Nakasirishwa sana na hawa watoto, wa kwanza yupo form five, wa pili form two na watatu standard seven english medium. Yaani najitahidi sana kuwalipia ada na kweli naweza na nafrahi sababu ni vipanga kila nikangalia matokeo nafurahi sana.
Huyu wa form 5 ni dada ndie anaeongoza chati yani kila siku sababu zisizoisha wa pili ni dume yeye hanaga mambo mengi anataka pesa za kucheza games na mziki mkali akirudi, haka kadogo kakiume kanapenda hela za kula chipsi na mandazi, ni kweli walimu wameniambia kanajimwaga kweli.
Plz najitahidi wanangu wana malezi mema hawajawahi nikera ila wananipiga mzinga sana inafikia mahali nataman niwaambie live sipendi hio tabia ila nafsi inakuwa ngumu plz nipeni ushauri.