Watoto watatu wa J.Baptist wafa Maji!!

analysti

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
729
612
Ndugu wana JF, Jana nilipitia Mahaba Beach Club, maeneo ya boko ununio, baada ya uchovu wa kazi jioni. Nikakutana na balaa lililo nisikitisha sana. Watoto watatu wa shule ya wasichana ya sekondari ya John Baptist waliopolewa wakiwa wamekufa baada ya kuzama baharini wakiogelea, huku wengine wawili wakiwa taabani.

Nikaongea na mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa yupo pembeni akiwa na majonzi, alinieleza kuwa, mwalimu wao aliwapeleka ufukweni huko ili wakafanye mazoezi ya viungo kama darasa, sasa walipofika ufukweni hapo wakaendelea na mazoezi lakini baadhi yao wakaanza kuogelea na mwalimu hakuwazuia kufanya hivyo. Ndipo hao mabnti wakajikuta wanazama maji na kupoteza maisha. Nikamwambia anioneshe mwalimu lakini sikufanikiwa kumuona.

Tukio hili lilinisikitisha sana mimi kama mzazi, kwani watoto wanapelekwa shule na wazazi kwa imani kuwa waalimu watawasimamia na kuwaongoza dhidi ya hatar zote za maisha. Lakini uzembe uliofanywa na huyu mwalimu ulinisikitisha sana na kunivunja moyo, Nikifikiria wazazi wa wale watoto wanajua watoto wao wapo shule kumbe wameshafariki.

Mungu zilaze mahali pema peponi Roho za watoto hawa.

Amen!!
 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe... Poleni wafiwa.

Ila mkuu ulivyotaka kumwona mwalimu lengo lako hasa ilikuwa nini?

So that i could have enough and reliable informations to post on JF.
 
Mungu awalaze peponi jamani na pole sana kwa familia zao
 
Back
Top Bottom