Watoto watatu familia moja wafariki kwa moto

Watoto watatu familia moja wafariki kwa moto

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Watoto watatu wa familia moja wamekutwa wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wanaishi kuungua moto
Watoto hao Membe Ndama (7), Mwaru Ndama (2)na Sayi Ndama (1)walikuwa wakiishi na wazazi wao katika Kijiji cha Nambilanje, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Jumatano Julai 16, 2025 saa 11 jioni katika Kijiji cha Nambilanje

Kamanda Imori amefafanua kuwa baba na mama wa watoto hao walitoka kwenda kuchota maji na kuchimba viazi hivyo waliwaacha watoto hao nyumbani, ambapo Sayi alikuwa amelala na wenzake walikuwa wakicheza nje ya nyumba hiyo

"Hawa wazazi wa watoto waliofariki walikuwa wametoka na eneo walilokwenda lilikuwa siyo mbali na nyumbani. Baada ya muda kidogo waliona nyumba yao inaungua moto," amesema Kamanda Imori

Amesema nyumba ilikuwa imeezekwa nyasi jambo lililosababisha kushika moto kwa haraka na kusababisha vifo vya watoto hao watatu

Kamanda Imori amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni moto uliokuwa kwenye jiko la mawe kushika nyasi za ukuta wa ndani na kusababisha nyumba kuungua

Miili ya marehemu hao imefanyiwa uchunguzi na Daktari Ezekia Ambekile wa Hosptali ya Wilaya ya Ruangwa na kubaini kuwa chanzo cha vifo ni kukosa hewa baada ya kuungua moto
"Nimepokea miili ya marehemu muda wa jioni (jana) na kuifanyia uchunguzi kisha kugundua kuwa vifo vyao vilisababishwa na kukosa hewa," amesema Daktari Ambekile.

Baba wa marehemu hao, Ndama Mashauri (33) amesema kuwa wakati wanachota maji na mke wake Mindi Msasu (20) waliona moto unawaka nyumbani kwao na walipofika walikuta watoto wameshafariki

"Nilitoka mimi na mke wangu kwenda kuchota maji na kuchimba viazi eneo kama la kilometa 2, tuliwaacha watoto nyumbani mmoja amelala na wawili walikuwa wanacheza, baadaye nikaona nyumba inaungua tulipofika karibu tuliwakuta watoto wetu wote watatu wamefariki dunia," amesema Mashauri

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuepuka tabia ya kuwaacha watoto peke yao bila uangalizi

1752732558014.png


Chanzo: Mwananchi_official
 
Tokea nijiunge jamii forum, hii ndo taarifa iliyonihuzunisha sana tena sana...

Lakini kilichonichekesha ni kuwa polisi hawajawahi kukosa comment au ushauri
 
Polisi wamewataka wananchi waache tabia ya kuwaacha watoto bila uangalizi, hivi hawa Polisi hawajui kuwa umasikini ndiyo chanzo kikuu cha haya yote?
 
Mtoto wa kwanza ana miaka 7, mama ana umri wa miaka 20 tiyari ana watoto watatu na sio mapacha.

Watoto wapumzike kwa amani.
 
Polisi wamewataka wananchi waache tabia ya kuwaacha watoto bila uangalizi, hivi hawa Polisi hawajui kuwa umasikini ndiyo chanzo kikuu cha haya yote?
Umaskini sio kigezo cha kuwa mvivu kusimamia, kulea, kutunza watoto.

Kama unajua ni maskini hutopata muda wa kujali watoto funga zipu mpaka pale utakapokuwa tiyari. Unataka nani aangalie wanao hata kama wewe maskini?
 
Poleni sana kupoteza watoto wote watatu ni huzuni kwa kweli
 
Umaskini sio kigezo cha kuwa mvivu kusimamia, kulea, kutunza watoto.

Kama unajua ni maskini hutopata muda wa kujali watoto funga zipu mpaka pale utakapokuwa tiyari. Unataka nani aangalie wanao hata kama wewe maskini?
Kijijini moto wa leo hautazimwa wanaweka majivu juu na kesho utawashwa tena bila kutumia kiberiti ndio chanzo cha kuunguza nyumba hiki..
 
Back
Top Bottom