Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Polisi katika mji wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 19 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa kwenye mulipuko uliotokea ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.

Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.

Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake, wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima.

Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.

Eneo kulikotokea mulipuko huo limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.

Ripoti ambazo hazijathitishwa kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao hawakutajawa zinasema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Ukumbi wa Manchester ambao ulikuwa ukifahamika awali kama ukumbi wa wanaume, ndio ukumbua mkubwa zaidi mjini humo wenye uwezo wa kuwachukua watu 18,000

Barabara ya ukumbi huo unuangana na kituoacha treni cha Victoria kati kati mwa mji.

Ukumbi huo hutumiwa kuandaa tamasha za manyota wakuu kama Ariana Grande nyota wa runinga mwenye umri wa miaka 23 ambaye sasa ni nyota wa muziki wa pop.
 
mlipuko wa bomu watokea katika ukumbi wa muziki mjini manchester n Kujerui watu 50 huku 19 wakifariki

mlipuko ulitokea wakati msanii kutoka marekani alean grand akimalizia kutumbuiza

26d7f78cf8aea527960fad172c7880cc.jpg
poliai.wamesema misumali miingi ilitapakaa chini baada ya tukio hilo huku wasababishaji wakiwa hawajapatikana bado
30bb3f02583ee3cf604dda9d77086a24.jpg
polisi wamesema.kma tukio hilo ni la kugaidi basi ni tukio kubwa kutokea uingereza tangi 2005
 
Watu wamechoshwa na dhuluma za mataifa haya ya magharibi

Leo Africa na middle east kuna unrest kwa ajili wanafanya hivyo kupora rasilimali

Matokeo yake ni hivi vifo vinavyotokana na chuki
Siyo dhulma za magharibi bali ni matatizo ya waarabu wenyewe.Kwani walioandamana Libya kumng'oa Gadafi walikuwa ni watu wa magharibi?

Hao ni wale wakimbizi wanaopewa hifadhi then wanataka kuchafua nchi za watu kama walivyochafua za kwao.
 
Siyo dhulma za magharibi bali ni matatizo ya waarabu wenyewe.Kwani walioandamana Libya kumng'oa Gadafi walikuwa ni watu wa magharibi?

Hao ni wale wakimbizi wanaopewa hifadhi then wanataka kuchafua nchi za watu kama walivyochafua za kwao.
Kwani wewe hujui kuwa mzungu alikuwa anahitaji rasilimali za Libya? Ina maana hujui kuwa waliohusika na kifo cha gadafi ni USA? Kama hujui basi panua mind yako ujitAmbue
 
Watu wamechoshwa na dhuluma za mataifa haya ya magharibi

Leo Africa na middle east kuna unrest kwa ajili wanafanya hivyo kupora rasilimali

Matokeo yake ni hivi vifo vinavyotokana na chuki
yaani uchoshwe na nchi za Magharibi ukaue watu wasio na hatia!? Hao raia wana kosa gani na umejuaje Kama wote ni raia wa nchi za magharibi? Acha kabisa kushangilia ugaidi
 
Back
Top Bottom