BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,800
UGONJWA wa Kipindupindu umetajwa kuibuka katika Kata ya Kagongwa, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga huku ikielezwa kuwa watu watano wametajwa kufariki dunia na wengine watano kuthibitika kuwa na maradhi hayo.
Wakati hali ikiwa hivyo, wakazi 452 wa eneo hilo wamewekwa chini ya uangalizi wa kitabibu (karantini) katika vituo vya afya maalum vilivyoandaliwa kwa ajili ya kushughulikia wagonjwa hao vya Mwendakulima na Kagongwa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, alithibitisha kuwapo kwa mlipuko wa ugonjwa huo jana wakati akizungumza na vyombo vya Habari. Alisema ugonjwa huo ulianza Desemba 25, mwaka jana, baada ya mtu mmoja kufariki dunia na dalili kuonyesha kuwa chanzo ni ugonjwa huo.
Alisema alipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kagongwa kuwapo kwa vifo vya watu watano vilivyoambatana na dalili za kipindupindu ambazo ni kuharisha na kutapika, hivyo kulazimika kutuma timu ya wataalamu kwenda kujua tatizo ni nini.