Watoto 147 wakutwa misikitini Kilimanjaro

Watoto 147 wakutwa misikitini Kilimanjaro

Status
Not open for further replies.

Miss X

Member
Joined
Dec 18, 2010
Posts
97
Reaction score
137
WATOTO 140 wenye umri kati ya miaka 10 na 21 wamekamatwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakilelewa katika misikiti mitatu tofauti. Taarifa zilizopatikana wilayani hapa zinasema watoto hao wamekuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, watoto hao waligundulika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Hai kupata taarifa na kuwafuatilia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, kati ya Machi 25 na 27 mwaka huu.

Taarifa hizo zimeyataja maeneo waliyokutwa watoto hao kuwa ni Misikiti ya Masjid Bilal, Masjid Othiman na Msikiti wa Kwa Kiriwe.Taarifa hizo zimesema katika Msikiti wa Masjid Bilal uliopo Mtaa wa Kibaoni wilayani hapa, walikutwa watoto wa kiume 70 wanaotoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Watoto wengine 50 wa kiume walikutwa katika Msikiti wa Masjid Othiman uliopo Mtaa wa Uzunguni ambao nao inasemekana wamekusanywa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa hizo zinasema watoto wengine 27 walikutwa katika Msikiti wa Kwa Kiriwe ambako pia walikuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam na walimu Watanzania. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthoy Mtaka, alikiri kuwapo watoto hao wilayani kwake.

"Tukio hilo lipo na wanaohusika ni watu wanaotumia mwamvuli wa dini fulani kufanya mambo yasiyofaa katika jamii. "Kwa hiyo naziomba mamlaka husika likiwamo Baraza Kuu la Waisalam Tanzania (BAKWATA) kutambua miskiti na shughuli zinazoendelea katika nyumba hizo za ibada.

"Hili lazima walifanyie kazi kwa sababu hao vijana inasemekana wanafundishwa mazoezi makali ya kareti na judo katika nyumba hizo za ibada," alisema Mtaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema atazungumzia tukio hilo leo. Kupatikana kwa watoto hao ni mwendelezo wa matukio ya watoto wanaolelewa kinyume cha sheria mkoani Kilimanjaro baada ya matukio mawili ya aina hiyo kuripotiwa hivi karibuni. La kwanza lilihusisha watoto 18 na la pili lilihusisha watoto 11 waliokutwa katika maeneo ya Lyamungo wilayani Hai.

Chanzo: Mtanzania

 
experience kwa nchi zenye matukio ya kujilipua ni kwamba mtu anayeweza kujifunga bomu na kujilipua ni yule ambaye amekulia katika mazingiza tengefu, na kuwa brainwashed kidini tangu utoto wake... kuyu hana reference ya mbayuwayu kwenye ubongo wake.....hajui hata utamu wa dunia..yeye kila kitu cha duniani ni kibaya...akiishachochewa na kukolezwa ndio anapewa bomu ajifunge ajilipue ili awahi akhera....ambako ndio kaaminishwa ndio kuna kuku za kumwaga.....
 
Acheni kutunga jamani, mi najua misikiti kibao ambayo wanapokea vijana toka sehemu mbali mbali kujifunza dini na kisha kurejea makwao......Kama kuna kitu kinatengenezwa basi mtengeneze vyema,....Mbona hamtupi taarifa ya wale watoto mliodai wamekamatwa nyumba moja huko moshi? kumbe walikuwa mayatima tena walikuwa wanaishi maisha mazuri na salama...naona kimya hadi leo.
 
Hao ni alshabab tu! Hao watoto waulizwe kama wapo waliograduate. Na wako wapi?
Dah kweli mwenzako akinyolewa we tia maji....
 
wakuu hii hatari sana maana ugaidi uwa unaanza hivi hivi,hawa watoto wanafundishwa ujasiri na mwisho wa siku watatulipua hawa. wanasema mbuyu ulianza kama mchicha
 
kuna taarifa kuwa magaidi wa IS walipanga kushambulia tz na aljazeera walisharipoti so tuwe makini.la sivyo tutakimbiana
 
unless kama wanaohusika wanahofia kutuambia ukweli lkn nahisi kama kuna njama za kuleta ugomvi wa kidini katika jamii yetu.
jamani tusiushokoe mchokoo kabla haujatuchokoa
hapa jeshim la polisi lina cha kujieleza
 
hizi imani sijui zinatoka wapi siku hizi sielewi kama maandiko ya hivi vitabu yanabadilika au sababu katika utoto wetu mpaka uzee huu hatukuwa tunaona ujinga huu na dini ni zile zile. jamani
 
Haya yetu macho, wakija wenyewe wenye kuyashughulikia watakwambia huu ni upepo tu utapita
 
acheni kutunga jamani, mi najua misikiti kibao ambayo wanapokea vijana toka sehemu mbali mbali kujifunza dini na kisha kurejea makwao......kama kuna kitu kinatengenezwa basi mtengeneze vyema,....mbona hamtupi taarifa ya wale watoto mliodai wamekamatwa nyumba moja huko moshi? Kumbe walikuwa mayatima tena walikuwa wanaishi maisha mazuri na salama...naona kimya hadi leo.


watu wanaupiga vita uislam kwa hali na mali,,,nadhani itafikia wakati mtu utaogopa ht kujitambulisha km wewe ni muislam,,, na ishafikia tayari,,,,ni hatari sana
 
Kosa ni lipi hapo? Wazazi wamelalamika watoto wao kupotea? Kupewa mafunzo ya Dini ni Kosa? Mwislam wa kweli lazima afanye mazoezi awe na afya njema... ndo maana Uislam unakataza Ulevi, Uzinzi, Uvutaji wa Sigara na vyote vyenye kudhuru Mwili... Isitoshe Uislam unahimiza kusaidiana baiana yao... Kosa ni nini? Nijuzeni tafadhali ..
 
Kosa ni lipi hapo? Wazazi wamelalamika watoto wao kupotea? Kupewa mafunzo ya Dini ni Kosa? Mwislam wa kweli lazima afanye mazoezi awe na afya njema... ndo maana Uislam unakataza Ulevi, Uzinzi, Uvutaji wa Sigara na vyote vyenye kudhuru Mwili... Isitoshe Uislam unahimiza kusaidiana baiana yao... Kosa ni nini? Nijuzeni tafadhali ..

Kama ni mafunzo ya ukakamavu kwanini hawakufunza mafunzo ya soka ambayo yana ajira pia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom