Watoto wa kambo

Better kubaki neutral tu, kuishi kawaida kabisa make binadamu tuna maneno ukimfokea kwa nia nzuri tu utaambiwa "kwa kuwa sio wako" ukimjali sana " unajipendekeza ili mzazi wake akupende" mmh stay neutral hakunaga shukrani kwenye hilo ni mara chache sana mama wa kambo kuonekana ni mzuri.
 
Yaani kuwin love ya mtoto ambaye umemkuta kwa mwanaume akiwa mkubwa ni kazi sana ni vizuri mtoto akiwa mdogo utamlea kwenye misingi ya malezi yako ila mmh! ni kazi sana kwakweli

Ila hata kwa watoto wa kambo kuna hali ya kujishtukia sana katika maisha ya kuishi na mtu ambaye sio mzazi wako.
 


Ndio shida ya kuingia kwenye ndoa zilizoachwa na wengine tena kwa talaka na kukuta watoto ambao vichwani mwao wana mtazamo tofauti kuhusu kuachwa kwa mama yao; usitegemee watakupenda na kukusikiliza kirahisi..... kazi kwako kujua jinsi ya kugeuza mawazo yao na kukukubali. Ni ngumu kumshauri mtu jinsi ya kuwateka watoto hao na kuwageuza bila kujua tabia zao na zako kwani inawezekana nawe una mapungufu yako kwao.
 
kuna mdada anapata shida sana na watoto wa kambo yan wale watoto ni pasua kichwa hadi ndoa anaiona chung. kibaya ndugu wa mume wanamuona anawatesa yani hadi huruma. mi nilishajiapiaga siolwi na mume mwenye mtoto na ikitokea bdy kazaa nje huyo mtoto alelewe na mama ake. lawama zinakondesha jaman waweza kufa cku c zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…