M.E.M.A
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 1,373
- 472
Wadau. Hivi mnapokuwa mmeshaoana, ni nani anayetakiwa apange kwamba 'huu ni wakati wa kupata mtoto'? Ni mume, ni mke, baba/mama mkwe au ni ile ghafla tu kitoto kinatokea!?
Kuna rafiki yangu ametengana na mke wake kwa sababu ya mtoto, kwamba jamaa hakuwa anataka mtoto mapema. Na isitoshe walikuwa hawakai pamoja kwa sababu ya kazi. Jamaa yupo Iringa mke Dar.
Wakati wa usulihishi wa swala lao, jamaa akasema "mke wangu unajua kabisa nilikuambia tusizae mapema, sasa imekuwaje?" Alichojibu mke ndio kilichonifanya niulize mauzoefu hapa. Alijibu "wewe unadhani tulioana ili tupike makande?". Hapo jazba zikaanza kikao kikavunjika, na hadi leo wametengana.