Watoto nje ya ndoa wanaweza kupata urithi?

Watoto nje ya ndoa wanaweza kupata urithi?

Kwanza FUTA KAULI YAKO.
Hakunaga mtoto wa nje. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na wanastahili urithi wa wazazi wao iwapo watatoweka duniani.

Mathalani wawepo wanandugu wenye roho mbayaa!!!!!
 
Kwa Sheria yetu mtoto atambulike Kwa ukoo ila kwenye dini Kuna dini inawakubali ila Kuna dini inawafyeka mbal
 
Hakuja mtoto aliyekuandikia barua umzae, nyege zako ndo zilikufanya umpate huyo mtoto,

Mrithishe mtoto Mali ulizonazo,

Na hii tabia unazalisha mtu watoto unapishana na wanao njiani kama hamjuani yaan wanajua tuu yule ni baba over,

Kingine unamzalisha mtu unaogopa kumleta mwanao nyumbn kisa unamuogopa mkeo mkiwa hapa mnabwabwaja kama mbubujikwa machozi ya furaha lukasii,
 
Wakuu Je watoto wa nje ya ndoa wanahusika kwenye mirathi
Inategemea na kama wewe ni mwajiriwa wa serikalini au la, na mazingira uliyoyaandaa. Kwenye malipo yanayotoka serikalini wanahusika nayo kama uliwaorodhesha kama wategemezi wako na ni watoto wako. Na kwenye mirathi zinazoamriwa na mahakama wanakuwepo. Ila ukiacha kienyeji enyeji tu, wanachinjiwa baharini. Niliuliza PSSSF wakaniambia watoto walioingizwa kwenye mfumo wao (PSSSF) wanagawiwa 50% ya kiinua mgongo chako kama haukuacha wosia na 50% anapewa mkeo wa ndoa. Ukiacha wosia basi huo ndio utakaofuatwa kugawa mali zako.
 
Back
Top Bottom