Watu 3 wajitokeza kumpinga Beyonce

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
160208122917_beyonce_mano_624x415_tinaknowles.instagram_nocredit.jpg


Image copyright Tina Knowles. Instagram Image caption

Beyonce na wacheza densi wake waliovalia kama wanachama wa Black Panther
Waandamanaji watatu walijitokeza katika mkutano wa kumpinga nyota wa muziki Beyonce nje ya uwanja wa soka ya Marekani mjini New York.

Maandamano hayo yaliitishwa baada ya onyesho la msanii huyo wakati wa mapumziko ya mechi katika uwanja huo ambapo yeye na wacheza densi wake walivalia kama wanachama wa kundi la itikadi kali la Black Panthers.

Watu wengi nchini Marekani walisema kuwa onyesho hilo lilikuwa pigo kwa maafisa wa polisi pamoja na wale wanaoshinikiza sheria kufuatwa.

Lakini kulikuwa na waandamanaji wengi wa kumuunga mkono Beyonce katika maandamano hayo.

160217135450_beyonce_black_panther_512x288_bbc_nocredit.jpg

Image caption Wacheza densi wa Beyonce

Onyesho hilo la Beyonce mapema mwezi huu lilishirikishi wacheza densi waliovalia kama wanachama wa kundi la Black Panther.

Kundi hilo lilikuwa la wapiganaji wa haki za weusi nchini Marekani kati ya mwaka 1960 na 1980.

Wakati mmoja kundi hilo la Beyonce lilitengeza umbo la X,ambalo wengi wanafikiri lilikuwa la kumuenzi mwanaharakati wa haki za kijamii nchini Marekani Malcom X ambaye alipigwa risasi mwaka 1965.
 
Hivi kwa nini hii kitu isichukuliwe na watu wote weusi duniani???
Kwamba itengwe siku moja ya kuwaunga mkono Black Panther???
Then siku hiyo kila mweusi atupie picha yenye maudhui ya kujivunia weusi???
 
Black Panthers ndio vugu vugu pekee LA kutetea Hadji ya watu weusi. Na Malcolm X ndio mwanaharaki pekee aliyejipambanua zaidi kutetea haki za watu wausi, ndio maana wazungu hawampendi ukilinganisha na Luther.
 
Talking abt the show ilikua 1of the best show Ever. Beyonce Bruno Mars waliua. Even Coldplay


Na message ilikua delivery kwa maana Police bdo wanaendeleza uonevu kwa Black Americans kitu ambacho ni ujing kwa dunia ya sasa. Sote tu sawa.
BigUp to Queen Be
 
Back
Top Bottom