Watoto wa Viongozi CCM wanalazimishwa kwenye siasa! Hawana mapenzi

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Kumekuwa na utaratibu wa kuweka watoto wa viongizi kwenye nafasi mbambali za nyama. Ukweli ni kwa hawaonekani kama wanafurahia badi ni kama wamelazimishwa kwa kunufaisha na kufurahisha familia zao. Kuanzia Nape mpaka makamba na wengineo ni watu wakukosana kila siku kwasababu ukweli wa nafsi zao hauko CCM.
 
nakubaliana kabisa huyu Sioi anaonekana kabisa hata uwezo wake wa kushawishi kisiasa ni mdogo mno hamuwezi kabisa Nassari. Yaani hajui kupangilia hoja kuvutia watu kumsikiliza
 
Kama wao wenyewe hao watoto wa vigogo wanashindwa kuwa na uchambuzi yakinifu wa hali halisi ya dunia na hasa siasa zinavyokwenda, wao ndio wa kuwalaumu kwa umbumbumbu wao. Wanasahau kuwa wazee wao muda wao umeshapita na kizazi kinachoingia ktk siasa ni tofauti kabisa, ni jukumu lao kukataa na kuendelea na mambo yao. Kwa swala la Sioi, atakuja jutia uamuzi wake huu wa kukubali kuingia ktk siasa tena kwa makundi yanayosadikika ni machafu.
 
Kumekuwa na utaratibu wa kuweka watoto wa viongizi kwenye nafasi mbambali za nyama. Ukweli ni kwa hawaonekani kama wanafurahia badi ni kama wamelazimishwa kwa kunufaisha na kufurahisha familia zao. Kuanzia Nape mpaka makamba na wengineo ni watu wakukosana kila siku kwasababu ukweli wa nafsi zao hauko CCM.
ulichosema ni ukweli lakini natofautina kidogo nawe kwenye issue ya Nape kwani yeye ametoka darasani na kukimbilia siasa moja kwa moja kwahiyo hana life experience nikiwa na maana ya private sector. hawa wengine at least walijaribu wakafaulu na wengine wakafeli ingawa hata kwenye kufeli kuna mambo mengi unakuwa umeyajua kama reality ya maisha.
 
Mkuu siudhani kama wanalazimishwa isipokuwa huko ndiko kwenye Ulaji na wengi wao wanataka umaarufu kama wa wazazi wao. kati ya hawa vijana wote nadhani Makamba he is the best kwa sababu anajua kazi Ubunge ni nini? ana exposure na anaonyesha anaweza kuleta mabadiliko japokuwa sii ya kitikadi.

Tatizo la vijana hawa wote ni kwamba wameingia ktk makundi ya Mtandao, ina maana wanashinikizwa kufanya ama kuungana na makundi jambo ambalo linawapunguzia sana uwezo wao kufikiri ama kufanya maamuzi. Lakini ukweli utabakia kwamba - Hakuna ajira iliyo rahisi kwao kama kuingia serikalini kwa sababu ndio urithi uliopo - If he can do, I can do better!
 
Back
Top Bottom