Watoto wa kambo

ila mtu hukai nae inakuaje tena unataka kum discipline? why not muachie baba yake ya kum discipline' for now,wewe kuwa 'a good cop' muache baba awe 'the bad cop'
Hili ni wazo zuri, ngoja yangu yawe macho tu
 

jamani pole, manake umeongea kwa uchungu mpaka nimesikia huruma, ila ukisema umuachie tu afanye anachokita mfano hilo swala la kucheza ndani mpaka jikoni na kuna kitu hatarishi mfano hayo mafuta ya moto ikitokea akaungua lawama zitarudi kwako na utawapa reason za kuona kweli humpendi, me nazani huyo bado mtoto mwenye kuhitaji msaada wa kumjenga kimaisha na kitabia hapo mbaya ni mama yake, sasa cha msingi kwa kuwa hili swala limefika mpaka kwa ndugu wa mume na mume mwenyewe, wewe itisha kikao awepo huyo mama yake na mtoto, mumeo, na baadhi ya ndugu wa mumeo ili uongee haya unayotumbia sisi na mengineyo yote yanayokukosesha amani kuhusiana na mahusiano yako na huyo mtoto, nazani hapo pekee ndo kutapatikana suluhisho
 
Malezi ya watoto wa kambo yamekuwa tatizo, wahanga wakiwa hao mama wa kambo. Mara nyingi wao wanatupiwa lawama, hata wajitahidi vipi, nimekuhurumia sana 64Bits kwa shida inayokupata katik malezi ya mtoto wenu.

Ninaamini mengi anajifunza au kuambiwa na mama mzazi. Hali inaweza kubadilika mkianza kuishi pamoja, kwa sababu mama hatakuwepo kumpa ushauri m'baya.

Lakini pia, kwa sababu ulijua kuwa mumeo ana mtoto hata kabla ya kuamua kuishi nae, huna budi kumlea huyo mtoto kwa malezi bora, kama mtoto wa tumbo lako. Omba busara, mshirikishe mume wako katika malezi ya huyo mtoto, kwa sababu akiharibika kuna uwezekano hata wadogo zake wakafuata njia hiyo.

Mwisho, mapenzi hayachagui, unaweza ku-fall kwa yeyote, lakini mtu mwenye mtoto aoe/aolewe na mwenye mtoto...single parents waoane...hii itapunguza matatizo kama haya..
 
Last edited by a moderator:
Kwanza HONGERA kwa kuweza kukubali swala la kulea mtoto wa mtu, kulea mtoto wa mtu ni kazi sana...
kwa case kama yako hii tuanze na upande wa huyo mama mzazi,kwakuwa mtoto hujaanza kukaa nae yaani anaenda kwa mama yake na kuja tena kwako...inawezekana mtoto akawa ni mzuri tu,lakini anaact upuuzi kwa kujazwa ujinga na mamake, kumbuka hakuna anayefurahia kuachwa yeye na mwingine atake over...hapo nadhani mwenyewe unamjua huyo mamake vizuri..

Pia, je babake anafahamu hayo yote yanayotendeka..kama ni ndio, mara nyingi mapokeo ya matukio anahendo vipi?
watu tunakariri kwamba mama wa kambo ni vimeo sasa kwakuwa umesema wewe unatunza mtoto vizuri nadhani akija kukaa hapo jumla itakuwa ni vizuri zaidi kuonyesha wewe ni mlezi mwema....
Tandika viboko inapohitajika,cheka na mengineyo kwani ukisema umuache tu akikua vizuri huyo dogo utakiona cha moto..kunja angali mbichi....ila sio kupiga piga hovyo mtoto wa watu
 
Pole kwa yote unayokabiliana nayo, ingawa neno lenyewe 'mtoto wa kambo' ni mtihani, lakini ngoja nijaribu kutoa mchango wangu japo waweza kuwa haujanyooka sana. I have been through yote unayopitia na anayopitia huyo mtoto but amini you are in more better position to make things right kuliko huyo mtoto kama ifuatavyo;

1. 8 yrs old kid : Usisahau, uwe umemzaa ama hujamzaa, huyo ni mtoto tu ... hebu jaribu kuvuta pita kipindi ukiwa na umri huo, hali yako ilikuwaje. Jaribu kumchukulia kama mtoto kwa kumkanya kwa upendo na saa nyingine kumweleza ukweli i.e Madhara ya makosa anayoyafanya, kumbuka siku moja atakuwa mkubwa na atakukumbuka kwa yote ....

2. Jiamini, tenda haki and do it for you: Prove that you are not spoil na mob psychology na stigma dhidi ya watoto wanaokutwa kwenye mahusiano yenu(NDOA?!), very sory malalamiko siku zote huwa yanatokea kwa wakina mama na si wa baba wa kambo .. umewahi kujiuliza kwanini?!Fanya hivi, jiamini na tenda kama vile MUNGU anakuona, usimpendelee na kama kuna kazi za umri wake mpe, akifanya kosa mkanye kwa 'sauti' but sikushauri sana kuchapa coz that tend to bring more harm than good even kwa mtoto wakumzaa mwenyewe unless proven otherwise.

3. Re asess yourself : Ni muda mzuri sasa kujiuliza kama mama(wa NDOA), nini ufanye kuweka mambo sasa ... la kwanza umekuja kuomba ushauri hapa jamvini, ni sawa kabisa but now its your time kuchukua akili za mbayuwayu ukajumlisha na za zako kupata maamuzi sahihi ... usisahau na kumbuka, lolote utakaloamua na kulitenda litakuwa na malipo baadaye(when in need) either mazuri ama mabaya.

(Ni mtazamo binafsi)
 
Nashukuru mrsleo na wote mlochukua muda wenu kunishauri
 

Nashukuru sana kaka dah manake mawazo yalinizidi nikaona bora niulize tu angalau mmenifungua macho kwa response zenu
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu kwa mawazo yako na kuchukua muda wako kunishauri
 
Me nimeish na watoto 2 wa kambo kwakwel had nilinenepa hakuna aliejua kama wale watoto c wangu had leo wananipenda zaid ya sana
 
Mtoto sio mbaya bali anapata ubaya kutoka kwa mama ake. Kuna baadh ya akina mama wanatabia ya kuwafundisha mambo mabaya watoto zao ili wawafanyie mama zao wakambo hali wao wameachika.

mkuu w jukwaa la kule, hapa umenena.Mambo yooote yameanzia hapo ...........

Grand PA
 
Kuishi ba mtt ambae hujamzaa halaf akawa mkaidi ni mtihani sana jamani haya mambo myasikie tu kwa wengine
 

Point ! Binafsi ni Mtoto niliyelelewa na Mama wa Kambo , naye alinikuta wakati akiolewa na Baba yangu , Namshukuru Mungu sana Mama yangu alinitoa kwa upendo kwake na kuhakikisha anamahusiano mazuri sana na huyu Mama aliyenilea , kutoka Moyoni Yule Mama alinilea kama Mwanaye Mpaka ikafika kipindi ikija Likizo nikiambiwa niende kwa Mama yangu Mzazi nagoma , Yaani Mpaka Namaliza secondary ndio nikamgeukia Mama yangu , Ninachoweza kusema Mtoto wa Kambo Mbaya sana ukikuta Mama yake au ndugu wa Mama yake wanamjaza Maneno , na kama Mama yake bado alikuwa na Mpango na Baba yake , kwa maana Bado anavizia vizia , Ila kama Mama yake alishaendelea na Maisha yake huwezi kuta akakusumbua maana kama vipi si akakae na MAMA yake , Pole sana Nimeolewa na Mimi nikakutana na Mtoto wa Kambo miaka sita hivi , Nilikaa naye wiki tu Nikamwambia Mume wangu aniwie radhi naomba either aoe Mwanamke Mwingine kwa Upendo kabisaaa au Mtoto akakae na Mama yake , Finaly mtoto akarudishwa kwa Mama yake , tukawa shwariiii, Nikianza kukusimulia hivyo vitimbi Utazimia wewe , Nikashangaa sana Maana na Mimi ninaexperience na hata Mume wangu nilikuwa namsimulia Mama yangu wa kambo alivyonilea , So Binafsi nakuelewa sana Kuna Watoto wa Kambo Balaaaa
 
Mmh, mie nikilea watoto wa mtu nalea kama ninavyowalea wangu, utaratibu ni ule ule. Sasa kama inaonekana vibaya labda waondoke ninapoishi, siwezi mlea mtoto kama glass, akiharibika baadae huku najua, nitajuatia sana.

Afterall magomvi ya wazazi yasiharibu well being ya watoto.
 
Kim nana nilikuwa nikiyafanya haya na mengine ila saivi kwa kweli moyo wangu unakufa ganzi kila kukicha

usife ganzi wala usikate tamaa jaribu kuongea na baba yake na huyo mamake kama anatangaza unamtesa mtoto mpuuze asikufanye ushindwe kuishi kwa amani
 

Binafsi umenchanganya sana na aina ya kauli zako! Naangalia umri wa mtoto, nafananisha na tuhuma zako, nakosa pa kushika! Daah, sijui lkn mtoto wa miaka 8, tena wa kukutana nae w.end hadi w.end, daaah!
 
Kadiri mtoto wa kambo anavyokuwa ndio matatizo hayo yanavyokuwa...mi na miaka 21 now na mtoto wa kambo, amekuwa kama mume mwenzangu tukigombana na mamake wana side upande mmoja, vumilia tu dada ukipenda boga.

Hold on, hebu twende taratibu, wewe umri wako ni miaka 21 au tangu uolewe huu ni mwaka wa 21 na unaishi na mtoto wa kambo?
 
Jamani mtoto huyu amekuwa mtihani kwangu, hata nimfanyie nini mimi mbaya tu kwake, nampenda, namjali namfanyia wema wote ambao mtoto anatakiwa afanyiwe lakini shukrani yake ni kunizulia uwongo wa kila aina.

Umemshirikisha mumeo kwa hili?

Kama ndio, ni upi mtizamo wake?
 
kama unahisi utapata shida kumlea basi cha kufanya ni akija jaribuni kumpeleka boarding school awe anakuja likizo tu
 
Binafsi umenchanganya sana na aina ya kauli zako! Naangalia umri wa mtoto, nafananisha na tuhuma zako, nakosa pa kushika! Daah, sijui lkn mtoto wa miaka 8, tena wa kukutana nae w.end hadi w.end, daaah!

Umenena, hapomtoto hajafika kwenye teens - jinsi zilivyokua na challenges wallah sipatipicha.

64Bits put yourself in the shoes of this poor 8 years old kid, mwanzoni alikuaanapata mapenzi ya baba na mama kwa pamoja, ghafla maisha yakabadilika in hislittle mind anaona jinsi ulivyo divert love of his father towards his mother,believe me or not mtoto huyo anaumia na hii inamuathiri psychologically. Hivyoanahitaji mapenzi na support ya kutosha.Ondoa kabisa ile dhana eti mama yake ana mpa maneno akuchukie, kama kweli weweni mwema kwake una mapenzi ya kutoka moyoni (sio ya unafiki alimradi tu) mtoto hataaambiwe kitu gani na nani hawezi kuwa against you.


Kumbuka
1. watoto ni kama wanyama (pets) aki-sense unamapenziya kweli kwake na yeye automatically ata reciprocate. Kama akiona uko hostile tegemeathe same.
2. Watotoumri huo hupenda kujaribu/ kutest zali, aone response yako mtu mzima,ukimchekea hata kama ni mwanao wa kumzaa utavuna mabua na atakupanda kichwanikwa mfano hiyo ya kucheza mpira ndani, mwambie madhara yake kwa upole siolazima u-shout kila mara. Hakikisha siku uki-shout hata yeye ajue mh kweli hapaleo nimechemsha mama whatever s/he calls you mpaka amefoka kweli nimeharibu,atajirekebisha.
3. Pamojana udogo wake anaelewa na kusikia kila unachomuongelea either yeye au mamayake, pia anaona jinsi unapokua na mwanao wa kumzaa namna unanyobehave.

Mwisho ushauriwangu, mpende, mpende, mpende kama mwanao wa kumzaa, na umuombee kwa Mungu. Fikiriahili, kuna leo na kesho na wewe usijejikuta huyo mwanao wa kumzaa anakujakulelewa na mama wa kambo kutoka kwa baba huyo huyo (sio maombi yangu ikutokeeni angalizo tu).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…