Watoto wanajua kile kilichobora

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
WATOTO WANAJUA KILE KILICHO BORA

Watoto wanajua sana, pengine vizuri zaidi kuliko hata wewe.Kuthibitisha hili muulize mtoto yeyote mwenye umri katia ya miaka mitano mpaka kumi swali hili; ukiwa mkubwa unataka kuwa nani?Niambie kama utasikia jibu kama hili;

Nikiwa mkubwa nataka niwe makamu wa raisi...
Nikiwa mkubwa nataka niwe napanga mafaili kwenye ofisi....
Nikiwa mkubwa nataka niwe naokota makopo...
Je umepeta jibu ambalo linaendana na hayo?

Jibu ni hapana, majibu utakayopata ni nataka niwe raisi, niwe rubani, niwe daktari, niwe mwalimu na mengine kama hayo.

Hivyo watoto wanajua, ya kwamba kwenye maisha unatakiwa kupata kile kilicho bora. Makamu wa raisi ni nafasi kubwa, lakini kuna bora zaidi, raisi, hivyo mtoto yeyote atataka kuwa raisi.

Sasa cha kushangaza hapa ni kwamba kwanini wewe umekataa kupigania kile ambacho unajua ni bora zaidi kwako? Kwanini umekubali kuridhika na pale ambapo ulipo sasa?

Na sio kwamba tunadharau baadhi ya kazi, ila kama kuna ambacho ni bora zaidi kwa pale ulipo, ni vyema kupenda kile kilicho bora zaidi.

Labda tuseme kwa uwezo wako na mazingira uliyonayo, kazi pekee unayoweza kufanya ni kuokota makopo. Vizuri sana, sasa anzia hapo lakini usiridhike na kubaki hapo. Anza kuokota huku ukiwa na malengo baada ya muda fulani utakuwa huokoti tena wewe, bali utanunua kwa wale wanaookota, na unaendelea kukuza hivyo mpaka siku moja na wewe unamiliki kiwanda chako cha kutengeneza makopo, hii ni bora zaidi.

Labda kwa sasa umeweza kupata kazi ya kupanga mafaili, au kufagia ofisi, vizuri sana, sasa anzia hapo kuifikia ile ndoto kubwa uliyokuwa nayo wakati ambapo ulikuwa na ubunifu mkubwa sana.

Watoto wanajua kilicho bora, lakini kadiri wanavyokwenda na kukua wanasahau na kuridhika na kile wanachopata, hii ni sumu kubwa sana kwa mafanikio makubwa. Usikubali kabisa kuizika ndoto yako kubwa.
 
Upo sahihi sna mkuu, hakupaswi kukata tama ni kupambana mpaka kufikia malengo yetu.
 
Unapokuwa mtoto unachukulia kila kitu ni rahisi... Unavyokuwa ndiyo unakuja kugundua kumbe zile ni ndoto tu, mimi kwangu huku...
 
Ndoto zingine sio halisi non feasible sio mradi una ndoto tu, utaishi maisha ya sanaa na ndoto zako.

Mimi nina ndoto ya kuwa rais wa marekani
Hahahahaaaaa
 
Back
Top Bottom