Watoto miguu vifundo wanatibika wapelekwe hospitali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
67648948_2415012295200498_1663058070550347776_n.jpg

Watoto 3,000 katika vizazi hai huzaliwa na miguu vifundo Kila mwaka Nchini Tanzania. Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu Hospitali ya CCBRT, Cyprian Nyomoka Jijini Dar es Salaam.

"Watoto laki nane katika vizazi hai, huzaliwa kila mwaka Duniani wakiwa na miguu vifundo, huku Tanzania watoto laki tatu kwa mwaka huzaliwa wakiwa na miguu Vifundo," alisema.

Alisema changamoto ni baadhi ya wazazi kutofika kwa wakati Hospitalini CCBRT kuwapeleka watoto kupatiwa matibabu.

Alisema matibabu yanachukua miaka mpaka mitano, mtoto kurudi miguu katika hali yake ya kawaida, lakini inatakiwa mzazi afike kliniki kila anapopangiwa, kama asipohudhuria vizurí hawezi kupona.
"Mtoto aletwe mapema CCBRT ili aweze kufanyiwa matibabu na kupona kama anacheleweshwa kupatiwa matibabu Uponaji wake unakuUwa mgumu," alisisitiza.

download.jpg

Vilevile, alisema wanawashukuru Miracoseet, kwa kuwafadhili fedha ili waweze kutoa hudumabure kwa watoto ambao wanafika kupata matibabu ya miguu kifundo.

Alisema hali ya uchumi kwa baadhi ya wazazi ni tatizo linalosababisha wazazi kushindwa Kupata nauli za kutoka maeneo waliopo kufika hospitali kwa matibabu.

Kwa mujibu wa Nyomoka, CCBRT Ilianza kutoa matibabu ya miguu kifundo tangu mwaka 2001.
 
Back
Top Bottom