Watu 50 Mbaroni wakituhumiwa kuchoma Msitu wa hifadhi, kufanya vurugu

Watu 50 Mbaroni wakituhumiwa kuchoma Msitu wa hifadhi, kufanya vurugu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Watu 50 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kuchoma hifadhi ya msitu na kufanya vurugu.

Katika taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Agosti 15, 2025 na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Adam Maro imeeleza watu hao wanadaiwa kuwashambulia maofisa misitu wanne, kuharibu mali mbalimbali za ofisi ikiwemo kuchomamoto pikipiki moja miche ya miti 50,000 iliyokuwa kwenye vitalu na miti 236,643 iliyokuwa imepandwa.

Awali, juzi inadaiwa wananchi wa Kijiji cha Lwamgasa, Kata ya Lwamgasa wilayani Geita waliandamana na kuchoma moto eneo lenye ukubwa wa hekta 213 na kuwajeruhi maofisa wanne wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa kile kinachodaiwa ni kupinga unyanyasaji na matukio ya ukatili wanayofanyiwa na maofisa hao

Pia, wananchi hao wanadaiwa kuchoma moto eneo pia wananchi kuharibu miti 236,643 iliyokuwa imepandwa pamoja na kuharibi vitalu vya miti 50,000 na kubomoa majengo ya ofisi zilizopo eneo la hifadhi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa TFS Kanda ya Ziwa, Ibrantino Mgiye, amesema wananchi hao walivunja milango, kuondoa madirisha na kuondoka nayo na kuvunja baadhi ya kuta za jengo jambo ambalo ni la kihalifu


Chanzo: Mwananchi_official

 
Hawa waandishi wa habari ni vilaza. Maelezo yote haya wameshindwa kutaja jina la msitu.
 
Nyie waandishi mnapaswa mkasome tena uandishi, sasa ndio umeandika nn, paragraph zote hizo zinarudia kitu kilele.. nini maana ya kutoa habari sasa??
 
Hii mliiona??


TFS nchi hii ni majambazi kabisa
tapatalk_jpeg_1755199088065.jpg
 
Population ya hiyo kata ni kubwa sana,kata inawakaazi 72000 na eneo ka km za mraba 149,hivyo wengi wanajikuta wanaingia porini kulima.
 
Back
Top Bottom