ya pili Sasa... Mmhh.. yaani siku tuliyoongea Mara ya mwisho au kesho take yaani maumivu niliyosikia kama nimepoteza ndugu yangu wa damu.Hadi leo hii nikimkubuka namuombea tuu, nawaza tuu kilimsukuma nini from no where akanitafuta na kuanza kuniongelesha hali ya kuwa yupo safarini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…